Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
Najua wengi tunamjua Elon musk kwenye Masuala ya Magari ya Kisasa yenye kutumia Umeme EV Pamoja na Masuala ya Safari za Anga. Sasa amekuja kwenye upande wa Smartphone lengo ni kuleta ushindani na Infinix, Samsung, Iphone na Google.
Inaitwa Tesla Pi Max Smartphone , ni toleo jipya la simu yenye Muonekano wa kipekee sana ikiwa na feature mbalimbali za kibabe sio mchezo mchezo.
๐ Starlink connectivity , simu hii kwanza zimeunganishwa na SpaceX s satellite Starlink Teknoloji inakupa uwezo wa kutumia intaneti yenye kasi balaa mahalo popote ulipo ulimwenguni bila limiit hata maeneo ambayo mtandao hakuna.
๐ Solar chaging
Simu hii ya Tesla Pi phone imekuja na Teknolojia ya solar panels kwa nyuma inakupa uwezo wa kuchaji simu kwenye mazingira ya jua kali bila kutegemea kutembea tembea na chaji kila mara.
๐ค Neuralink compatibility
Simu hii imeunganishwa na Neuralink chip ambayo ni Ubongo wa Elon musk wenye uwezo wa kumruhusu mtumiaji kuweza ku control simu yake hatakavyo na kutumia kwa kufikiria tu.
๐ธ Advanced Camera system
Tesla Pi phone inakuja ikiwa na uwezo mkubwa wa kamera yani Teknolojia waliyotumia kwenye mfumo wa kamera ni ule wanaotumia kwenye kuunda kamera za telescope zenye uwezo wa kupiga picha kali kwenye mazingira yoyote yale tunaita astrophotography yani usiku ni kama mchana.
๐ Tesla system integration
Simu hii itakua na uwezo wa kuingiliana na Magari ya Tesla itampa uwezo mkubwa mtumiaji wa simu hii kuweza ku control gari lake kupitia simu hata kufanyika baadhi ya matengenezo kupitia simu.
โ๏ธ Operating system
Tesla wataweza kutumia mfumo wao wenyewe wa Operating system japo mfumo wa Android utakuwepo lakini mfumo wao utakua na uwezo wa kuingiliana na Magari, Satellite zao na huduma zinginezo.
๐๏ธ PowerFul Hardware
Kwenye suala la Processor wataunda processor zao wenyewe ambapo simu hii inakuja ikiwa na storage yenye nguvu Ram mpaka kufikia kiwango cha 16Gb na storage ya 1TB.
Wataachia lini bado haijajulikana lakini simu hii kwa upande wa Gharama itaanzia Dola $800 mpaka kufikia dola $1,500 inategemea na storage.