Sasa kama anafanya uzinzi sii maana yake ana mafanikio.....utapataje mbususu bila hela kwa karne hii?
Na shetani nae ndio katulia hapo kwenye mbususu na de libolo. Anajua kabisa hapa anatupata.Hahahaaa uzinzi haunaga mafanikio. Tena unakuta ule uzinzi ni wa kukusudia ndio mbaya mno. Yaani inawezekana kabisa inakua ngumu kuacha lakini ni kuomba neema ya Mungu tuu mtu uweze kuacha kabla ya kukutana na adhabu yake
Adhabu ya zinaa popote kwenye maandiko ni kifo tuu... iwe biblia iwe Qur'an adhabu ni kifo
Sheria zimekua zikisimamia haki za binadamu lakini Mungu mkaliiiiiiii
unaweza usife kwa kupigwa mawe lakini ukafa ukiwa unafanya zinaa au ukafa baada ya zinaa kwa magonjwa
Mungu atusaidie
Na shetani nae ndio katulia hapo kwenye mbususu na de libolo. Anajua kabisa hapa anatupata.
Mie kwa kweli katika kitu nachojutia kuhusu uzinzi ni jinsi uzinzi ulivyonifanya niwaone wanawake kuwa sio binadamu wa kuwaheshimu. Yaani kweli shetani ana nguvu mnooo.
Binadamu mwenzio unaishia kumuona kama chombo cha starehe tuu...huna empathy yoyote kumuelekea mwanamke unachoona wewe ni kama likitu tuu ambalo unaweza limwagia shahawa na kusepa zako. Its realy bad. Unataka kuacha lakini demu akikula nauli yako tuu basi ndio unapata justification ya kuwachukulia kama chombo cha starehe.
Wanawake muwe na ubinadamu pia kwenye suala la nauli zetu tunazowatumia. Mnatufanya tuendelee kuwa wafuasi wa shetani.
Nikiweza toka kwenye huu uraibu wa mbususu kwa kweli nitajiita mwenye bahatiMuda sio mrefu Mungu atakuondoa kwenye huo udhaifu
Usiache kuja hapa kushukuru
Nikiweza toka kwenye huu uraibu wa mbususu kwa kweli nitajiita mwenye bahati
HAPANA MKUU MUNGU HAKUWAHI KURUHUSU,SOMA MUNGU ALIMWAMBIA NINI NA ALIVYOKASIRIKA:Mkuu howardlite tafadhali tunaomba msaada hapa..
Hapa Yesu anaulizwa maswali na wasomi wa dini(Mafarisayo) kuhusu talaka na kuwa na mke zaidi ya mmoja na wanamwambia mbona Musa aliruhusu?HAPANA MKUU MUNGU HAKUWAHI KURUHUSU,SOMA MUNGU ALIMWAMBIA NINI NA ALIVYOKASIRIKA:
1 Wafalme 11:1-13
[1]Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,
[2]na wa mataifa BWANA aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.
[3]Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.
[4]Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.
[5]Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.
[6]Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
[7]Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.
[8]Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.
[9]Basi BWANA akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha BWANA, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,
[10]akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru BWANA.
[11]Kwa hiyo BWANA akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako.
[12]Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako.
[13]Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua.
Ni sawa mkuu,lakini sio niliyoongelea nimejikita kwenye kumkufuru Roho Mtakatifu,by the way tunaposogea kwa ibada huwa tunajihoji,Yesu mahali fulani anasema hata Kama una neno na ndugu yako hamjasameheana na umeshika sadaka usiitoe mpaka umeenda kutengeneza kwanza uhusiano wenu kwa msamaha(toba).Moyo ni kibebeo cha ibada kama moyo hauko safi ni kelele,anasema niondoleeni kelele za vinywa vyenu.Shukrani kwa ufafanuzi pia katika ZABURI 33:1 imeandikwa "Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo" je mtu anaposifu na kuapoabudu akiwa anajijua ana dhambi na hajatubu hiyo ni kufuru au sio kufuru.
.... Ni kweli, zamani things was very Serious... kuna Kanisa kule Tosamaganga - Iringa Padre alikemea tabia ya watu wanaosemekana kuwa ni washirikina wasiende kukomunika baadhi ya watu hao wakapuuza... siku hiyo akasema nimefunga Novena ya siku 9 ninaomba ambaye ni mshirikina na hajaungama asije kukomunika leo wale watu wakaleta ubishi wakaelekea kukomunika muda wa komunio...mtu wa kwanza alipofika kaanguka kabla ya kukomunika, wapili naye baada ya muda kafika kaanguka, watatu naye kafika kaanguka ghafla wakaona watu wengine wawili wakichomoka kwenye foleni ya kukomunika na kutimka mbio kuelekea nje.. Lilikuwa fundisho tokea siku hiyo na watu wale wakanyolewa nywele na wazee wa kimila wakaenda kuungama.!Ni sawa mkuu,lakini sio niliyoongelea nimejikita kwenye kumkufuru Roho Mtakatifu,by the way tunaposogea kwa ibada huwa tunajihoji,Yesu mahali fulani anasema hata Kama una neno na ndugu yako hamjasameheana na umeshika sadaka usiitoe mpaka umeenda kutengeneza kwanza uhusiano wenu kwa msamaha(toba).Moyo ni kibebeo cha ibada kama moyo hauko safi ni kelele,anasema niondoleeni kelele za vinywa vyenu.
