Venezuela Criss

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
VENEZUELA TAIFA LILOBARIKIWA MAFUTA NA GESI, LILIASISIWA NA SIMÒN BOLIVAR, LIKAJENGWA NA HUGO CHAVEZ SASA LINATEKETEA MIKONONI MWA NICOLAS MADURO.

Na. Comred Mbwana Allyamtu
Thursday -14/3/2019.
Marangu -Kilimanjaro, Tanzania.

Niliombwa na rafiki yangu Advocate Jeremiah Odinga kufanya uchambuzi yakinfu juu ya hali ya mambo katika taifa la Venezuela. Kufatia ombi lake pamoja na wadau wengine ambao wamekua wakiniomba niandike kitu juu ya siasa za Caracas zinazo iandama Ikulu ya "Palace de Naćional Florais" iliyopo kwenye viunga vya jiji la Caracas nchi Venezuela, dhidi ya Juan Guaido na washirika wake. Nimetekeleza ombi hilo leo, huku nikibakiza deni moja juu ya ombi la ndugu yangu John Anajus ambae ametaka niandike juu ya kile kinachoendelea baina ya mgogoro wa "Rwanda na Uganda".

Sasa turejee mpaka Caracas Venezuela.....

Eneo ambalo sasa linajulikana kama Venezuela miaka 419 huko nyuma lilikuwa ni koloni la Hispania, Hispania yenyewe ilifika eneo hilo na kuanzisha utawala wake mwaka wa 1522, pamoja na upinzani kutoka kwa watu wa kiasili wa eneo hilo ambao Wahispania waliwaita Wahindi wekundu (Red Indian) bado Uhispania ilifanikiwa kuanzisha himaya yake eneo hilo. Lakini kufatia vuguvugu ya ukombozi na uhuru hatimae mwaka wa 1811 Venezuela Ilipata uhuru wake na kuwa mojawapo ya eneo la kwanza kabisa la koloni la Kihispania na eneo la kwanza Amerika kusini kutangaza uhuru wake, pamoja na kijitangazia uhuru mapema, Venezuela chini ya Simon Bolivar haikulizika na uhuru wake, iliendelea na harakati za ukombozi katika makoloni mengine ya kihispania ndani ya Amerika ya kusini mpaka mwaka 1821 ilipokomboa eneo lote la himaya ya Uhispania iliyokuwa ikiitwa Granada Colombia.

Wakati wa vita ya ukombozi iliyo ongozwa na mwanamapinduzi anae heshimika mno Amerika ya kusini, na kutazamwa kama baba wa ukombozi na mwasisi wa mataifa ya Amerika ya kusini Simon Bolivar, katika vita ile ya ukombozi Bolivar alifanikiwa kuyashinda majeshi ya Uhispania katika maeneo ya Peru, Colombia, Bolivia, Panama, Ecuador, Nicaragua, Chile kaskazini, Costa Rica na Venezuela. Hivyo baada ya ushindi wa maeneo hayo na kuyatangazia uhuru maeneo hayo ambayo yalikuwa yakitawaliwa na Uhispania kama makoloni yake, wazo la kuyaunganisha maeneo hayo ilizaliwa katika "Kongamano la Angostura" lilo fanyika mwaka 1819, baada ya uhuru wa maeneo hayo yote kufanikiwa mwaka 1820 Bolivar aliyaunganisha na kuunda jamuhuri moja ya shirikisho iliyo itwa "Shirikisho la Colombia" (Glan Colombia) muungano huo ulifaatia baada ya kongamano lingine liloitwa "Kongamano la Càucuta" la mwaka 1821, kupitia kongamano hilo mataifa yote yaliungana na kuunda dola mmoja Ili kupambana na tishio la uvamizi wa Uhispania, Bolivar aliamua kuiita nchi mpya Colombia kufatia heshima ya mgunduzi wa kihispania Cristopher Columbus aliye fika Amerika ya kusini mwaka 1492.

Jamuhuri mpya ya Gran Colombia ilijumuisha nchi za Peru, Colombia, Bolivia, Panama, Ecuador, Nicaragua, Chile kaskazini, Costa Rica na Venezuela. ambapo makao makuu ya shirikisho hilo yaliwekwa Bogotá Colombia ambapo ni mji mkuu wa Colombia mpaka sasa. Simon Bolivar alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa shirikisho hilo mwaka 1821 katika kongamano la Càcuta kufatia kupigiwa kura na wajumbe wa baraza hilo lilojumuisha wakombozi na wachaguzi (electro voters) mbali mbali na Francisco de Paula Santander, alichaguliwa kuwa makamu wa raisi, hata hivyo jamuhuri hiy ya Gran Colombia ambayo wakati wa kuundwa kwake Ilikuwa tishio na nchi ya kifahari zaidi katika Amerika ya kusini mpaka kufika John Quincy Adams, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani ambae baadae alikuja kuwa Rais wa sita wa Marekani, alipata kusema "taifa hilo jipya ni moja ya mataifa yenye nguvu zaidi duniani". Utukufu wa taifa hilo, ulioongezwa zaidi na sura ya ukombozi na uzalendo wa Bolívar.

