Uzi kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu

Mi natamani sana kuwekeza katika biashara hii lakini sijui maeneo gani yanaleta uhakika wa kutopoteza mtaji mf: kuwa na mwalo wa kusafisha dhahabu, kununua na kuozesha mchanga, ama kuchimba kabisa
Kama huna ABC ya bihashara hii, nakushauri hiyo pesa nunulia watu pombe wanywe wakusifu. Hii bihashara ni zaidi ya uchawi.

Ukitaka kuifanya anza taratibu ujue ABC kwenye practical sio hapa JF ( J fa fa fa fa in Gwajima's voice)
 
Mi natamani sana kuwekeza katika biashara hii lakini sijui maeneo gani yanaleta uhakika wa kutopoteza mtaji mf: kuwa na mwalo wa kusafisha dhahabu, kununua na kuozesha mchanga, ama kuchimba kabisa

Mkuu wasikutishe eti uchawi unahusika hakuna vitu kama ivo nifuate PM nikujuze zaidi hata kuwekeza inawezekana maeneo ni mengi sana na karibu lakini jipange mtaji tu.
 
Mkuu wasikutishe eti uchawi unahusika hakuna vitu kama ivo nifuate PM nikujuze zaidi hata kuwekeza inawezekana maeneo ni mengi sana na karibu lakini jipange mtaji tu.
Hapo ulipo mwambia akuje PM, naona ndio umekosea mkuu.
Sababu kama kweli unayo nia njema na mhusika, haipo sababu ya kukimbilia PM kana kwamba kuna jambo la siri unalo taka kumueleza
 
Wakuu, ngoja nifunguke hapahapa ili isijekuonekana kama mimi ni kanjanja. Aiseee kiukweli ili uweze kuwekeza katika uchimbaji mdogo kwa uzoefu wangu, ni lazima usipungue mtaji wa milioni thelathini 30,000,000/= halafu ukitaka kuozesha mchanga kama unaanza lazima uwe na milioni mia moja 100,000,000/=. Hapo unakuwa umejenga plant humo humo ndani ya pesa hiyo na mtaji umebaki mkubwa wa kuanzia. Wakuu, na ninapenda munielewe, siyo kwamba nilimwambia mtu mmoja anikute PM lakini nikataka kuonekana tapeli fulani wakuu.
 
Wakuu ngoja nifunguke hapahapa ili isijekuonekana kama mimi ni kanjanja aiseee kiukweli ili uweze kuwekeza katika uchimbaji mdogo kwa uzoefu wangu ni lazima usipungue mtaji wa Milioni thelasini 30,000,000/= halafu ukitaka kuozesha mchanga kama unaanza lazima uwe na Milioni miamoja 100,000,000/= hapo unakua umejenga plant humo humo ndani ya pesa hiyo na mtaji umebaki mkubwa wa kuanzia wakuu na napenda mnielewe siokwamba nilimwambia mtu mmoja anikute PM lakini nikataka kuonekana tapeli fulani wakuu.
Umeeleza vyema mkuu.

Ebu naomba unifanyie kunyumbua hiyo 30 milioni.

1. Je, unamaanisha hapo nitaanzisha duara (shimo), kulisha wachimbaji, kutoa vifusi pamoja na unyonyaji wa maji toka shimoni?

2. Je, kama ninahitaji kuozesha mchanga, kujenga processing plant kama ulivyotangulia kusema, hii 100 milioni inatosha kusomba kifusi madini, kujenga jiko la uchomaji (refinery smelter), madawa ya kuchenjulia, umeme na maji, structures, malipo ya wafanyakazi nakadhalika?

Kwasasa naomba niishie hapa.
 
Umeeleza vyema mkuu.
Ebu naomba unifanyie kunyumbua hiyo 30 milioni.
1. Je, unamaanisha hapo nitaanzisha duara (shimo), kulisha wachimbaji, kutoa vifusi pamoja na unyonyaji wa maji toka shimoni?
2. Je, kama ninahitaji kuozesha mchanga, kujenga processing plant kama ulivyo tangulia kusema.... je hii 100 milioni inatosha kusomba kifusi madini, kujenga jiko la uchomaji (refinery smelter), madawa ya kuchenjulia, umeme na maji, structures, malipo ya wafanyakazi na kadhalika?

