barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Kumetokea mabishano makali sana kati ya Mbunge Msigwa na DC Kasesera eneo la Iringa Mjini baada kuwa wamewatembelea wahanga wa nyumba zilizoezuliwa na mvua kubwa na kusababisha baadhi ya watu ktk Tarafa ya Nduli
Vurumai hizo zilizotokea baada ya Msigwa kukasirishwa na kitengo cha DC kutaka kumuengua ili asionekane anatoa msaada kwa watu wa jimbo lake bali DC ndio ionekane anajali wananchi.Shutuma zilienda mbali baada ya Msigwa kumueleza DC kuwa anajuwa anamhujumu na amekuwa anapanga mikakati ya siri ya kumfanyia hujuma ili aonekane hafanyi kazi jimboni kwake.
Juhudi hizo zimefanyika week iliyopita ambapo DC kwa kushirikiana na Humphley Polepole waliandaa "mdahalo" na wanafunzi wa vyu vikuu mkoani Iringa na kuanza kumsema vibaya Mbunge Msigwa,katika mdahalo huo Polepole amerekodiwa akisema Iringa awalikosea sana kumchagua Msigwa sbb alikuwa anamuunga mkono "fisadi" Lowassa
Wakati DC Kasesera alimshutumu Mb Msigwa kutokwenda Tarafa ya Pawaga kusaidia wahanga wa mafuriko na Msigwa akamjibu kuwa aanze kumwambia Lukuvi kwanini hajaenda maana Tarafa ya Pawaga ipo ndani ya Jimbo la Isimani,na hata yeye akienda sio lazima DC ajue,kama ambavyo yeye anaenda na kupiga picha na kurusha Facebook akimbeba mpiga picha ambaye haitaji msaada wa kubebwa.
Vurugu hizo ziliamuliwa na diwani na Meya wa Mji. Mwishoni Msigwa akamwambia DC awaite polisi wamuweke ndani maana katika viako vya CCM DC Kasesera amekuwa akisema lazima amuweke ndani Msigwa kumtia adabu