Simon Bolivar alivutiwa zaidi na mawazo ya umoja na utaifa ulio jaa harakati za uhuru, alitaka kuona Amerika ya kusini huru yote inaungana na kuunda dola moja, huko Cuba chini ya mwanamapinduzi Josè Mart na kule Jamhuri ya Dominika pamoja na Puerto Rico, ambazo nazo pia zilijaribu Kufata nyayo za Bolivar za kuunda shirikisho lakini wailishimdwa kufanikiwa. Gand Colombia ambayo nayo pia muungano wao haukudumu, kwani uli dumu kwa miaka Kumi (10) tu na baadae kusambaratika, kufatia mgawanyiko wa kisiasa ulijitokeza kati ya wale waliounga mkono Katiba ya Cúcuta na makundi mawili yaliyotaka marekebisho ya Katiba ya Càcuta.Mgawanyiko huo misingi yake Ilikuwa ni kupunguza madaraka kwenye nchi kuwa jamhuri ndogo na kuziongezea madaraka nchi zilizo ndani ya shirikisho Ili kudumisha umoja, kikundi hiki kiliongozwa na Makamu wa Rais Francisco de Paula Santander, wakati upande wa pili waliunga mkono mfumo wa shirikisho uliokuwepo wa kuwa na mamlaka katika serikali kuu na kuziacha nchi washiriki kuwa maeno ya majimbo, upande huu uliongozwa na Rais Simón Bolívar. Hawa viongozi wote wawili walikuwa wameungana katika vita dhidi ya utawala wa Kihispania wakati wa vita ya ukombozi, lakini mwaka 1825, tofauti zao zilikuwa kubwa mno kwani ziliugawa umma na kusababisha kutokuwepo na utulivu wa kisiasa tangu mwaka huo.

Kufatia Mgogoro huo Gran Kolombia ilifutwa mwaka wa 1831 kutokana na tofauti za kisiasa zilizopo kati ya wafuasi wa shirikisho (Federist) na wale wa uongozi (Republicanist), pamoja na mvutano wa kikanda kati ya watu waliokuwa ndani ya shirikisho hiyo ilipelekea kuvujika kwa taifa hilo na kuzaliwa nchi za Colombia, Ecuador, Chile, Paraguay, Bolivia na Venezuela. Hii Panama ilitenganishwa kutoka Colombia mwaka 1903, huku Costa Rica ilijiunga na Marekani kama Jimbo lake la nje mwaka 1901.

Simòn Bolivar, mwasisi na mwanamapinduzi wa Venezuela na Amerika ya kusini...
Je Simòn Bolivar ni nani?

Simòn Bolivar ni mwanamapinduzi mkubwa sana huko Amerika ya kusini, ni mwasisi wa mataifa Saba na hupewa heshima kuliko kiongozi yoyote yule huko kusini mwa Bala la Amerika kusini, yeye na wenzake Sita yani Simòn Bolivar wa Grand Colombia, Francesca Martin wa Argentina, Uruguay,Chile na Jose Marti wa Cuba, Tousant Lòventure wa Haiti pamoja na Fidel Castro wa Cuba na Che Guevara wa Argentina. Hawa huitwa 6 G.A.L (6 Great American liberators)

Huyu Simòn Bolívar alizaliwa July 24, 1783 katika familia tajiri, familia ya Criollo Fransisco Puerto Vallarta yenye asili ya Hispania, na kama ilivyokuwa kawaida kwa familia za wamiliki wa mashamba makubwa na watumwa zilikuwa ni familia za tabaka la juu katika kipindi hicho, Bolivar alizaliwa katika eneo la Caracas, katika kitongoji cha Cruz Ndani ya eneo la Venezuela ambayo kipindi hicho Ilikuwa ni sehemu ya himaya ya Uhispania katika koloni huko Amerika ya kusini (New Granada). Bolivar alipelekwa kusoma nje ya nchi huko Hispania akiwa na umri wa miaka 16 Ili kupata elimu na baadaye akahamishiwa Ufaransa kujiunga na elimu ya chuo kikuu. Wakati Bolivar akiwa Ulaya, alianzisha harakati zilizobeba mawazo ya Mwangaza kwa watu wa Amerika ya kusini kwa lengo la kutaka kujikomboa kutoka mikononi mwa ukoloni. Harakati hizo za Bolivar zilisababishwa na vuguvugu la uhuru alilo likuta huko ulaya kwa mataifa mengi yakitaka kujitawala na kupinga kukaliwa na mataifa yenzao, kufatia hali hiyo ikachochea mageuzi katika fikra za Simòn Bolivia za kutaka kujitawala.

Fikra hizo ambazo baadaye zilimshawishi Bolivar kurudi nyumbani Venezuela kwenda kudai uhuru Amerika ya Kusini. Kufatia harakati hizo akapata ushawishi kutoka Uingereza, Bolívar alianza vita yake ya uhuru mwaka 1808. Vita ya uhuru wa Venezuela baadae ikazaa vita ya ukombozi ya eneo lote la New Granada eneo ambalo lilikuwa ni himaya ya Uhispania, vita hiyo iliimarishwa mpaka ushindi ulipo patikana katika vita vya mwisho vya Boyacá tarehe 7 Agosti 1819. Baada ya ukombozi wa eneo la Venezuela, Colombia, Ecuador, Panama na Chile kaskazini ambayo Ilikuwa sehemu ya New Granada, Bolivar baadaye alianzisha kikao cha kitaifa kilicholenga kuunganisha nguvu katika nchi alizo zikomboa, Kufuatia ushindi huu juu ya utawala wa Kihispania, Bolívar alishiriki katika kongamano la umoja wa kuunganisha mataifa hayo kwenye kongamano la kwanza la mataifa huru ya Amerika ya kusini huko Angostura, baada ya azimo la Angostura na lile la Càcuta, shirikisho la Gran Colombia, liliundwa ambapo Bolivar aliteuliwa kuwa rais kutoka 1819 hadi 1830.