Miaka ya 1980's kuna dini fulani ulikuwa ukijaribu kutaka kuingia Kanisani na huko vizuri moyoni ulikuwa unaanguka mlangoni,was very serious.
So before going to church ilikuwa lazima utubu kama kuna mahali ulikosea nguvu za Mungu was revealed isivyokawaida kiasi kama kipindi cha Anania na Safira in the book of Acts
ππ bro kumbe wewe wa zamani,hizi mambo bwana siku hizi zimekuwa adimu,watu wanawanga mpaka mimbarini.Sijui ndio siku za mwisho au moto umezimika?.... Ni kweli, zamani things was very Serious... kuna Kanisa kule Tosamaganga - Iringa Padre alikemea tabia ya watu wanaosemekana kuwa ni washirikina wasiende kukomunika baadhi ya watu hao wakapuuza... siku hiyo akasema nimefunga Novena ya siku 9 ninaomba ambaye ni mshirikina na hajaungama asije kukomunika leo wale watu wakaleta ubishi wakaelekea kukomunika muda wa komunio...mtu wa kwanza alipofika kaanguka kabla ya kukomunika, wapili naye baada ya muda kafika kaanguka, watatu naye kafika kaanguka ghafla wakaona watu wengine wawili wakichomoka kwenye foleni ya kukomunika na kutimka mbio kuelekea nje.. Lilikuwa fundisho tokea siku hiyo na watu wale wakanyolewa nywele na wazee wa kimila wakaenda kuungama.!
Nakubaliana na bandiko lako mm mwenyew nimeonywa San Jua ya uzinzi na adhari zake kwangu mmHabarini za wakati huu wakuu..
Mimi ni kijana wa kiume, umri wangu ni kati ya miaka 30-37, sijaoa. Kwa taaluma ni Mwanasheria. Pia ni mwandishi wa vitabu vya Sheria kwa lugha ya Kiswahili.
Niko JF tangu 2012, ukifuatilia nyuzi zangu nyingi tangu najiunga JF utagundua kwamba zilikuwa zikihusiana na uzinzi huohuo (Biblia inasema kile kimtokacho mtu ndicho kilichoujaza moyo wake), kiukweli nimeandika mabandiko mengi sana humu JF ya kuutukuza uzinzi kwasababu uzinzi ndiyo ulikuwa umeujaza moyo wangu.
Unajua, kwa sisi wanaume, ipo fahari ukiwa na wanawake wengi. Lakini kwenye ulimwengu wa kiroho ipo hatari kubwa mbeleni kuliko hata hiyo fahari ya muda mfupi. Nakushuhudia kwamba ujana wangu nimeutumia kufanya uzinzi/umalaya wa kiwango cha SGR, nimetembea na wanawake wa marika na sifa tofautitofauti. Nimeumiza sana mioyo ya wanawake bila kujua hatari niliyokuwa naikaribia.
Baada ya kupitia changamoto flani ofisini nikajikuta nimeokoka. Mungu alinipitisha kwenye jaribu ambalo lilinifanya nimgeukie yeye kwasababu, kibinadamu nilikosa majibu ya changamoto hiyo, nikajisalimisha kwake, lakini nikiwa wokovuni, dhambi pekee niliyokuwa napambana nayo vikali ilikuwa ni hiyo ya uzinzi na ulevi, nikawa bado nafanya zinaa na kunywa pombe kwa kificho halafu natubu, kuna mambo yangu yakawa hayaendi.
Mimi ni msomaji mzuri sana wa Biblia, msomaji mzuri mno. Nilitambua kwamba ni hatari kufanya dhambi kwa kujua; lakini nikawa napuuza, nikijipa moyo kwamba eti nitatubu baadaye! Kwahiyo nikawa mlokole vuguvugu.
Siku za hivi karibuni nikamuomba Mungu sana anisaidie niushinde uzinzi na ulevi. Sasa naamini kwamba yasiyowezekana kwa mwanadamu yanawezekana kwa Mungu, ni kweli nimefanikiwa kuachana na uzinzi na ulevi, sikatai kwamba majaribu ni mengi hasa kwenye uzinzi, lakini mara zote Mungu ananitengenezea mlango wa kutokea kwenye kila jaribu. Ukiokoka, wadada ndiyo wanajileta kwa wingi hadi inatisha, usipokuwa na nguvu za Mungu unaweza ukasalimu amri!
