Vatican yamkataa Balozi wa Ufaransa

Yericko Nyerere

Platinum Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,027
Reaction score
20,519
Rais wa Ufaransa Francois Holland, amempendekeza muumini mmoja wa kanisa hilo ambaye ni mpenzi wa jinsia moja kuwa balozi wake mjini Vatican. Lakini utawala wa Vatican umesema uteuzi huo haukubaliki.

Makao makuu ya papa mjini The Vatican hayajasema lolote kuhusiana na uteuzi huo,lakini ni dhahiri kuwa baadhi ya maafisa wakuu katika kanisa hilo hawajakubali msimamo wa papa kuhusiana na waumini wa kanisa hilo ambao ni wapenzi wa jinsia moja. Papa alinukuliwa akihoji kuwa yeye hawezi kumhukumu mtu yeyote kwa misingi yoyote.

Serikali ya Ufaransa ilimteua laurent Stefanini kuwa balozi wake mjini vatican mnamo mwezi Januari mwaka huu.

Balozi Stefanini mwenye umri wa miaka 55,amekiri hadharani kuwa yeye anashabikia mapenzi ya jinsia moja na amewahi kufanya kazi katika ubalozi huo mjini Roma na amekuwa mshauri wa masuala ya kidini katika wizara ya mambo ya nje ya ufaransa.

Kwa sasa hakuna upande unaoonekana kuwa tayari kubadili msimamo wake.

Ufaransa ilhalalisha ndoa za jinsia moja mwaka 2013 na uamuzi wa The vatican wa kukataa kumkubali balozi Stefanini huenda ikawa ni thibitisho la The vatican la kutoidhinisha msimamo huo wa Ufaransa.
 
Ushoga unatamalaki kila pembe ya dunia iwe kwa hiari au kwa kulazimisha.
 
waliberali wanapendakulazimisha wakubalike na kila mtu....wanataka ideology zao ziheshimiwe na yeyote pasi kutoheshimu za wenzao....Yaleyale ya Indiana na NCAA Final Four
 
waliberali wanapendakulazimisha wakubalike na kila mtu....wanataka ideology zao ziheshimiwe na yeyote pasi kutoheshimu za wenzao....Yaleyale ya Indiana na NCAA Final Four
Viva Vatican viva
 
Huu ni unafiki kwa Vatican vipi kuhusu kauli ya papa kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja? Vipi kuhusu mapadre wafiraji watoto pale Scotland? The Church had rotten.
 
Huu ni unafiki kwa Vatican vipi kuhusu kauli ya papa kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja? Vipi kuhusu mapadre wafiraji watoto pale Scotland? The Church had rotten.
Ni lini Pope alisema anaunga mkono mapenzi ya jinsia moja!? Kama Ile kauli aliyoitoa.brasil kwenye kongamano la vijana wa katoliki hukulielewa kalisome upya!!
 
Hapo nasapoti Vatican - kulazimishana ushoga kukomeshwe. Lakini pia Vatican iangalie suala la mapadri kuoa
 
Usenge unashika kasi duniani Mungu utuhurumie na utuepushe na ghadhabu yako.
 
mbona hili neno mnalirembaremba?
eti "mpenzi wa jinsia moja"

Sema SHOGA tu au MFIRAJI kama sio MFIRWAJI
 
Wachambuzi wa Masuala ya Vatcan wanafikiri wanasema iajpokua Vatican haijatoa tamko lolote kunusu Balozi huyo ni dhahiri Vatican haikubaliani na Uteuzi huo.wa Ufaransa.

Jumapili hii katika Maadhimisho ya Misa:Ibada itakayoongozwa na pope Fransis waamini wengi wanategemea kumsikia papa akito tamko.

Msemaji wa Vatican Fadher Federico Lamberd vile vile anataraniwa kutoa tamko la vatican mapema wiki hii.

ikumbukwe si mara ya kwa Nchi za Ulaya Magharibi kujaribu Kuwapeleka Mabalozi wanaoshiriki Mapenzi ya Jinsia moja lakini hata hivyo Vatican haikuwahi kukubali Mabalozi Mashoga.
 
Huu ni unafiki kwa Vatican vipi kuhusu kauli ya papa kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja? Vipi kuhusu mapadre wafiraji watoto pale Scotland? The Church had rotten.

Mkuu una bifu na kanisa katoliki Papa hajawai kusuport huu upumbavu,hii ishu ya ushoga ipo kwenye jamii na kama kanisa wanajua kuna tatizo lakn kuna makundi ya watu wengine wanajifanya wao watakatifu wanabaki kulisakama kanisa utazani hili tatzo halipo kwenye dini zao au jamii zao lakn mifano tunayo hata hapa Tanzania sehem walipo mashoga wengi ni sehem za hao hao wanaojifinya malaika kwamba kwao hakuna mashoga wakati wamejaa kibao
 
------- waruhusiwe Vatican!!! Piga chini huyo ama aletwe kwa kina ba Khadija mkunazini
 
Kumkataa wamefanya jambo la maana wakristu hatuwezi kusapoti huu ujinga wa wazungu.
 
uonevu mbona sera yao inaukubali ushoga

Sera ipi hiyo labda ya kwenu .ID yako BOKO HALALI lakini unaweza kuwa mfuasi wa boko haramu ndo wale wale mmeshalaaniwa na Mungu siku nyingi.
 
Waache unafiq vatican
 

Attachments

  • 1428733796514.jpg
    21.3 KB · Views: 249
mbona hili neno mnalirembaremba?
eti "mpenzi wa jinsia moja"

Sema SHOGA tu au MFIRAJI kama sio MFIRWAJI

Mfiraji/mfirwaji ni mtu anayeingilia/anayeingiliwa 'kinyume na maumbile'. Mwanaume anaweza kumwingilia mwanamke 'kinyume na maumbile'. (FYI research shows less than 10% of gay men actually practice anal sex)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…