Pia akiwa rais alivamia maeneo ambayo yalikuwa bado yamekaliwa na Uhispania ambayo yalikuwa ayajapata uhuru na kuwafurumusha Wahispania huko Ecuador, Peru , na Bolivia, ambayo hii Bolivia ilpewa jina kwa heshima yake. Baada ya kuyakomboa maeno hayo aliyaunganisha kwenye Gran Colombia (Venezuela, Colombia, Panama na Ecuador) Bolivar aliunganisha nchi hizo kuwa nchi moja alilenga kuwa na Amerika yenye nguvu dhidi ya vitisho kutoka Hispania inayoweza kuivamia tena, pia alitaka kukabiliana na ubepari kutoka nchi za Ulaya. Katika utawala wake Bolívar ilitawala eneo la shirikisho la Grand Colombia lilo kuwa na ukubwa kutoka mpaka wa Argentina hadi Bahari ya Caribbean.

Shirikisho hilo lilivunjika mwaka 1831. Baada ya kuvujika kwa Gran Colombia Simòn Bolivar alikuwa ameshafariki dunia mwaka mmoja nyuma, yani 1830. Kifo chake na kutokuwepo kwake kuliongeza nguvu upande wa waliotaka kujitenga kupata nguvu.Venezuela nchi yake aliyo zaliwa na mahali alipo anzisha harakati zake za ukombozi imekuwa ikiomba mwili wake urudishwe Venezuela kwa mazishi lakini Colombia imekuwa ikikata na kudai kuwa kwao ni baba wataifa hivyo kuzikwa kwao ni halali, huko Venezuela aliteuliwa kuwa mkombozi na baba wa taifa kwa heshima na ndivyo Mataifa mengine ya ile iliyokuwa Glan Colombia yalivyofanya kwa kumpa hadhi ya baba na mwasisi wa mataifa yao kwa heshima. Bolívar alipewa cheo cha Field Marshall hii ni kutokana na kupigana vita nyingi zaidi, alipigana vita 472 na kishinda vita zote hizo, na kutajwa kuwa ndio mtu aliye pigana vita nyingini zaidi katika bala la Amerika ya kusini na kaskazini, wakati wa vita hiyo ya ukombozi alisafiri kwa farasi umbali wa kilomita 123,000, mara 10 zaidi kuliko Anibal, mara tatu kuliko Napoleon, na mara mbili zaidi ya Alexander Mkuu.

Bolívar anachukuliwa kama icon ya kitaifa katika sehemu kubwa ya Amerika ya Kusini ya kisasa, na anachukuliwa kuwa mojawapo ya mashujaa wa uhuru wa Puerto Rico wa karne ya 19, hupewa heshima pamoja na José de Francisca San Martín, Josè Mart au Francisco de Miranda na wengine. Katika mwisho wa maisha yake, Bolívar alitoa hotuba maarufu sana huko Colombia iyoitwa "Zimwi la Utengano limetutafuna" katika hotuba hiyo aliyosema "Wote walio hudumu mapinduzi wamelima bahari." Bolivar alifariki mwaka 1830 Ilikuwa ni tarehe 17/12/1830, kwa ugonjwa wa Kifua kikuu (Tuberculosis)

Venezuela, taifa lilobarikiwa mafuta na gesi....
Lifahamu taifa la Venezuela.

Venezuela Ilipata uhuru wake wa kwanza mwaka 1811. Lakini uhuru kamili kama nchi ulipatikana mwaka 1830 baada ya kuvunjika kwa Grand Colombia. Taifa hili linapatikana katika bala la Amerika ya kusini, eneo la mashariki mwa Amerika kusini. Nchi ni jamhuri na rais ndio mkuu wa nchi ambae pia ndio mkuu wa shirikisho linalojumuisha majimbo 23, Wilaya ya mji mkuu wa Caracas haina jimbo la utawala kama Washington DC kwa Marekani, na shirikisho la Venezuela ni pamoja na eneo lote la Guyana magharibi ya Mto Essequibo, Jumla ya ukubwa wake ni kilomita 159,500 za mraba (61,583 sq mi). Venezuela ni miongoni mwa nchi za Amerika ya Kusini, raia wengi wa Venezuela wanaishi miji ya kaskazini, hasa katika mji mkuu wa Caracas ambao pia ndio mji mkubwa zaidi nchini Venezuela.

Katika karne ya 19, Venezuela alipata shida ya kisiasa kwa kukumbwa na mapinduzi, utawala wa kidikteta, uvamizi wa mataifa ya magaharibi hasa Marekani na utawala wa Kiimla (Autocracy), tawala hizo zilizo pachikwa na Washington zilikuwa zikitawala kwa nguvu za kijeshi mpaka katikati ya karne ya 20. Tangu 1958, nchi ya Venezuela Ilianza kupata mwelekeo mpya kisiasa kwani imekuwa na mfululizo wa serikali za kidemokrasia japo zimekuwa zikikumbwa na kashfa za ufisadi na rushwa za kutupa na hii inatokana na tawala hizo kuwa vibaraka wa marekani. Mwaka 1989 Venezuela ilikumbwa na mauaji mabaya yaliyo fahamika kama Caracazo, mauaji hayo yalifatia kupinga utawala wa Rais Carlos Andrés Pérez ambae alikuwa kibaraka wa Marekani anaetajwa kama kiongozi muharibifu wa nchi na mfujaji wa fedha za umma ambae alilifanya taifa hilo kuwa masikini wa kutupwa na kusababisha wimbi kubwa la wavenezuela kuelekea marekani kusaka maisha bora.

