Uzi maalum kwa wauzaji wa vifaa vya simu

Sina mood

Senior Member
Nov 15, 2018
197
1,310
Huu ni uzi mahsusi kwa sisi ambao tunaanza biashara ya kuuza vifaa vya simu mfano makava ya simu, chaja , earphones, nk.

Kwa hiyo tupeane maujuzi kwa ambao wanaujuzi wa hii biashara , bei ya jumla kwa kila bidhaa na bei ya kuuzia.
 
Asante ndugu

Bei za jumla zinafuatana

Maana kila siku kuna toleo jipya

Kwa mfano makava huwa yana uzwa kulingana na fashion yake na kwa wakati Fulani

Ukija chaji ninavyo jua Mimi kuna za kuanzia (1000 mpaka 2000) hizi ni kwa chaji za chini kabiasa

Hizi ni bei za jumla bei ya kuuzia utangalia wewe

Ukija chaji zinazo fauatia hapo zinaanzia (2500 mpaka 5000)

Hizi ni bei za jumla kuuza utachagua wewe

Zipo chaji mpaka za kuanzia (8000 mpaka 15000)

Hizi ni bei za jumla kuuzia uaangalia wewe

Earphones bei ya jumla inaanzia (1000 mpaka 1500)

Na zingne zinaanzia (2000mpka 5000)

Bettery za kawaida zinaanzia 1000 mpaka 2000

Bettery olginal zinaanzia 5000 na kuendelea

Hizi bei nimetaja kwa mtu unae anza ila kama umekamilika

Utaongeza na vingne zaidi
 
Mimi natamani sana sana kujua na hatimaye kuagiza mzigo moja Kwa moja,labda tupeane maujanja wapi hapa bongo waweza nunua hizo accessories Kwa gharama nafuu?na huko wanakojumua wenzetu kama vile Gwanzhoul hali ikoje??je namna gani waweza kutumia mtandao kama Albaba,Amazon,kuagiza mzigo na ukafika salama???????njooni njooni
 
Wafuate mafundi maana wakakufanyie cost analysis ya matengenezo!!au uwauzie wazifanye sreper
 
Mimi natamani sana sana kujua na hatimaye kuagiza mzigo moja Kwa moja,labda tupeane maujanja wapi hapa bongo waweza nunua hizo accessories Kwa gharama nafuu?na huko wanakojumua wenzetu kama vile Gwanzhoul hali ikoje??je namna gani waweza kutumia mtandao kama Albaba,Amazon,kuagiza mzigo na ukafika salama???????njooni njooni
Mkuu Huko wanako fuata mzigo unaweza kuagiza ila changamoto ni nyingi sana
 
Tupeane Uzi jamani,nauli mpaka Gwanzhou go and return Tsh ngapi,na uwe na mtaji wa Tsh ngapi ili iweze kukulipa na TRA imekaaje?Transport cost ipoje??
 
kwa haraka haraka bei ya makava huwa sh ngapi?
Makava yapo aina nyingi ila ya visimu vidogo yanaanzia 800 hadi1000

Ya simu kubwa yanauzwa kulingana na fashion

Ila yanaanzia(3000 mpaka 5000)

Hizi bei ninazo taja ni za mahali nilipo na machimbo ya huku kwetu

Ila kwa walioko dar sijajua bei zao japo najua hazitoautiani sana
 
Tupeane Uzi jamani,nauli mpaka Gwanzhou go and return Tsh ngapi,na uwe na mtaji wa Tsh ngapi ili iweze kukulipa na TRA imekaaje?Transport cost ipoje??
Garama za usafir andaa dola 2000+

Mtaji unaweza anza na mil. 15

Ila ukitaka upate faida kutokana na kufata mzigo China.

Jitahidi kuepuka kutumia bandari yetu hii

Pale mzigo unaeza fika mapema kisha ukapigwa kalenda kibao ili mradi tu wapate kukuchaji ada zao za kihuni.

Nowdays,
Nmeamua kutumia Ndege maana ni uhakika zaidi na haraka sana kibiashara.
Na mzigo ukishafika airport, hakuna longo longo ni fasta fasta kuchukua chako na kusepa.
 
Bei za Jumla za Makava
1. Back cover za simu ndogo kama techno,itel,Nokia,viwa,vodafone,n.k
(Old model)@pc=600

2.Back cover za simu ndogo
(New model-Autofocus) @pc=650

3. Back cover za smartphone brand kama techno,itel,infinix, n.k Pc = 1,200

isipokua kwa brand kama Samsung, iPhone, Nokia, Sony na Opo @pc= 1,500

4. Kava za kufunika na kufunua bei ni @pc=3,000
 
Back
Top Bottom