Uzi maalum kwa Ununuzi na uuzaji wa Mbaazi msimu wa 2017/2018

Jack HD

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
852
1,159
Tunapouanza msimu wa Mbaazi. Naomba wadau wote wa zao hili kwenye upande wa kuuza locally na exportation. Tujadili kwa pamoja kuhusu masoko, bei, upatikanaji, Packaging, procedures za kuexport, usaidizi wa vibali etc

Binafsi ni mdau wa zao hili kwenye upande wa kuexport, yeyote mwenye masoko, mwenye kuuza, na mwenye chochote kinacholihusu zao hili karibu tujadiliane.

Karibuni tujifunze na tutajirike kwa pamoja.
 
Mpya niliyoipata ambapo nilijiona nipo outdated sana ni kuwa Kigoma inafanya kufuru kwenye mbaazi. Hususani maeneo ya Kasulu huko. Nasiki MO na Azam wanaload kwa wingi kutokea huko
 
Tunapouanza msimu wa Mbaazi. Naomba wadau wote wa zao hili kwenye upande wa kuuza locally na exportation. Tujadili kwa pamoja kuhusu masoko, bei, upatikanaji, Packaging, procedures za kuexport, usaidizi wa vibali etc

Binafsi ni mdau wa zao hili kwenye upande wa kuexport, yeyote mwenye masoko, mwenye kuuza, na mwenye chochote kinacholihusu zao hili karibu tujadiliane.

Karibuni tujifunze na tutajirike kwa pamoja.

Mkuu huku kusini( Mtwara ) mbaazi ipo ya kutosha tu.
Kama utakua na bei inayoeleweka tutafanya business nna vikundi vya uzalishaji mbaazi tunatafuta mtu abae tunaweza kuingia nae makubaliano ya manunuzi.
 
Mkuu samahani Kama nitakua nakutoa nje ya mada, Nina maswali mawili

1. haya masoko ya nje unayapataje? Kuna website au mahali ambapo unapata taarifa za uhitaji na kuunganishwa na wateja?
2. Utaratibu(Vibali, usafirishaji na malipo) wa kuuza nje ukoje?
 
Nami nakomea hapa kwanza kusubiri majibu
 
Mkuu samahani Kama nitakua nakutoa nje ya mada, Nina maswali mawili

1. haya masoko ya nje unayapataje? Kuna website au mahali ambapo unapata taarifa za uhitaji na kuunganishwa na wateja?
2. Utaratibu(Vibali, usafirishaji na malipo) wa kuuza nje ukoje?
Kuna njia nyingi za kupata masoko ya nje. Hizi njia tatu ndizo huwa natumia mara kwa mara

Moja, kupitia jamaa zangu ambao wapo kwenye nchi husika ninapotaka kupeleka mazao ama kupitia jamaa za hao wenye kuitaji hayo mazao. Kuna wahindi wengi wanasaidia jamaa zao kuwaunganisha na exporters wa hayo mazao. Lakini ni lazima uwe umefanya nao kazi kadhaa na wamejenga imani na wewe.

Pili, unawezakujitangaza na kukutana na watu wenye mahitaji kupitia kwenye trade exhibitions

Tatu, Unaweza kuwa wa digital na kuamua kujitangaza kwenye website ambazo ni potential for international trade. For indian market india mart iko poa.

Vibali ni rahisi kama ukiwa kwenye biashara rasmi inayotambulika kisheria. Kwa mazao kama mbaazi, dengu, choroko, kunde hakuna complications nyingi kama nilivyoona kwenye baadhi ya post humu ndani.
 
Mkuu huku kusini( Mtwara ) mbaazi ipo ya kutosha tu.
Kama utakua na bei inayoeleweka tutafanya business nna vikundi vya uzalishaji mbaazi tunatafuta mtu abae tunaweza kuingia nae makubaliano ya manunuzi.
Mkuu huko mnauzia kwenye vyama vya msingi ama kila mkulima anauhuru wa kuuza apendavyo. Bei inasimamaje?
 
Kuna njia nyingi za kupata masoko ya nje. Hizi njia tatu ndizo huwa natumia mara kwa mara

Moja, kupitia jamaa zangu ambao wapo kwenye nchi husika ninapotaka kupeleka mazao ama kupitia jamaa za hao wenye kuitaji hayo mazao. Kuna wahindi wengi wanasaidia jamaa zao kuwaunganisha na exporters wa hayo mazao. Lakini ni lazima uwe umefanya nao kazi kadhaa na wamejenga imani na wewe.

Pili, unawezakujitangaza na kukutana na watu wenye mahitaji kupitia kwenye trade exhibitions

Tatu, Unaweza kuwa wa digital na kuamua kujitangaza kwenye website ambazo ni potential for international trade. For indian market india mart iko poa.

Vibali ni rahisi kama ukiwa kwenye biashara rasmi inayotambulika kisheria. Kwa mazao kama mbaazi, dengu, choroko, kunde hakuna complications nyingi kama nilivyoona kwenye baadhi ya post humu ndani.

Nashukuru sana mkuu. Naomba univumulie kwa maswali ya ziada

1. Vipi kwa upande wa india kule huhitaji kuwa na kibali kuingiza mzigo?

2. Kwa uzoefu wako Minimum quantity ambayo huwa wanahitaji ni kiasi gani?

3. Nina plan ya kulima mwenyewe ufuta au mbaazi niuze india nikipata soko la uhakika. Je kuna uwezekano wa kuingia mkataba na mnunuzi ukishavuna unamuuzia?