Mafuta nchini Venezuela yaligunduliwa mwanzoni mwa karne ya 20, na leo, Venezuela ndio nchi ambayo ina hifadhi kubwa zaidi ya mafuta yanayojulikana duniani na imekuwa moja ya nchi duniani ambayo ni wauzaji wakubwa wa mafuta wa dunia. Data hizi ni kwa mujibu wa utafiti wa OPEC, shirika la nchi zinazozalisha mafuta ya petroli duniani, shirika hilo linasema kwamba akiba ya mafuta iliyosalia katika ardhi ya dunia mpaka kufikia mwaka 2017 ni takribani mapipa trilioni 1.7. Na kiasi hicho Venezuela pekee inahodhi robo ya mafuta yote duniani huku Venezuela pekee ikiwa na asilimia 20% ya mafuta yote ambayo hayajachimbwa duniani, ikifatiwa na Saudi Arabia 18%, kisha Canada 13% na Iran 9%.Hapo awali, nchi hiyo ilikuwa na umasikini na ufukara wa kutisha mpaka mwaka 2000 pale bei ya mafuta Ilipo fufuka ambapo Venezuela ilipata fedha nyingi za kigeni na kupelekea kufufuka kwa Uchumi chini ya Serikali ya Hugo Chávez, Hugo Chavez katika utawala wake ilianzisha sera za ustawi wa jamii ambazo zilianza kukuza uchumi wa Venezuela na kuongeza matumizi ya pesa kwenye kuboresha huduma za kijamii, kupunguza uhaba wa Chakula na umaskini katika miaka ya mwanzo ya utawala wake.

Hugo Chavez, mshosholist na muumini wa itikadi ya Ubolivarian....
Je Hugo Chavez Raphael Frias ni nani?

Huyu Hugo Chavez ni shujaa wa itikadi ya Ujamaa mpaka kifo kilipomchukua Machi 5, 2013. Watu wenye imani isiyoyumba ya falsafa zote za Mrengo wa Kushoto (Left-Wing) duniani kote, kwao Chavez alikuwa jemedari kinara dhidi ya Ubepari. Chavez aliuchukia ubepari na aliijenga Venezuela kuwa taifa la Kijamaa kupitia vyama vya Movement for the Fifth Republic kati ya mwaka 1997 mpaka 2007 kisha United Socialist Party kuanzia mwaka 2007 hadi roho yake ilipotengana na mwili wake.

Historia ya Hugo Chavez ndani ya Venezuela ni ya kutukuka mno, anaheshimika kama mkombozi na Simòn Bolivar wa kizazi cha leo, kisiasa Hugo Chavez alianza kuchomoka mwezi Desemba 17, 1982, mwaka huu kwa Chavez ni muhimu mno katika historia ya kuelekea ikulu ya Caracas, kwani mwaka huu Chavez aliasisi Vuguvugu la Kimapinduzi la Wana-Bolivar-200 (Revolutionary Bolivarian Movement-200) ambayo kwa kifupi hutambulika kama MBR-200. Vuguvugu hilo, Chavez alilianzisha kwa kushirikiana na maofisa wenzake wa jeshi, walio itwa Felipe Carles na Jesus Hernandez. Jina Bolivar, walilitumia kama heshima kwa Simon Bolivar, ambaye alikuwa mtawala wa kijeshi na kisiasa, aliyefanya kazi kubwa kuasisi mataifa ya Venezuela, Bolivia, Colombia, Ecuador, Peru na Panama katika miaka ya mwanzo ya Karne ya 19.

Maono na nadharia za kiutawala za Bolivar ambaye alijulikana pia kama El Libertador, ndiyo sababu ya Chavez na wenzake kuita harakati zao kuwa Vuguvugu la Kimapinduzi la Wana-Bolivar. Februari 4, 1992, Chavez akisaidiwa na Serikali ya Cuba, chini ya hayati Fidel Castro, walifanya jaribio la kwanza la mapinduzi ya kumwondoa aliyekuwa Rais wa Venezuela, na mfuasi mkubwa wa Marekani, Carlos Perez. Kushindwa kwa jaribio hilo, kulisababisha Chavez na wenzake wafungwe jela. Novemba 27, 1992, jaribio la pili tena lilifanyika kumwondoa madarakani Perez, wakati Chavez akiwa jela. Vijana watiifu wa MBR-200, walipokea maagizo kwa Chavez, aliyesuka mpango akiwa jela. Hata hivyo, jaribio hilo pia lilikwama. Julai 1997, MBR-200 walibadili jina na kujiita Movement for the Fifth Republic (MVR) ili kitambulike kuwa chama cha kisiasa, lengo likiwa kumwezesha Chavez kugombea Urais katika Uchaguzi wa Rais wa Venezuela mwaka 1998.

Uchaguzi ulifanyika Desemba 6, 1998, Chavez alishinda kwa asilimia 63.5 dhidi ya aliyekuwa Gavana wa Jimbo la Carabobo, Henrique Romer. Kuanzia hapo, Chavez aliamua kuifanya Venezuela kuwa nchi ya Ujamaa, akifuata nyayo za Castro wa Cuba ambaye alikuwa Mkomunisti kindakindaki na mfuasi wa falsafa za ‘manabii’ wa Ukomunisti, Carl Marx na Vladimir Lenin, yaani Marxist-Leninist.Chavez alijitangaza kuwa Marxist kisha kutengeneza ushirika na Serikali za Kijamaa za Evo Morales (Bolivia), Rafael Correa (Ecuador) na Daniel Ortega wa Nicaragua.

