Uzeruzeru ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzeruzeru ni nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, May 19, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [h=1][/h]Uzeruzeru ni nini?
  Huu ni ugonjwa wa kurithi ambapo mtoto hutoa seli chache zinazotathmini rangi ya ngozi, nywele na macho, maarufu kama ‘melanin’. Sehemu hii ya juu ya ngozi inayotathmini rangi ya ngozi huwa na jukumu la kukuza baadhi ya near.
  Hii husababisha ukolevu dani wa rangi - ambapo hakuna rangi kwenye ngozi yako, nywele na macho au huwapo rangi hafifu kinyume na watu wengine katika familia.
  Umuhimu mmoja wa rangi hii ya ngozi ni kuvuta mialeya jua. Kwa hivyo, watu wengi walio na uzeruzeru husumbuka sana wanapokuwa kwenye jua na wapo katika hatari ya kushikwa na saratani ya ngozi.
  Macho ya waathiriwa wa uzeruzeru hayakuwa vizuri na hata hayaoni vizuri hata wakivaa miwani.
  Ingawa hakuna fiba ya uzeruzeru, waathiriwa wanaweza kuchukua hatua ya kuboresha maono na lazima waepuke jua kali. Uzeruzeru hauathiri werevu au uwezo wa elimu ya mtu. Kwa bahati mbaya, watu walio na uzeruzeru hujihisi kubaguliwa kijamii na hushuhudia kubaguliwa.
  Dalili na Ishara
  Ngozi
  Dalili inayoshuhudiwa kawaida ili ngozi nyeupe. Iwapo wathiriwa wanakaa kwenye jua, wan a kuwa na alama au madoadoa meusi kwenye ngozi. Pia huchomwa kwa jua.
  Nywele
  Rangi ya nywele inaweza kuwa nyeupe zaidi, manjano, nyekundu nyekundu au yenye maji ya kunde.

  Rangi ya Macho
  Huanzia rangi hafifu ya bluu hadi maji ya kunde na vile vile huweza kubadilika kulingana na umri.

  Kuona
  Dalili za uzeruzeru zinazofungamana na umuhimu wa macho hujumwisha.

  • Kupepesa macho haraka haraka bila kutarajia, mbele na nyuma.
  • Macho yote kutoweza kuelekezwa upande mmoja au kusogezwa kwa pamoja.
  • Kutoweza kuona vitu vilivyo mbali.
  • Kusumbuliwa najua
  Nyanzo
  Chanzo cha uzeruzeru ni mabadiliko ya moja ya seli za kimaumbile ambazo hukadiria utuaji wa seli za rangi ya ngozi. Katika aina nyingi ya uzeruzeru, lazima mtu arithi sampuli mbili za seli za maumbile zilizobadilika – moja kutoka kwa kila mzazi – ili mtu kuwa na uzeruzeru. Iwapo mtu ana sampuli moja, basi hawezi kuwa natatizo hili, awe mke au mme.
  Unapostahili kutafuta ushauri wa daktari

  • Iwapo mtoto wako hana rangi kwenye nywele au ngozi anapozaliwa
  • Iwapo mtoto wako ana macho yanayosogezwa kutoka upande mmoja hadi mwingine.
  • Iwapo mtoto wako aliyeathirika kutokana na uzeruzeru anavuja kutoka puani, hupata vilia haraka au kuathirika kutokana na magonjwa ya muda mrefu.
  Matatizo
  Matatizo ya uzeruzeru hushusisha hatari za kimwili pamoja na changamoto kijamii na kihisia.
  Matatizo ya ngozi
  Moja wapo ya matatizo hatari yanayofungamana na uzeruzeru ni hatari ya saratani ya ngozi. Kukaa muda mrefu kwenye jua husababisha ngozi kuwa ngumu, nene na kuparara

