Uzi maalumu kwa ajili ya kueleze kwa ufupi tukio ambalo hautokuja kulisahau maishani mwako.

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,525
Kama tunavyojua maisha ni safari ndefu ambayo imechanyanyika na vikwazo, Mikasa na matukio ambayo mara nyingne binadamu wenzako wanaweza wasiamini na wakajua ni uongo au ni matukio ya kubuni ila leo ningependa tupate kujifunza na kuambiana ni kitu gani ambacho kiliwahi kukutokea ambacho hautakuja kukisahau japo kwa ufupi.

Kwangu mimi Binafsi nakumbuka ilikuwa tarehe 28/01/2012.
Nikiwa mwanza nilipopiga paka wa jirani aliekuwa akiniudhi kila siku alikuwa akilia akizunguka nyumba yangu bila kujua, cha ajabu mida ya usiku kama saa nne hivi paka yule alikuja room kwangu na kuanza kuniuliza kwanni nilimpiga kusema kweli niliogopa sana na nilistushwa na kitendo kile ila gafla nilikumbuka maneno ambayo niliwahi kuambiwa na mchungaji wangu kuwa likitokea jambo lolote ambalo linasadikika kuwa ni jaribu la mwovu shetani ukemee kwa kutamka neno "NAKUANGAMIZA KWA JINA LA YESU KRISTO"
kusema kweli sikuwa na iman kubwa sana kwa mungu ila nilijikuta nikitamka maneno hayo kwa mfululizo hadi nilipostuka nikakuta paka yule ameondoka,

Kusema kweli niliogopa sana na ni moja ya tukio ambalo stakuja kukaa nilisahau katika maisha yangu.

Pia
Pia nakumbuka 06/12/2015.
Nikiwa jijini mbeya nikiwa nafanya kazi ofsi fulani jina siwezi kulitaja kulitokea upotevu wa mali za kampuni katika mazingira ya kutatanisha kusema kweli watumishi wote walinishuku mimi kutokana na mazingira yaliyokuwepo na upotevu wa mali zile kwani chumba kilichokuwa na mali zilizoibiwa mimi ndie nilikuwa natunza funguo japo siku ya tukio la wizi nilipoteza funguo hizo kwa mazingira ya kutatanisha kidogo ambayo nitaelezea hapo baadae ilikuwaje...

Kusema kweli nilipigwa sana ili niseme mali za kampuni nimeiba na nani, Japo nilikuwa na uhakika sijahusika na kitendo kile niliumizwa mkono pamoja na kuteguliwa ubavu wangu wa kushoto ila sikuweza kukili kosa kwa kuwa niliamini sijahusika hivyo nilijitoa kufa kwa ajili ya kutetea haki yangu, Kusema kweli niliteswa sana na kipigo ambacho sitakuja kukaa nikisahau ila namshukuru mungu baada ya wiki kadhaa mwizi alifahamika ila nilikuwa tayari nimefukuzwa kazi na kuumizwa vibaya sana,

Na baada ya kugundulika kuwa sikuhusika Maneger wa kampuni alinitaka nirudi kazini, Ila sikutaka kurudi tena kazini wala sikutaka kufuatilia fidia ya kunidhalilisha kwa kosa ambalo sijahusika niliamua kumwachia Mwenyezi mungu Huku nikiamini yeye pekee ndie alipae kwa haki na usawa,

Na ninamshukuru mungu kwa sasa nipo naendelea kupambana na kazi ya mikono yangu inayonipa riziki yangu japo si kubwa sana ila nina amini ndani ya kazi yangu ya mikono ipo siku nitampiga vita adui umasikini...

Najua yapo mengi sana ambayo ningependa kuyasimulia hapa ila sipendi kumchosha msomaji wangu,

Ila nipo nafikiria nitumie njia gani ili niweze kuwafikishia watanzania wenzangu mikasa yote iliyowahi kunikuta katika maishani mwangu bila ubaguzi na kwa urahisi zaidi kwani yapo mengi ambayo sijaweza kuyasimulia hapa!

Hivyo ninaamini wapo ndugu zangu, Watanzania wenzangu, ambao wamewahi kupatwa na mikasa mikubwa hata zaidi ya haya na wanakosa sehemu ya kuweza kushare na watanzania wenzao ili kuwaelezea japo kwa kifupi tu, Hivyo ningependa leo japo kwa kifupi uzi huu uwe maalumu kwa ajili ya kila mmoja wetu ambae anamkasa japo kwa ufupi aweze kutusimulia hapa ni kutu gani hatakuja kukaa akisahau maishani mwake.
"Bytozy92"
 
Back
Top Bottom