Hata hivyo Hugo Raphael Chavez Frias alizaliwa julai 28,1954 na amekalia kiti cha urais wa Venezuela tangu mwaka 1998, Chavez mzaliwa wa mji wa Sabaneta, ni mtoto wa pili wa wazazi ambao walikuwa walimu. Chavez ni mchanganyiko wa kiafrika kwa mama na wahindi wa Amerika ya kusini kwa baba. Alikulia katika nyumba ya makuti kabla ya yeye na kaka yake mkubwa Adam kuhamia kwa bibi yao mbali na wazazi wao, akiwa huko, Chavez alipenda sana kuchora, kuimba na kucheza mpira. Alijiunga na shule ya Julian Pino na baadae elimu ya sekondari katika sekondari ya Daniel Florencio,alipofikisha umri wa miaka ya 17 akajiunga na chuo cha jeshi alikohitimu mwaka 1975. Alilitumikia jeshi kwa miezi kadhaa na kisha kujiunga na Chuo Kikuu cha Simon Bolivar huko Caracas kuchukua shahada ya mambo ya siasa lakini alishindwa kupata shahada kufatia changamoto za kimaisha. Akiwa chuoni, Chavez pamoja na baadhi ya wanafunzi wenzake walipenda siasa na kuhusudu falsafa za mwanamapinduzi wa Venezuela Simon Bolivar na rais wa zamani wa Peru ,Juan Velasco Alvarado. Katika utumishi wake jeshini kwa miaka 17 alishika nafasi mbalimbali hadi kufikia ngazi ya Luteni Kanali, alitumika kama mwalimu wa mambo ya kijeshi na alipendwa na wanafunzi wake kwa staili yake ya ufundishaji, akitumia muda wake mwingi kuiponda serikali ya Venezuela.

Jambo ambalo Hugo Chavez hatasahau ni pale mkuu wa majeshi Lucas Rincon Romero Mwaka 2000 alipo utangazia umma kwamba Chavez amekubali kujiuzulu na kwamba anashikiliwa katika makao makuu ya jeshi, huku Pedro Carmona akiwa Rais katika kipindi cha mpito, mapinduzi haya baridi yalifatia mwaka mmoja tu Hugo akiwa madarakani. Jambo la kwanza alilofanya Carmona baada ya mapinduzi hayo ni kuongeza uzalishaji wa mafuta, Ni kama vile mkuu wa majeshi hakujipanga vyema na bila shaka alisahau nguvu na ushawishi wa Chavez,Siku mbili baada ya Carmona kutangazwa Rais ,wafuasi wa Chavez walikuja juu na kuleta ushindani mkubwa. Askari waaminifu wa Chavez wakaingia vitani na kufanikiwa kulitwaa jengo la Rais na Usiku wa Aprili 13, wakafanikiwa pia kumpata Chavez kwenye ngome ya jeshi na kumrudisha madarakani, pamoja na kwamba Romeo aliasi ,cha kushangaza ni kwamba Chavez alimrudishia cheo chake na mwaka uliofuata akamtangaza kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, wapinzani wakasema kuwa kitendo cha Chavez kumrejesha Romero madarakani ni ishara tosha kuwa hayakuwa mapinduzi ya dhati, bali ni mchezo ulio sukwa na wawili hao.

Nje na hayo katika ufufuaji wa uchumi, Hugo mara baada ya kuwa Rais alipendekeza katiba mpya ambayo iliongeza haki kwa makundi ya wanyonge na ni kwa kupitia katiba hiyo, alihakikisha elimu inatolewa bure kuanzia ngazi ya chekechea hadi Chuo Kikuu, elimu Ilikuwa bure na alihakikisha pia chakula kinapatikana kwa kusambaza pembejeo vijijini na kuhakikisha masoko ya mazao ya shamba ni ya kutosha baada ya shakula kuwa cha kutosha, alihakikisha pia huduma ya afya inatolewa bure, aliomba madaktari toka Cuba, urafiki wake na Fidel Castro alipewa madaktari kadhaa ambao waliingia Venezuela kuwatibu watu bila gharama. Kubwa zaidi, Hugo alianzisha mpango wa ujenzi wa makazi kwaajili ya watu wa tabaka la chini aliyo yaita "Camino eśtat" ambapo katika hili alitumia utajiri wa mafuta waliyonayo kulifanikisha. Mpango huu alio anzisha Hugo uliwanufisha wa-Venezuela zaidi ya familia Milioni 2. Akaanzisha ruzuku itokanayo na mafuta kuwalipa watu wazima wasio jiweza. Kufatia hatua hiyo, WaVenezuela walimchagua tena mwaka 2000 kuwa Rais kwa ushindi wa kishindo.

Kipindi hiki, Hugo alianzisha mfumo wa misheni ya Kibolivarian, alianzisha mfumo wa halmashauri za kijamii, alianzisha vyama vya ushirika vilivyokuwa vinasimamiwa na wafanyakazi pia alifanikiwa kutaifisha viwanda muhimu kwa maslahi ya Taifa. Kimsingi alisimamia kile alichokuwa anakiamini. Kutokana na mafanikio hayo wapinzani wake walijawa hofu na kueneza propaganda ya kuwa Hugo anamomonyoa uwakilishi wa kidemokrasia na kujiongezea madaraka. Jambo ambalo mataifa ya magaharibi yakiongozwa na Marekani yaliishutumu vikali serikali ya Hugo Chavez. Wapinzani wa Hugo hawakuishia tu kueneza propaganda chafu dhidi yake bali mwaka 2002 walitaka kumpindua kijeshi na wakashindwa. Pia mwaka 2003 kwa msaada wa shirika la kijasusi la Marekani CIA, walitaka kumwondoa tena madarakani kwa kura ya maoni lakini walishindwa tena.

