lete rimoti
Senior Member
- Aug 24, 2021
- 159
- 202
Habari zenu Macomrade. Bila Shaka Kila Mmoja anaendelea na Mapambano ya Maisha yake.
Uvccm Ina pande mbili
1. Wapo vijana wazalendo ila ni Waoga.
Hili ni kundi la vijana Wasomi lakini wamejawa na Uoga. Wanatambua Wajibu wao lakini hawataki Kutimiza kwasababu ya Uoga. Wananyimwa Fursa pia Kwasababu ya UAkili Zao kuonekana kubwa.
2. Machawa (kundi hili Lina vijana wasiojua kwanini wapo kwenye Chama, vijana machawa na wanafki, na vijana ambao wao husubiria Fursa tu zitokee na waendelee na Maisha Yao. Siasa haiwi sehemu ya Harakati Zao. Wana uwezo wa kusimama kuropoka na kutukana Watu Bila Kuangalia athari za Baadae.
Nimefungua Uzi Huu ili Vijana wazalendo wa kweli mpate Kuonyesha Kwenye Akili zenu Kuna Vitu Gani.
Nina Nia ya kugombea Uongozi niibadilishe jumuiya hii. Nataka iwe Ile ambayo Nyerere aliitaka, Jumuiya ya Vijana ambao watakuwa Tayari kuhoji Vitu vyenye Athari chanya katika Taifa. Jumuiya ambayo hata Rais wa nchi mwenyewe ataiogopa. Hatuwezi Kuwa Watu wakulalamika wakati Sisi wenyewe tunao uwezo wa kubadilisha Vitu.
Yaani Mwenyekiti Wetu analalamika na kuongea Kwa uchungu kuhusu Watu Wanaokula Pesa ya Serikali alafu, vijana tupo na tena tupo kimya tu. Hakuna hata mashinikizo tunayoyatoa huu unyonge hauhitajiki. Kuna Siku Hawa wananchi watachoka na Hali itakuwa Mbaya Zaidi.
Karibuni Vijana wazalendo, karibuni tuonyeshe kwamba Watu wema Bado wapo, lakini pia muwe Tayari hata kukosoa pale mnapoona Kuna mabaya yanatendeka katika Jumuiya au Chama Kwa Ujumla.
Na wahakikishia Huu, Uzi unasomwa na Wakuu wa idara nyingi katika chama. TUNAPOELEKEA ni lazima watahitaji vijana wenye Akili wakaongoze Taasisi za nchi. Sasa kama tutakaa kimya Bila Kuonyesha Nini tunacho katika Akili zetu basi Kila kukicha watawachukua vijana wa Vyama vingine wake watusaidie Kazi.
Lakini Pia Nakaribisha Maoni, Ushauri na ikiwezekana hata Matusi Kwa Watu ambao mmechoshwa na CCM nataka Kutumia Hoja Zenu Hapo Baadae nirekebishe mfumo Huu.
#TanzaniaKwanza[emoji120]