Valentine day, tuwapende pia tunaowachukia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Valentine day, tuwapende pia tunaowachukia

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BPM, Feb 14, 2012.

 1. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Wengi leo wanaamini wanasherehekea siku ya wapendanao kwa kuonyesha upendo kwa wenzi wao kwa kufanya hili na lile mradi tu ionekane kwamba anapenda / kumpenda. lakini hebu tuongee na mioyo yetu huo upendo tunaotaka kuuonyesha leo ni kweli unatoka moyoni au unafiki ndani ya mioyo yetu ?

  wengi siku ya leo walioko kwenye ndoa hawana mapenzi ya kweli wanawafanya wake au waume zao ni kama maadui wa kila siku kwani mengi huyafanya tofauti na yale ambayo mume au mke anatakiwa kuyafanya kwa mwenza.. Nyumba zetu ziekuwa jehanamu mtu anapokuwa njiani hufanya yafuatayo
  1. huhakikisha anafuta (call history)
  2. msg kwenye inbox and sent
  3. ana kakikisha anawaaga wale wote anaoona wa muhimu kwa bashasha zote na kuwaeleza ndo anafika nyumbani (jehanamu)
  4. anakosa raha kila anapovuka kizingiti cha kuingia kwake
  pia imekuwa kama tabia ya kawaida kushindwa hata kupata walau dk 15 za kuongea na mwenza hata kutaniana nao kwa vile tunapenda kulimbikiza matatizo ya wenza wetu.
  je leo hii umeondoka nyumbani umemwambia mwenza wako kinafiki unampenda , je ni wangapi umewaambia kwa bashasha zote na kuwaahidi lunch na hata kuwapelekea kadi mtandaoni kuonyesha wawapenda zaidi ??
  nini nafasi ya mke au mme katika mapenzi yako ??? haijalishi ni siku ipi hata kama ni hii unayolazimishwa kupenda
   
Loading...