Uhodari wake ulimfanya mwaka 2006 kuchaguliwa tena kuwaongoza WaVenezuela Ili aweze kusimamia utajili wa taifa hilo lenye utajili wa mafuta na gesi. Mwaka 2007 Alianzisha chama Kipya kiitwacho United Socialist Party of Venezuela-PSUV. Hiyo ndiyo sababu ukimgusa Chavez, unaweza kukutana na hasira za wafuasi wa itikadi za Mrengo wa Kushoto. Misimamo ya Chavez dhidi ya Marekani ambalo ni taifa kiranja la Ubepari duniani, ni jambo ambalo humfanya atetewe na Wajamaa kokote duniani

Chavez aliugua matatizo ya saratani ya mapafu, alisumbuliwa tatizo hili kwa miaka miwili mfululizo, na matibabu yake mwanzoni alipatiwa nchini Cuba, lakini hatimae March 5,2013 alifikwa na mauti akiwa Hospitali ya Jeshi, Caracas, Venezuela na kuzikwa kwa heshima kubwa katika makaburi ya kitaifa katika eneo la Cuartel de la Montana . Hata sasa, mwili wake ukiwa umepumzishwa kwenye makaburi ya Cuartel de la Montana, yaliyopo Caracas, Venezuala. Chavez anakumbukwa kama mwasisi wa Serikali ya Bolivarian, serikali ambayo sasa inaongozwa na Nicolas Maduro, mfuasi mwingine wa Chavez ambae anakumbwa na Zimwi la Wabepari wanao pania kumgoa madarakani.

Nicolas Maduro, Mshosholist mwingine anae andamwa na njama za mapinduzi dhidi yake...
Je Nicolas Maduro Moros ni nani?

Nicolas Maduro ni rais wa 46 wa Venezuela, kwa sasa ni rais aliyopo kwenye mgogoro wa kimadaraka (presidential disputed) na rais wa bunge la nchi hiyo Juan Guaido ambapo wote wamejitangaza marais wa taifa hilo na kupata wafuasi kidplomasia jambo ambalo limeendelea kuchochea vurugu ndani ya nchi hiyo. Maduro mwenye miaka 56 amezaliwa November 23,1962, katika wilaya ya Caracas kitongoji cha Guerra kilichopo kati kati ya jiji la Caracas.

Maduro Moros hakupata elimu sana kufatia uwezo wa maisha ya familia yake, hivyo alipo maliza elimu ya sekondari alijiunga na shughuri za udereva wa mabasi, baadae alijiunga na vyama vya ushirika vya wafanyakazi mpaka mwaka 2000 alipochaguliwa kuwa mbunge wa Caracas. Maduro alitajwa kuwa mshirika wa karibu wa Hugo Chavez na ghafra mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Waziri wa mashauriano ya kigeni wa Venezuela mpaka mwaka 2012 alipoteuliwa kuwa makamu wa rais ambapo alishika nafasi hiyo ya makamu wa rais mpaka 2013 alipo kaimu nafasi ya urais kufatia kifo cha Hugo Chavez.

Nicolas Maduro toka achukue kijiti toka kwa Hugo Chavez kupitia uchaguzi wa April 14 2013, amekuwa kwenye wakati mgumu kufatia vita kubwa anayopambana na mataifa ya kibepari. Vikwazo vimeongezwa maradufu na Marekani nchini Venezuela jambo linalo ongeza ugumu wa maisha ndani ya Venezuela, umasikini umeongezeka na ukosefu wa huduma muhimu limekuwa jambo la kawaida katika utawala wake. Migomo na Maandamano ya kila siku imekuwa maisha ya Wavenezuela kupinga utawala wake. Sera zake zimeonekana kayumba na kushindwa kupambana na uchumi wenye vikwazo vingi jambo ambalo mtangulizi wake Hugo Chavez alifanikiwa, usalama umezorota katika maeneo mengi ya nchi ya Venezuela huku raia wengi wakiikimbia nchi hiyo kuelekea Marakeni na Brazil kutafuta unafuu wa maisha. Mgogoro wa Maduro na mataifa ya kibepari yaliongezeka mwaka 2015 pale eneo jipya la mafuta lilipo guduliwa katika eneo la Guyana eneo ambalo Venezuela hudai ni eneo lake toka mwaka 1879.

Sababu kubwa ya muendelezo wa mgogoro baina ya serikali ya Venezuela na ile ya Marekani ni utajili wa mafuta na gesi inayopatika Venezuela, ikumbukwe kuwa nchi ya Marekani ndiyo inaongoza kwa matumizi makubwa ya mafuta duniani, na hivyo kuongoza kampeni ya kimataifa kutaka bei ya mafuta ishuke.hii inatokana na kuwa bei ya mafuta upanda kutokana na Venezuela ndio taifa la kwanza linalouza mafuta mengi kwenye soko la dunia hivyo limekuwa na turufu ya kupanga bei ya mafuta kwenye soko hilo jambo ambalo humuumiza kichwa sana taifa la Marekani. Jambo hilo ndiyo imeathiri mno uchumi wa nchini Venezuela, ambayo ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uuzaji wa mafuta kwenye soko la dunia. Venezuela ikiwa na shehena kubwa ya mafuta ambayo hayajachimbwa ardhini na pia ikiwa jirani na Marekani, utawala wa Washington umekuwa ukiitolea macho nchi ya Venezuela kwa muongo miwili sasa, hivyo kwa miaka mingi imekuwa mlengwa wa kampeni hiyo ya Marekani kutaka bei ya mafuta ipunguzwe.