4. Ukiacha mbaazi, choroko, dengu na kunde zao gani lingine linahitajika sana huko India?
 
  • Thanks
Reactions: SDG

Mkuu kama we ni mnunuzi nicheki PM nikupeleke machaka yote ya huku kusini, kwa sasa ufuta ndio umechanganya na ukiamua kuingia mtaani "chomachoma" unaweza pata kwa bei kati ya 1300-1500 ingawa bei elekezi imesimama TZS 2000/=.
Mimi kesho inshallah nitakuwa Newala kuna jamaa ameniita tunaweza kuingia chaka, ila nilishapita Nanjilinji-kilwa, Liwale kuna sehemu wanaita kibutuka wanalima sana ufuta, Ruangwa kwa majaliwa tena pale pale hom kwao Nandagala na maeneo jirani ufuta na mbaazi vinapatikana na choroko Nanyumbu zinapatikana kwa wingi sana ukihitaji nakupeleka machaka yote hayo mkuu.
 
Kuna njia nyingi za kupata masoko ya nje. Hizi njia tatu ndizo huwa natumia mara kwa mara

Moja, kupitia jamaa zangu ambao wapo kwenye nchi husika ninapotaka kupeleka mazao ama kupitia jamaa za hao wenye kuitaji hayo mazao. Kuna wahindi wengi wanasaidia jamaa zao kuwaunganisha na exporters wa hayo mazao. Lakini ni lazima uwe umefanya nao kazi kadhaa na wamejenga imani na wewe.

Pili, unawezakujitangaza na kukutana na watu wenye mahitaji kupitia kwenye trade exhibitions

Tatu, Unaweza kuwa wa digital na kuamua kujitangaza kwenye website ambazo ni potential for international trade. For indian market india mart iko poa.

Vibali ni rahisi kama ukiwa kwenye biashara rasmi inayotambulika kisheria. Kwa mazao kama mbaazi, dengu, choroko, kunde hakuna complications nyingi kama nilivyoona kwenye baadhi ya post humu ndani.
Naunga mkono hoja 100% ila kwenye biashara upo kitambo?

Na mimi napenda kujumuishwa kwenye hii business mkuu
 
Shusha nondo mkuu!!

Ushuru/kodi hulipwaje.
Kwenye exportation ya mazao haya tunayoongelea hakuna kodi kabisa kwa hapa nchini. Utalipia tu ushuru wa kijiji kule unapotolea mzigo. Exportation huwa haina kodi isipokuwa kwa korosho na ngozi mkuu
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Nashukuru sana mkuu. Naomba univumulie kwa maswali ya ziada

1. Vipi kwa upande wa india kule huhitaji kuwa na kibali kuingiza mzigo?

2. Kwa uzoefu wako Minimum quantity ambayo huwa wanahitaji ni kiasi gani?

3. Nina plan ya kulima mwenyewe ufuta au mbaazi niuze india nikipata soko la uhakika. Je kuna uwezekano wa kuingia mkataba na mnunuzi ukishavuna unamuuzia?

4. Ukiacha mbaazi, choroko, dengu na kunde zao gani lingine linahitajika sana huko India?

1.Mkuu inategemea unafanya international trade kwa incoterms zipi. Je, unafanya kwa DDU, DAP, DDP, FOB, CIF, C&F, Exwork ama? Biashara nyingi za kimataifa zinafanywa kwa C&F ama CIF. Maana yake obligation zako kama exporter ni mpaka mzigo utakapofika kwenye bandari ya nchi husika unapokwenda mzigo. Kuhusiana na masuala ya kodi za kule hausiki kwa namna yoyote. Binafsi nimesaidia sana watu kuexport, kuanzia kufanya packaging na logistics nzima mpaka mzigo kufika.

2. Minimum quantity for exportation ni 1X20FT Ambapo ni kama 17.5-18 TONS Ikishuka kwa tani moja si mbaya. Ila ikishuka zaidi unaweza kusababisha kushuka sana kwa profit kwa sababu cost per unit itakwenda juu sana.

3. Mkuu hiyo mikataba mimi nishaifukuzia sana lakini sikuambulia kitu. Unajua wenzetu japo si wote hawataki kujicommit kwa sababu pia demand ya hivi vitu kule kwao pia vinafluctuate sana. India wanalima sana ila mahitaji ni makubwa kuliko supply na ndio maana wanaagiza kutoka nje. Kuna muda inahitajika sana na kuna wakati demand hushuka kiasi pia price fluctuations wanaziogopa maana wakianticipate vibaya ni hasara kwao. Cha muhimu wewe anza na local suppliers ama exporters wa hapa hapa. usivuke mipaka, ukitaka chain yote uikabe peke yako itakugharimu ila pia sikukatazi.

4. Ukiacha mimea ya jamii ya mikunde, kuna mtama, korosho na ufuta
 
Mkuu naomba nielezee zaidi kuhusu soko la mtama na aina ya mbegu ya mtama unahitajika zaidi. Asante.
 
Naomba unisaidie demand ya hayo mazao ikoje nje na hasa nchi gani?
1.Maharage
2.Mbaazi
3.Kunde
4.Choroko
Na mazao ya jamii hiyo

May Allah bless Me and You
 
Back
Top Bottom