Utangulizi
Ni mara nyingi utasikia viongozi wa kisiasa wakisema tuweke utaifa mbele. Je, hii ni sawa na kusema tuweke uzalendo mbele?. Si lengo langu kuelezea utofauti kati ya mambo haya mawili. Nizungumzie Uzalendo ambao ni hali ya mtu kuwa na mapenzi na nchi yake, (mapenzi ya kipekee) na kutaka kuwa na utambulisho wa kipekee, huzingatia sana mwenendo na afya ya nchi yake na hufikia hatua ya kujitoa [kwa dhati] kupigana katika kutetea maslahi ya nch yake.
Hakuna wakati tunatakiwa kurudi nyuma na kuimba wimbo wa hamasa wa mapenzi na nchi yetu kwa Tanzania kama kipindi hiki:
basi tuhamasishane kwa wimbo huu
Wimbo wa Hamasa:
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana,
Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.
Tanzania Tanzania, ninapokwenda safarini,
Kutazama maajabu, biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu hakika

Tanzania Tanzania, watu wengi wanakusifu,
Siasa yako na desturi, ilituletea uhuru
Hatuwezi kusahau sisi, mambo mema ya kwetu hakika

Tanzania Tanzania, watu wako ni wema sana,
Wenye shida na taabu, kukimbizwa na walowezi,
Tanzania yawakaribisha, mpigane kiume chema wee,
Tanzania Tanzania, heri yako kwa mataifa.

- Kipindi ambacho kundi dogo la wanasiasa wanaotumia fedha na 'media' ili kila uchwao tuwaimbe wao.
- Kipindi ambacho 'matajiri' wanatumia fedha zao kutuandalia viongozi wanaitwa 'king makers'
- Kipindi ambacho Tanzania imekuwa si kimbilio tena kwa wenye taabu
- Kipindi ambacho tanzania imekuwa 'shamba la bibi' kwa rasilimali na utajiri wetu kubebwa na walowezi mchana kweupeee.
- Kipindi ambacho 'hongo' au rushwa si aibu tena. Haki hununuliwa kwa ktu kidogo
- Kipindi ambacho uongozi si 'dhamana' bali ni biashara ya kuuza na kununua.
- Kipindi ambacho mawaziri husoma kurasa 400 za mkataba 'uhusuo madini' mwenyewe akiwa hoteli ya 5* ughaibuni.
- Kipindi ambacho 'utawala' una nguvu kuliko 'bunge' na 'mahakama'.
- Kipindi ambacho sifa za spika wa bunge ni 'jinsia yake' na wala si utumishi wake uliotukuka
- Kipindi ambacho spika yupo kulinda maslahi ya mtu au kikundi cha watu flani wasiotakia mema nchi
- Kipindi ambacho uteuzi wa majaji unaacha maswali mengi.
- Kipindi ambacho mateso na matatizo ya wananchi yamekuwa mtaji wa kisiasa
- Kipindi ambacho ufa kati ya wenye nacho na wasio nacho unakuwa kwa kasi sana
- Kipindi ambacho ni 'bora elimu' na sio 'elimu bora' kwa sababu watoto wao hawasomi hapa
- Kipindi ambacho gharama za kupeleka wagonjwa Apollo India kwa mwaka tungeboresha hospitali zetu ili huduma hizo zipatikane hapa.
- Kipindi ambacho ukihoji utajibiwa 'una wivu wa kike'
- Kipidi ambacho....