HATARI ZA UZINZI:-
Kwanza ukisoma Yakobo 4:4 inasema, "Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu?". Kwa lugha nyepesi kabisa ni kwamba, ukizini tu, automatically unakuwa adui wa Mungu.
Ufunuo 21:8 inawataja wazinzi na adhabu watakayokutana nayo huko Mbinguni, lakini mwishoni wa mstari huo wa 8 kuna maneno, "mauti ya pili".
KWANINI UZINZI NI DHAMBI YA MAUTI?
Kwanza nitoe angalizo kwamba hakuna dhambi kubwa wala ndogo. Ila kwa asili, mara baada ya kuwepo kwa misingi ya Ulimwengu, Mungu amekuwa akichukizwa sana na uzinzi (Soma Hesabu 25:1-3).
Uzinzi ni dhambi ya mauti kwasababu, kwetu Wakristo hii miili yetu ni hekalu (makazi) ya Roho Mtakatifu (1Wakorintho 6:19). Mathayo 12:31-32 inasema kwamba dhambi nyingine zote zinasameheka isipokuwa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Kwahiyo ukizini kwa kuutumia huo mwili wako ambao ni hekalu la Roho Mtakatifu unakuwa umemkufuru huyo Roho Mtakatifu aliyeko ndani yako, ataondoka na kukuacha ubaki peke yako.
Lakini pia, dhambi pekee inayofanyika mwilini katika amri 10 za Mungu ni dhambi ya uzinzi, dhambi nyingine zote ni nje ya miili yetu.
Kwahiyo ukizini na mwanamke unafanyika kuwa mwili mmoja naye (1Wakorintho 6:15-16) , kwahiyo kama mwanamke alikuwa na mapepo yanahamia kwa mwanaume, halikadhalika kama mwanaume alikuwa na mapepo yanahamia na kwa mwanamke. Kwa mfano; kama mwanamke/mwanaume unayezini naye ana pepo (roho) ya kukataliwa na wewe unaanza kukataliwa, kama alikuwa na pepo la umasikini, linahamia na kwako pia. So usishangae mambo yakibadilika, tatizo ni huo uzinzi wako.
Kwahiyo vijana wenzangu hasa humu MMU msione ufahari kuzini, mnaziangamiza nafsi zenu wenyewe. Hata Samsoni (Mnadhiri wa Mungu) aliiangamiza nafsi yake mwenyewe kwa uzinzi.
Mwisho, Mtume Paulo kwenye Waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho Sura ile ya 7:1-2 anatuambia, tusiwaguse (tusizini na wanawake), lakini kwasababu wanaume tumejawa na tamaa, basi tuoe mke mmoja. Namuomba sana Mungu anitangulie katika mchakato wangu niliounza wa kupata mke mwema.
Kwa wewe uliyeoa halafu ukazini, hatari ni kubwa zaidi, kwasababu maombi yako hayatajibiwa na Mungu (Soma 1Petro 3:7).
Sensa ya Watu na Makazi ni tarehe 23/08/2022; tujiandae kuhesabiwa, mimi niko tayari, wewe je?
Aksante kwa kusoma uzi wangu na Mungu akutie nguvu uufanyie kazi. Amen!
Imani zamani ilikuwa juu sana, kuna wimbi la Church Business limekuja-interfere mambo ya kiimani hapa katikati... ila Kanisa litasimama tena maana siku za Unyakuo zinakaribia kulingana na utungu wa mambo kama ilivyotabiriwa na manabii na kuandikwa na waandishi.ππ bro kumbe wewe wa zamani,hizi mambo bwana siku hizi zimekuwa adimu,watu wanawanga mpaka mimbarini.Sijui ndio siku za mwisho au moto umezimika?
Lakini Mungu hadhihakiwi siku ya kikiumana ni hatari.
Amen ubarikiwe mtu wa Mungu, Ila dhambi ya kumkufuru roho mtakatifu kadiri ya ufafanuzi wa andiko kwa andiko na wanatheolojia mbali mbali ni kile kitendo cha kuikata sauti ya huyo roho inayokuhimiza kuacha matendo maovu kila leo hadi inafikia hatua unazoea kuishi ktk hiyo dhambi bila hatia moyoni na kuwa jambo la kawaida kwa muhusika then inatokea mauti yanakukuta bila ya toba pia hakuna dhambi isiyosameheka na toba ya kweli na dhati ni ombi linalojibiwa sekunde hiyo hiyo... Ila huyu anaemkufuru roho hasamehewi kwa mantiki ya kwamba haoni hatia ya dhambi ivyo moja kwa moja anakuwa haifanyii toba hadi mauti yanamkuta ila akipata neema ya kuitubia kabla ya mauti anasamehewa...Habarini za wakati huu wakuu..