Ushawishi wa Marekani dhidi ya kuishambulia serikali ya Caracas inayoendelea sasa nchini Venezuela kutaka kuuondoa madarakani utawala wa Bw Nicholas Maduro (56) wenye kufuata mrengo wa siasa za Kikomunisti, na badala yake kumuunga mkono mpinzani wake mkuu ambaye ni Bw Juan Guaido (35), kiongozi wa bunge imetafsiliwa ni kama hatua mojawapo kwelekea kutaka kukamata siasa na uchumi wa nchi hiyo. Guaido ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani akiwa na Shahada ya Utawala, ndiye kinara katika mapambano haya yanayoungwa mkono na Marekani dhidi ya Maduro ambae ametaka Maduro kuachia nchi kwa madai kuwa taifa hilo limemshinda.

Mzimu wa Juan Guaido, dhidi ya Nicolas Maduro na pepo la magaharibi katika siasa za Caracas.....
Je Juan Gerardo Guaido Màrquez ni nani?

Juan Guaido ni mbunge kutoka jimbo la Vargas katika bunge la Venezuela, lakin pia ni rais wa bunge la taifa hilo,kupitia chama cha Centrist social-Democratic Popular Will, chama ambacho amekianzisha toka mwaka 20015. Juan amezaliwa kwenye familia yenye uwezo wa kiuchumi akitoka kwenye familia ambayo baba yake alikuwa pairot.

Juan alizaliwa July 28, 1983, huko La Guaira Venezuela, amekuwa mpinzani mkubwa wa Nicolas Maduro na amekuwa akiungwa mkono na mataifa hasimu ya Venezuela. Guaido ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani akiwa na Shahada ya Utawala, amekuwa mwiba katika serikali ya Venezuela. Venezuela ni miongoni mwa nchi ambazo zimekumbwa na majaribio mengi ya mapinduzi yasiyozaa matunda nyuma yake yakiwa yameratibiwa na shirika la ujasusi la Marekani(CIA). Na hata jaribio la sasa serikali ya Washington kwa uratibu wa CIA umeonekana kutia mkono wake.

Kufatia mitufuano ya sasa ambao unatishia usalama wa Venezuela na serikali ya Caracas chanzo chake kiliibuka mnamo tarehe 23 Januari 2019, pale kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido(36) alipo jitangaza kwamba yeye ndiye kiongozi wa mpito wa Venezuela(Interim president) na baada ya tamko hilo tuliona uungwaji wake mkono kutoka kwa mataifa ya magharibi. Kauli nyingi zinazoambatana na vitisho zimekuwa zikitolewa kila uchao na viongozi wa mataifa ya magharibi hasa Marekani kumtia hofu Nicolas Maduro aweze kung'atuka madarakani na kumuachia nchi Guaido jambo ambalo Maduro amekataa na kulaani jambo hilo huku akiyashutumu mataifa hayo kuingilia maswala ya ndani ya Venezuela.

Marekani na nchi za magaharibi zimeendelea kutia petrol kwenye Mgogoro huu hasa pale baada Guaido kurejea nchini kwake Venezuela mapema mwezi huu akitokea Ecuador mshauri mkuu wa masuala ya kiusalama wa ikulu ya Marekani balozi John R. Bolton kupitia akaunti yake ya Tweeter aliandika ."Rais Guaido amerejea salama nchini kwake kwenda kulisukuma gurudumu la demokrasia kwa ajili ya manufaa ya watu wake. Marekani inamuunga mkono yeye pamoja na bunge lake. Lazima ahakikishiwe usalama wake, Dunia inatazama" Kauli hii kutoka kwa bw Bolton inaweza ikaleta madhara makubwa sana kwa uongozi wa Maduro. Na kuchochea mdororo wa kisiasa ndani ya Venezuela.

Chanzo cha Mgogoro huu wa sasa baina ya Juan Guaido na Nicolas Maduro ulizuka baada ya tarehe 20 may 2018 pale wananchi wa taifa la kishosalist la Venezuela walipo piga kura katika uchaguzi mkuu wa kidemokrasia ambapo Rais Nicolas Maduro alichaguliwa tena kwenye awamu ya pili ya muhura, kuliongoza taifa hilo kwa kipindi kingine cha miaka 6. Kufatia ushindi wa Maduro, hatimae Tarehe 19 Januari 2019, Rais Maduro aliapishwa kuwa Rais wa Venezuela baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa urais kwa kujinyakulia jumla ya kura Milioni 5.8 dhidi ya mshindani wake na gavana wa zamani aitwaye Henrico Falcon kutoka upinzani aliyepata kura Milioni 1.8. Falcon ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha kijamaa cha Maduro na pia gavana wa zamani alihamia upinzani mwaka 2010 na kugombea urais dhidi ya Maduro kwenye uchaguzi ambao ulilalamikiwa na mataifa ya magaharibi.

Katika uchaguzi uliofanyika tarehe 20 May 2018 ulikuwa ni uchaguzi ambao Marekani na nchi za kibepari yenye maslahi na rasilimali za Venezuela hasa mafuta waliwekeza nguvu kubwa kuhakikisha kuwa Rais Nicolas Maduro anaondoka madarakani. Kushindwa kufanikiwa katika mpango huo wameamua kuonesha wazi kuto kuuitaji utawala wa Maduro. Vikwazo na hali ngumu ya kiuchumi imeanza kuwagawa wananchi wa Venezuela, na marekani inatumia wakati huu kuvuruga hali ya utulivu ndani ya Venezuela Ili kuichafua serikali ya Maduro, raia wengi wa Venezuela wamesahau tabia ya mabepari ilivyo watesa zaidi ya miaka 200 huko nyuma, na namna vita aliyokuwa akiipigana Hugo Chávez dhidi ya ya Marekani na maswahiba wake, baadhi wameanza kusahau ugumu alioupitia Hugo Chavez ili kulinda heshima na uhuru wa kiuchumi wa taifa la Venezuela.

