Uzi wa kutafutana waliopoteana kwa muda mrefu

Mwaka 2003 nilikutana na dada mmoja wa kinyakyusa alikuja Arusha na alikua anaenda monduli kwenye mahafali,huyo dada nilikutana nae stand ya kilombero na kwa maelezo yake wakati anatoka dar walikubaliana na wenzake wakutane stand ya ubungo wapande gari moja,ila alipofika stand rafiki zake walikua hawajafika hivyo alipanda basi la Amazon,baada ya kufika Arusha alibaki ndani ya basi akiwasubiri hao rafiki zake na alikua anawasiliana nao kupitia sim ya kondakta wa basi sababu yeye hakua na sim zaid ya no ya baadhi ya ndugu zake akiwemo huyo aliekua ana graduate huko Monduli, huyo kondakta wa hilo alikua mshikaji wangu,so baada ya binti kukaa pale zaid ya masaa mawili rafiki zake hawapatikani wala yule nduguye wa monduli yule mshikaji wangu kondakta aliamua kunipa majukumu ya kuhakikisha huyo binti anapata sehemu salama ya kulala ili kesho yake aelekee monduli,bahat nzuri na mimi kuna dada nilikua nafahamiana nae anafanya monduli kwenye ile supermarket ya jeshi so sikuwaza kwa kumpeleka zaid ya hapo kwa huyo sister,ikabid niondoke na yule dada kwa majina yake aliniambia anaitwa Mage ila sasa alikua na wasiwasi hatar,nilijaribu kumtoa hofu lkn bado alikua na wasiwasi,imagine tumetoka kilombero kwa miguu kuja kupanda daladala za sakina maeneo ya stand ndogo tulipofika chini mti maeneo idara ya maji aligoma kuendelea na safari,akaniambia kama vip tuchukue chumba maeneo haya tulale huko unapotaka twende siende je? Mkienda Kunibaka mtungo si heri mtu mmoja ambae ni mimi kuliko wengi,nikamwambia umewaza mbali sana ila sina mawazo hayo wewe ni kama dada yangu siwezi kukufanyia uhuni,nilitumia nguvu za ziada mpaka akakubali tuendelee na safari,tumefika stand tumepanda kidala safari ya kuelekea sakina imeanza kufika maeneo ya mianzini si akashuka kwenye gari amegoma tena kuendelea na safar na muda huo ni saa moja moja usiku kuelekea saa 2,mmh na mm ikanibidi nishuke nikawa mkali kwake kiaina nikamwambia hapa ulipoteremkia ni pabaya usije ukanilaumu ukidhurika,dah kwa ikabidi arudi kwenye gari kishingo upande,tumefika maeneo ya morovian tukashuka tukaelelea anapoishi yule dada.Tumefika nikamtambulisha vizur kwa yule dada bahat nzuri yule dada nae kumbe anafahamiana na yule mjeshi anaegraduate,dah binti alishusha pumzi moja ya furaha akapewa maji akaenda kuoga,baada ya hapo akapata msosi baada ya msosi akaniomba nimpeleke sehemu akapate huduma ya kupiga sim,kipindi hicho sim tunapigia kwenye vibanda wenye sim walikua watu wachache.
Aliniambia anaitwa Magreth au Mage kwa kifupi ubini wa baba yake nimesahau na alinipa no za kaka yake huyo baada ya pale nimekua nikimtafuta bila mafanikio,kabila lake ni mnyakyusa ila wazaliwa wa Dar es salaam.

Kuna uwezekano kaka yake au yeye ni member wa jf so wapatapo huu ujumbe au wale marafiki zake lazima watakumbuka tukio lilivyokua,pls wasisite kunicheki pm ni zaid ya miaka 20 sasa
 
Nafikiri kwa maelezo yako Huyo mage yupo Iringa kwa Sasa, naeneo ya Ruco
 
Namtafuta binti mmoja anaitwa Alicia,tulikutana Dodoma wilaya ya Mpwapwa kijiji kimoja kinaitwa Chogola hukoo winza, alikuwa anasoma shule ya secondary chogola kama sikosei ilikuwa 2008,na nyumbani kwao aliniambia ni kijiji cha chalinze ambacho kipo Dodoma,mwenye kumjua naomba anijulishe,na kwa maelezo yake kipindi hicho wazazi wake walikuwa wameshafariki ila masuala ya shule kaka yake ambae alikuwa broker wa madini huko Tunduru ndio alikuwa anamsomesha huyo binti Alicia,nimemmis saana
Daaaah nimefarijika sana kuona umetaja sehemu zote ambazo ninazijua hasa zinazohusu wilaya ya mpwapwa.
 
Namtafuta Jeremiah Kiswaga, huyu alikuwa mwalimu wangu wakati nasoma tuition shule ya Central Dom. Huyu mwalimu alitokea kuwa rafiki yangu na hata kuniamini ananipa baiskeli yake nirudi nayo nyumbani kula Cha mchana halafu badae namletea.
Nilishangaa huyu mwalimu anamuamin vipi mtu ambaye hamjui!!?
Baadae alikuja kuwa rafiki yangu akaniambia Yuko iringa ni mkuu wa shule inaitwa Lord's Hill, bahati mbaya nilipoteza mawasiliano yake. Popote alipo au kama Kuna mtu anamfahamu naomba msaada wa kumpata.
 
Kuna mtu anaitwa benard James mwanawile.
Alikuwa anakaa pande za kimara.
Anatafutwa na binti yake.
 
Namtafuta huyu mtu Kwa jina Grace jina la utani G g' alisoma Ushirka wa neema Moshi 4+ yrs back, sijui kilichomsibu simpati kupitia no yak. na acc zake seem haziko active kam yupo anichek please
 
Namtafuta SELINA ALLY tulisoma wote Chiungutwa secondary school Masasi Mtwara 2004-2007

Mlioko Lupaso masasi, msaada kwenu plz kama Kuna anaemfahau
 
Namtafuta rafiki yangu wa utotoni tulianza shule pamoja mwaka 1998 shule ya msingi LUGOMBO Mwakaleli anaitwa GWALUGANO MWAKIPOSA popote alipo au unayemfahamu please naomba nijulishe.
 
Back
Top Bottom