Kwasasa naomba niishie hapa

Aaaaah mkuu hii milioni 30,000,000/= nikweli unaweza kuchimba duara vizuri lakini kwenye maji itaongezeka na nimemaanisha maeneo ambayo hayana maji na ukifika kwenye maji tayari utakua umeshazalisha na utakua na nguvu hata ukianza kuvuta maji utaongeza kidogo tu halafu kuhusu plant nimemaanisha ni kujenga tu tena tank 6 na hela inayobaki utaanzia kanunua maozesho na madawa ya kuanzia lakini angalizo hiyo gharama ni Kibongobongo kulingana na mitaji yetu na kuhusu jiko tena standard lazima uwe 1bilion mkuu.
 
Aaaaah mkuu hii milioni 30,000,000/= nikweli unaweza kuchimba duara vizuri lakini kwenye maji itaongezeka na nimemaanisha maeneo ambayo hayana maji na ukifika kwenye maji tayari utakua umeshazalisha na utakua na nguvu hata ukianza kuvuta maji utaongeza kidogo tu halafu kuhusu plant nimemaanisha ni kujenga tu tena tank 6 na hela inayobaki utaanzia kanunua maozesho na madawa ya kuanzia lakini angalizo hiyo ghalama ni kibongo bongo kulingana na mitaji yetu na kuhusu jiko tena standard lazima uwe 1bilion mkuu.
Mkuu, kwa aelezo haya naomba nihitimishe kwa kusema kwamba umeanzisha mada ngumu ilio kuzidi kimo.

Wewe unachokijua ni kuhusu wachimbaji na hakuna unachokijua kuhusu biashara ya uchumbaji.
 
Hakuna biashara ngumu duniani kila kitu kujifunza ila biashara ya dhahabu cha kwanza inabidi uwe intelligent hata kama haujasoma inabidi uwe mjanja kupindukia main reason (hatuna vifaa vya kuweza kutambua kama katika mwamba huu kuna dhahabu kiasi fulani na kutokana na gharama ntapata faida au hasara kiasi fulani)
 
Mkuu, kwa aelezo haya naomba nihitimishe kwa kusema kwamba Umeanzisha mada ngumu ilio kuzidi kimo.
Wewe unacho kijua ni kuhusu wachimbaji na hakuna unacho kijua kuhusu biashara ya uchumbaji...
Mkuu hebu jaribu kuchangia unachokijua ,usijaribu kucrush mwenzio,yeye amejaribu kutoa yake ...kama unajua zaidi na wewe changia
 
Mkuu, usinibeze ninafahamu kuhusu wachimbaji na uchimbaji sana, tena kwa kina. Vilevile, biashara ya dhahabu naifahamu na ninaweza kuelekeza na kulinda mtaji wa mtu usipotee na nikutoe wasiwasi, nilishalinda mtaji mpaka wa rais wa wachimbaji wadogo na ukiingia kichwa katika biashara hii kuuwa mtaji ni kugusa chief.
 
Hivi kati ya kuwa mchimbaji na mnunuzi wa dhahabu ni bora kufanya kipi?

Mkuu kwa kawaida wote wanaitwa wachimbaji lakini inategemeana ila walio wengi walianza kuwekeza katika kuchimba halafu wakapanua wigo katika ununuzi na pia ili uweze kuwa mnunuzi mzuri anayeweza kuepuka hasara nyingi ni bora ukaanza kuchimba ili uzifahamu changamoto maana ni nyingi sana mkuu.
 
Mkuu kwa kawaida wote wanaitwa wachimbaji lakini inategemeana ila walio wengi walianza kuwekeza katika kuchimba halafu wakapanua wigo katika ununuzi na pia ili uweze kuwa mnunuzi mzuri anayeweza kuepuka hasara nyingi ni bora ukaanza kuchimba ili uzifahamu changamoto maana ni nyingi sana mkuu.
Asante kiongozi.
 
Back
Top Bottom