Katika Mgogoro huu baadhi ya viongozi, maafisa kadhaa wa wanajeshi na wananchi wameanza kumuunga mkono Marekani, Uingereza na jumuiya ya ulaya, kwa kumpinga Maduro kwa kudhani kuwa Marekani ni mkumbozi wao na Maduro ndiye chanzo cha umasikini wao na kikwazo cha ustawi wao. Marekani na mataifa mengine ya magharibi walitumia propaganda za uongo na kweli ili kumdhoofisha Rais Maduro, kwanza waliiwekea serikali ya Maduro vikwazo vya kiuchumi kabla ya uchaguzi mkuu, hali ya wananchi ikiwa mbaya, uchumi ukatikisika, mfumko wa bei ukapaa kuliko matarajio ya wengi na hali ya huduma za afya ikadorora, katika hilo wakawa wamefanikiwa kwa kiasi flani kumchonganisha Rais Maduro na wananchi wake. baada ya kufanikiwa kwa hilo mara baada tu ya uchaguzi wakamuibua Juan Guaido kwa shabaha ya kuuchomoa utawala wa kiborvalian.

Baada ya Juan Guaido kujiapisha kama raisi wa Venezuela kinyume na Nicolas Maduro Marekani lilikuwa taifa la kwanza kumtambua Juan Guaidó kama Rais wa Venezuela, baadae nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini zikiongozwa na Brazil zilimtambua Juan Guaidó kama Rais, umoja wa ulaya kwa pamoja umetangaza kumtambua Juan kama Rais isipokuwa Italia pekee ndio unaendelea kumtambua Nicolas Maduro kama raisi halali wa Venezuela, punde tu baada ya Juan Guaidó kujitangaza Rais na Marekani kumtambua kama Rais, Marekani ilimtaka Rais Maduro atangaze kuitisha uchaguzi mwingine wa urais ndani ya siku 8, wakati amri hizo zikiendelea kutolewa na Marekani na washirika wake Marekani ilitangaza kuliwekea vikawzo vipya vya kiuchumi shirika la mafuta la Venezuela ( PDVSA), pamoja na kutaifisha Mali za shirika hilo zilizopo ndani ya Marekani.

Kufatia hali hiyo Rais Maduro aliamua kufunga balozi zake nchini Marekani na nchi nyingine ambazo zimeungana kuiangusha serikali yake. Wakati hayo yakiendelea kwa mujibu wa Bloomberg, kulikuwa na biashara ya dhahabu (gold market) yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.2 iliyokuwa ikiendelea baina ya serikali ya Venezuela na serikali ya Uingereza. Serikali iliamua kuwatuma maafisa wake waende Uingereza kufuatilia uhamishaji wa fedha hiyo ambayo ni mali ya Venezuela ili ihamishiwe Venezuela kutoka Uingereza, lakini Uingereza imegoma kuitoa dhahabu hiyo baada ya kushawishiwa na Marekani. Serikali ya Uingereza imegoma kuwatambua maafisa hao wa Maduro ikidai kuwa inamtambua Juan Guaido kama raisi wa Venezuela. Pia Uturuki ni mojawapo ya nchi ambako inasemekana kuwa na fedha za kigeni za Venezuela, na mpaka sasa inasemekana Marekani imeanza ushawishi wake ili fedha hiyo isije ikaenda Venezuela.

Baada ya Juan Guaidó kujitangaza Rais, amesha itisha maadamano makubwa mengi yakiwa na lengo la kulishinikiza jeshi la nchi hiyo kumuunga mkono Juani Guaido, Rais aliyejiteua na kujitangaza kisha kuungwa mkono na mataifa ya magaharibi, lingekuwepo na tuhuma za Guaido kuhusika katika hujuma za kuzima umeme katika miji kadhaa ndani ya Venezuela, serikali ya Maduro imemshutumu Juan Guaido kuhalibu vituo vya kufulia umeme ndani ya Venezuela jambo ambalo limesababisha kuwepo na giza katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Hiki ndicho ka kinachoendelea Venezuela, na ukweli ni kwamba Juan Guaido anakaribia kushinda maana wamefanikiwa kuteka sehemu nyingi katika propaganda pamoja na kuwashawishi sehemu kubwa ya askali ambao wamemuunga mkono, huku wananchi wengi Pia wanaonekana kuvutiwa na Guaido kufatia matatizo yanayo endelea Venezuela huku nchi ikiwa haina umeme, huduma za afya hospitalini zimesimama, ukosefu wa chakula na kuzorota kwa usalama katika vitongoji vingi katika jiji la Caracas na maeneo mengi sana ya taifa hilo la Venezuela. Kadri siku zinavyozidi kwenda ndio ushawishi wa Maduro unapungua na Guaido anaendelea kupata nguvu ndani ya nchi hiyo yenye historia ndefu barani Amerika ya kusini.

Maswali ya kujiuliza je kuzorota na kuzidiwa mbinu kwa Maduro inaashiria taifa hilo litateketea mikononi mwake? Ikiwa ndio je nini kilicho nyuma ya Guaido kufatia kuungwa mkono na mataifa ya Marekani na washirika wake? Kwanini Maduro ameshindwa kumdhibiti Juan Guaido mpaka kufika hatua ya kuhatarisha usalama wa taifa hilo lilo asisiwa na Simòn Bolivar na kujengwa na Hugo Chavez? Historia itasema let's wait tuone mpaka mwisho wa safari ya bundi huyo katika anga za Caracas.


Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
IMG_20190507_091411.jpeg
 
Back
Top Bottom