Uzanizibari kwanza sera mwisho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzanizibari kwanza sera mwisho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, Aug 6, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=2][/h][​IMG]Nassor Ahmmed Mazurui

  Wananchi wametakiwa kuachana na sera za vyama vyao vya siasa juu ya mfumo wa muungano wakati wa kutoa maoni yao ya undwaji wa katiba mpya ya jamhuri ya muungano Tanzania.
  Mwakilishi wa jimbo la Mtoni Nassor Ahmmed Mazuri amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuwachia wananchi kutoa maoni yao juu ya mfumo wa muungano wanaoutaka, baadala ya kuwahimiza kuangalia sera za vyama vya siasa.
  Akizungumza katika semina juu ya mambo ya muungano, Mazuri amesema kero za wafanyabiashara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbili bado haijamalizika na kusema zaidi gari 500 zimekwama katika bandari ya Dar es Salaam.
  Amesema viongozi waliopita wameshindwa kutatua kero hizo hasa kwa wafanyabiashara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbili
  Nae mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Mansour Yussuf Himid amewataka wazanzibari kuondoa fikra za kuvunja muungano, na kuwataka kuzingatia mfumo wa muungano wa mkataba utakaoleta maslahi.
  Amesema wazanzibari bado wana haki ya kujadili aina ya mfumo wa muungano unaofaa bila ya kuzuiliwa lakini, haitakuwa busara kuwa na fikra za kuuvunja.
  Amesema kulilia kiti cha Zanzibar katika umoja wa mataifa na kujiunga na OIC sio dhambi kwa vile katiba ya Zanziba inahimiza ushirikiano wa kimataifa wenye nguvu za kiuchumi
  Semina hiyo ya wajumbe wa baraza la wawakilishi ina lengo la kuwaelimisha wananchi jinsi ya kutoa maoni ya undwaji wa katiba mpya katika tume ya taifa ya kukusanya maoni hayo.
  [h=3][/h]Like
  Be the first to like this.
   
Loading...