View attachment 2309778
View attachment 2309892
Leo ni uzinduzi rasmi wa Simba Week, tuna mambo mengi kwenye wiki hii.
"Msimu huu tunarudi kwa nguvu, tunarudi kutetea ubingwa wetu na slogan yetu ni WE ARE UNSTOPPABLE - HATUSHIKIKI – HATUZUILIKI.- CEO Barbara
Zoezi la usajili bado linaendelea. Wiki ijayo timu yetu ya digital itaanza kutangaza wachezaji wengine.- CEO Barbara.
Kesho mtajua tofauti ya mdhamini na msaada. Tutakuwa na tukio na mdhamini wetu mpya, kampuni ya M-Bet."
"Wachezaji ambao tunawasajili sio wa sandakalawe, ni wachezaji muhimu kwenye vikosi vyao hivyo kunakuwa na ugumu kuwapata, inabidi kuzungumza na vilabu vyao ili kuwashawishi."- Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally.
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema jezi za timu hiyo msimu wa 2022/23 zitazinduliwa wiki hii na zitatengezwa Ulaya badala ya Asia.