Van Gaal:''Mkutano na Mourinho utanikata tamaa''

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
160207110409_louis_van_gaal_640x360_pa.jpg
Image copyright PA
Image caption Mourinho na Van Gaal katika mkutano wa hapo awali.

Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa atakata tamaa iwapo Manchester United ilifanya mazungumzo na Jose Mourinho.


United haikutoa tamko lolote baada ya ripoti hizo za juma lililopita kwamba maafisa wa kilabu hiyo walifanya mazungumzo na wawakilishi wa aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho.

Alipoulizwa iwapo anafikiri kulikuwa na mazungumzo,Van Gaal alisema: katika soka hilo linawezekana,lakini sidhani kama kulikuwa na mazungumzo.


Amesema kuwa alikuwa na uhusiano mzuri na mkurugenzi mkuu wa United Ed Woodward na mmiliki Glazers na kwamba wangemwambia.

Manchester United kwa sasa hawako katika michuano ya kilabu bingwa Ulaya,na wako nafasi ya tano katika jedwali la ligi ikiwa pointi sita nyuma ya manchester City ambao wako katika nafasi ya nne.

160124011430_van_gaal_640x360_reuters_nocredit.jpg
Image copyright Reuters
Image caption Van Gaal
Van gaala amebaye alichukua ukufunzi wa kilabu hiyo 2014 na kuiongoza United katika nafasi ya nne mwaka uliopita alikubaliana na pendeko kwamba nafasi nyengine ya nne itaonekana kama mafanikio.

United itachuana na Sunderland katika uwanja wa Stadium of light siku ya jumamosi.
 
Back
Top Bottom