Uzembe wa TBC

kuna swala la sauti pia! anaye control sauti ya kipindi kimoja kwenda kingine sijui anatatizo gani....au kile kibonyezeo kimeisha na kinasubiri tupate msaada kutoka benki ya dunia?
 
Vichwa havipati kazi huko.
Hapo zinatolewa kiundugu.
Mwisho wa siku kumejaa vilaza
 
Hahaha huwa wana kopi model za wengine wanatusomea sisi.
Mi huwa nasema TBC hawakujiandaa na hawajajiandaa kuwa television, vipindi vyao wangevirudisha RTD tuvisikilize kuliko kuviona.
 
Kwani kuna TV inayoelezea mafanikio mazuri ya Ras wetu kiutendaji na maendeleo yanayochukua nafasi hivi sasa nchini kamaTBC?

Tena LIVE

TBC - UKWELI NA UHAKIKA.
 
Azam malizaneni na TCRA mrudishe local channels twateseka na TBC maana hawataki kuumiza vichwa kabisa, habari zao ni mbili tatu taarifa ya habari imeisha, wanarudia vipindi hadi kero.
 
Mkuu nilikua naangalia juzi nilisikitika sana aisee...

Yaani utabiri wa Hali ya hewa wana copy na kupaste utabiri wa nyuma.... Na kushindwa hata kufanya editing..
Shame!!!!
 
Back
Top Bottom