Uzalishaji mbegu za kiume waporomoka duniani

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
Jerusalem. Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Hebrew-Hadassah Braun, cha Jerusalem umebaini kuwa kiwango cha mbegu za kiume kwa wanaume duniani kimepungua kwa zaidi ya asilimia 50.

Utafiti huo umeeleza kuwa kiwango na ubora wa mbegu za kiume kimeshuka katika kipindi cha chini ya miaka 40 na hakuna ushahidi kuwa kiwango hicho kitaongezeka.

Hata hivyo utafiti huo umesisitiza kuwa kiwango na idadi ya mbegu za kiume kimeshuka zaidi kwa wanaume wa nchi za Magharibi.

Pia imeelezwa kuwa kushuka kwa ubora na idadi ni tishio kwa uwepo wa watu duniani.

“Utafiti huu unawapa wasomi kazi kubwa zaidi hasa kwani idadi ya mbegu za kiume na afya ya binadamu ni muhimu zaidi. Wasomi sasa wanatakiwa kuchunguza chanzo cha kushuka huko kwa idadi ya mbegu za kiume na namna ya kutatua tatizo hilo,” amesema Dk Hagai Levine.

Profesa Hagai ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mazingira na Afya wa Chuo cha Hebrew, amefanya utafiti huo kwa kushirikiana na Profesa Hannah Swan wa Chuo Kikuu cha New York kitengo cha Afya ya Jamii.

Madaktari wengine waliohusika katika utafiti huo ni wa Brazil, Denmark, Israel, Hispania na Marekani.

Utafiti huo umefafanua zaidi kuwa kiwango na idadi ya mbegu za kiume ni kipimo sahihi cha uwezo wa kuzalisha wa mwanaume.

Chanzo: Mwananchi
 
Huo utafiti umefanywa kwa hao kuku wa kizungu umekuwa wa dunia nzima?sisi huku kuna watu wana watoto 18 .
 
HII NI HABARI NJEMA KWA WALE WANACHAMA WA CHAPUTA.
Badala ya kumwaga mbegu chini wakauze huko
 
Uzalishaji mbegu za kiume waporomoka duniani.

Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Hebrew-Hadassah Braun, cha Jerusalem umebaini kuwa kiwango cha mbegu za kiume kwa wanaume duniani kimepungua kwa zaidi ya asilimia 50.
 
nchi za magharibi wanavyoshabikia nawanavyoruhusu wanaume kufirana wanategemea nini
ndo mana nawaambia wanaume wenzangu wa mikoani nyie fyatueni tu, ukikutana na halima fyatua, suzy fyatua, debora fyatua,maiumuna fyatua wasitupangie vya kufanya uzazi wa mpango wakapaniane huko huko si tunafyatua tu
HAPA KUFYATUA TU
 
Jerusalem. Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Hebrew-Hadassah Braun, cha Jerusalem umebaini kuwa kiwango cha mbegu za kiume kwa wanaume duniani kimepungua kwa zaidi ya asilimia 50.

Utafiti huo umeeleza kuwa kiwango na ubora wa mbegu za kiume kimeshuka katika kipindi cha chini ya miaka 40 na hakuna ushahidi kuwa kiwango hicho kitaongezeka.

Hata hivyo utafiti huo umesisitiza kuwa kiwango na idadi ya mbegu za kiume kimeshuka zaidi kwa wanaume wa nchi za Magharibi.

Pia imeelezwa kuwa kushuka kwa ubora na idadi ni tishio kwa uwepo wa watu duniani.

“Utafiti huu unawapa wasomi kazi kubwa zaidi hasa kwani idadi ya mbegu za kiume na afya ya binadamu ni muhimu zaidi. Wasomi sasa wanatakiwa kuchunguza chanzo cha kushuka huko kwa idadi ya mbegu za kiume na namna ya kutatua tatizo hilo,” amesema Dk Hagai Levine.

Profesa Hagai ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mazingira na Afya wa Chuo cha Hebrew, amefanya utafiti huo kwa kushirikiana na Profesa Hannah Swan wa Chuo Kikuu cha New York kitengo cha Afya ya Jamii.

Madaktari wengine waliohusika katika utafiti huo ni wa Brazil, Denmark, Israel, Hispania na Marekani.

Utafiti huo umefafanua zaidi kuwa kiwango na idadi ya mbegu za kiume ni kipimo sahihi cha uwezo wa kuzalisha wa mwanaume.

Chanzo: Mwananchi
....mbegu za kiume ni kipimo sahihi cha uwezo wa kuzalisha wa mwanaume......Kumbe ndio maana mademu wanazaliwa kwa wingiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Uzuri wake ni kuwa kwa kuwa supply itakuwa juu, basi demand itashuka. The same na kwenye bei ya kuuziana.
 
hizo mbegu za miaka 40 iliyopita wamezipata wapi..... au wamechukua mbegu ya mtu mwenye miaka 60 wakalinganisha na ya yule mwenye miaka 20.....
 
Back
Top Bottom