Valentine day

Valentine day

peho

Member
Joined
Oct 9, 2013
Posts
75
Reaction score
23
Napenda kujua na mnipe majibu mazuri wapendwa wana JF.Nini hasa maana halisi ya hii siku,na ni nini hasa kinatakiwa kufanyika?
 
Ni siku ya wadanganyanao kwamba wanapendana! Kama una watoto hiyo ni siku nzuri sana ya kupima DNA!
 
Napenda kujua na mnipe majibu mazuri wapendwa wana jf.nini hasa maana halisi ya hii siku.na ni nini hasa kinatakiwa kufanyika?

sikukuu ya kishetani,,inayosherehekewa na wafuasi wa shetani..
 
Ukitaka kujuwa maana yake ijumaa na wewe piga nyekundu kuanzia sox chup.i hata miwani na karaba kenye msitari mwenkundu kweny soli utajuwa maana yake
 
Ni siku ya kilele cha malimbukeni kuwatajirisha wajanja kwa kununua mavazi mekundu, kadi nyekundu na maua mekundu kisha kupeana na wapenzi feki ili waonekane wanapendana. wizi mtupu.
 
Siku ya valentine ni kila mwezi wa pili ambapo watu hudhihirisha mvuto na haiba za mapenzi kwa kila mmoja kwa kupeana kadi na zawadi.

Sherehe hii chanzo chake ni mambo ya dini za kirumi.

Lupercalia ni sherehe iliyoadhimishwa na Warumi wa zamani kila mwezi wa pili tarehe kumi na tano. Lengo lake ilikuwa kuwaheshimu miungu Lupercus na Faunus na ndugu mapacha wawili ambao ni Romulus na Remus ambao huaminiwa kuwa waanzilishi wa mji wa Rumi.

Sherehe za Lupercalia zilifanyika juu ya kilima kiitwacho Palatine ambapo warumi wa zamani walijenga nyumba zao.

Makuhani wa miungu lupercus walivaa mavazi ya ngozi ya mbumzi. Baada ya kutoa kafara ya mbuzi na mbwa, walijipaka damu ya mbuzi na mbwa kwenye miili yao, walikimbia kuzunguka kilima wakiwa wamebeba usinga wa ngozi ya mbuzi ulioitwa Februa(kifaa cha utakaso).

Wanawake wa Kirumi walisimama kando ya Kilima cha Palatine ili wale makuhani waweze kuwapiga na ule usinga/ februa wakiamini kwamba tendo hilo litawasaidia kuwa na uzao mwingi na wepesi wakati wa kujifungua.

Pia sherehe hii ilihusiana na vijana wa kiume na wa kike kuchagua mpenzi. Makuhani waliweka majina ya wasichana kwenye boksi na kila mvulana alichukua karatasi ya jina la msichana kwenye boksi na msichana huyo atakuwa mchumba wake mpaka sikukuu nyingine ya Lupercalia.

Mwaka 270 A.D, Sikukuu ya Lupercalia iligeuzwa na kuwa sikuu inayoitwa ya kikristo Kumuheshimu mtakatifu Valentini aliyeuwawa karne ya tatu

Kuna hadidhi nyingi kuhusu Valentini.
Kuna hadidhi inayosema valentini alikuwa mkristu aliyekuwa rafiki ya watoto wengi, warumi wakamfunga kwa sababu ya kukataa kutambikia miungu yao. Watoto wakapeleka kadi zenye maneno ya upendo na kuppachika kwenye Vizingiti vya dirisha la chumba cha gereza alimokuwamo Valentini.

Hadithi nyingine inasema Valentini alimponya binti wa mfungwa mwenzake na baadae huyo binti kuangukia kwenye penzi la Valentini.

Inaaminiwa kuwa valentini aliuwawa Februari 14 mwaka 269 A.D.
Mwaka 496A.D Papa aliamuru Februari 14 kuwa sikukuu ya valentini. Ikawa ianasheherekewa na kanisa kama mbadala wa sikukuu za kipagani.

Chanzo: Kitabu cha GLOBAL HISTORY AND GEOGRAPHY, the grouth of ccivilizations kilichoandikwa na HENRY BRUN, LILLIAN FORMAN na HERBERT BRODSKY



Yehoshua Hamochiah
 
Ni siku ya kupigwa mimba,kuambukizwa ukimwi,kuharibu future za watu kwa kiini macho cha wapendanao,siku ya kusaliti ndoa......ole wao wanao kwenda kutenda uzinzi tumewaonya mapema Mungu atawalipa uovu huu vichwani mwenu.
 
Back
Top Bottom