Wakuu,
Naomba kujuzwa na wataalam wa magari kati ya gari zenye injini ya I4 cylinder na V6 cylinder. Je ni kweli gari zenye injini ya v6 zinatumia mafuta mengi kuliko I4? Mfano nina gari lenye injini ya ukubwa wa 2.0L moja ni V6 na lingine I4, je zinaweza kuwa na tofauti gani ya kilometa kwa lita moja?
Kujibu swali, ni kwamba bila kuzingatia mengine, ni kweli gari la V6 lina ulaji wa mafuta zaidi ya I4.
Ijapokuwa engine zote ni 2.0L, moja ina cylinder 6 na ingine ina 4, kwa hivyo yenye 6 inachoma zaidi kwa cylinder 2.
Ukiangalia, tuseme I6 na V6 kwa sababu siku hizi ni vigumeu kupata V4, utaona tofauti ya engine hizi. I6 chamber zake zimepanga foleni moja nyuma ya mwenzake, kwa hiyo huwa ndefu na konda.
Kwenye V6, chamber zake ni kama vile ukiangalia foleni mbili za chupa za soda kwenye kreti, kwa hiyo haziwi na urefu wa I6 lakini ni pana kidogo.
V huwa na advantage ya kuwa na nguvu kuanzia rev za chini, hii ni kwa sababu piston zake zina sukuma kutoka pande mbili tofauti, wakati I inasukuma kutoka juu pekee.
Zaidi ya hapo inakubidi, uangalie specs za gari, kwani vitu kama turbo charger vinaongeza ulaji wa mafuta, VVTI amabyo ni teknolojia inayo wezesha engine kuchelewesha ama kufungua valve mapema, kulingana na mahitaji, yaani kama unavyo endesha gari inahitaji nguvu zaidi au ulaji nafuu wa mafuta. VVTI/VTEC ina weza kupunguza au kuongeza ulaji kulinga na unavyoendesha gari.
Lingine ni kama gari ina injectors ama ni ya kabiurata. Ya kabiurata ukilinganisha na ya injekta ina ulaji mkubwa. Na pia uzito wa gari, sababu ukiangalia gari mbili zenye engine aina moja, ikiwa moja ni nzito kuliko ingine, basi ulaji wake unkuwa wa juu kuliko hiyo nyingine.
La mwisho ambalo huwa naona watu hawazingatii. Watu wengi huleta magari kutoka ngambo, kisha sababu ya mabarabara yetu mekanik anawashauri wabadilishe tires kuweka kubwa, hapo unapobadilisha tu basi ujue lazima engine ita fanya kazi zaidi ya hapo awali kuyazungusha, matokeo yake ni ulaji zadi wa mafuta.