  Sababu za kijamii na hisia

  • Mitazamo ya watu dhidi ya wale walio na uzeruzeru ni kwamba wanaweza kuwa na mtazamo mbaya kwa wale walioathirika.
  • Watoto zeruzeru hubandikwa majina, hukejeliwa au kuhangaishwa kwa maswali kuhusu maumbile au macho yao.
  • Historia ndefu ya hekaya imechangia kuwapo kwa nguvu za mazingaombwe dhidi ya uzeruzeru. Wengine huwaona kama watu wasiostahili katika familia au kuwaona kama laana katika jamii.
  • Zeruzeru kawaida huonekana tofauti na watu wengine katika familia zao. Pia hujihisi kutambuliwa kama watu wa nje.
  Sababu hizi zote huweza kuchangia kubaguliwa kijamii, kutojitambua na hata mahangaiko.
  Tiba

  • Kwa sababu uzeruzeru ni tatizo la kijenetiki, ni ngumu kutibiwa.
  • Watoto watafaa kuvaa miwani itakayoboresha maono yao. Macho yao yanastahili kutazamwa na daktari kila mwaka.
  • Zeruzeru wanatakikana kumuona daktari kila mwaka ili kuona kama wana dalili za saratani ya ngozi.
  Utunzaji wa kibinafsi
  Unaweza kuwasaidia watoto wako kujifunza namna ya kujitunza wakiwa peke yao.

  • Tumia mafuta ambayo yanaweza kuwazuia kutokana na jua kali.
  • Epukana na jua lilio na hatari kubwa, kwa mfano kuwa kwenye jua wakati wa mchana au wakati ambapo kuna jua kali.
  • Vaa mavazi yanayokuzuia yakiwemo yale yenye mikono mrefu kama shati, suruali na kofia.
  • Zuia macho ya kwa kuvaa miwani mieusi.
  Maarifa ya kupambana na ugonjwa huu
  Kupambana na shida ya kutoona vizuri
  Zeruzeru wengi hukuza maarifa yao ya kupambana shida ya kutoona vizuri. Kuweka kitabu karibu na macho wakati wa kusoma hufanya kazi kuwa rahisi bila kusababisha hatari yoyote kwa macho. Wewe kama mzazi, usipunze mikakati hii.
  Kupambana na changamoto za elimu
  Iwapo mtoto wako ni zeruzeru, anza kushirikiana na walimu, wataalamu wa masomo maalum wakiwemo wasimamizi wa shule. Anza kufunza wataalamu wa shule wapate kujua maana ya uzeruzeru na namna inavyoathiri mtoto wako. Pia unaweza kuzungumza na wadau shule au kuulizia namna ambavyo shule inaweza kutekeleza mahitaji ya mtoto wako akiwa shuleni.
  Baadhi ya mabadiliko darasani ambayo yanaweza kusaidia mtoto wako hujumuisha.

  • Kiti kilicho karibu na sehemu ya mbele ya darasa
  • Vitu au picha zilizochapishwa zenye tofutti kubwa kama vile herufi nyeusi kwenye karatasi nyeupe kuliko herefu zenye rangi au karatasi yenye rangi.
  • Vitabu vikubwa vilivyochapishwa.
  Kupambana na kutishwa, kukejeliwa na kubaguliwa
  Msaidie mtoto wako kuwa na maarifa kuchukukia mitazamo ya uzeruzeru na watu wengine:

  • Mdai mtoto wako kukuambia kuhusu yale aliyoyashuhudia au hisia zake.
  • Kufanya mazoezi kuhusu namna ya kuwajibikia kejeli au maswali yanayokera.
  • Tafuta huduma za mshauri au mwanasaikolijia ambaye atakusaidia wewe na mtoto wako kuwa na mawasiliano ambaye na maarifa ya kupambana na matatizo.
  Kumbuka, zeruzeru ni binadamu aliye na uwezo, fikira na hisia kama watu wengine. Wananchi wa Tanzania wamemchagua zeruzeru kuwa mbungekwa mara ya kwanza.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  asante kwa elimu
   
Loading...