Vazi moja la taifa, matamanio yasiyoweza kufikika

Vazi moja la taifa, matamanio yasiyoweza kufikika

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2017
Posts
10,484
Reaction score
19,987
Salamu wana JF

Hii mada ya vazi la taifa ni miongoni mwa mada zinazoonesha namna gani hatupendi kukubaliana na ukweli wa mambo sisi kama watanzania.

Ukweli ni kwamba kama taifa lenye zaidi ya makabila 120 haiwezekani kuea na vazi moja la taifa tena tukabaki kuzingatia tamaduni zetu.

Ni vipi taifa lenye makabila zaidi ya 120 likawa na tamaduni moja?, desturi moja?, hii ni uongo. Tupo na mchanganyiko wa tamaduni nyingi sana za makabila yetu.

Mimi wazo langu ni bora tukawa na mavaxi rasmi kwa kila ukanda au makabila kisha baadae yapi yatakayobaki kuwa kama utambulisho wa watu wetu.

Hata huko Nigeria hawana vazi moja la taifa bali wana mavazi yanayowakilisha makabila yao.

Changamoto kuu ya hili swala ni liamshwa kwa hali na hulka za ukabila na hili hatuwezi kulikwepa kama tutataka kuwa na hicho tunachokiita vazi la taifa.

Kama taifa tukiona hii mada haina maslahi mapana ya utaifa ni bora tukaachana nayo.

Asanteni.
 
Binafsi naona hili jambo ni kama kupoteza muda tulishachelewa.
 
Hivi ni mavazi gani hayo unayoyazungumzia kwa hawa mabinti wa siku hizi wavaa vimini.
 
Back
Top Bottom