Uzalendo ni chanzo cha Usalama wa Taifa?

Mkuu nashukuru sana nimepata kitu kipya hapa.
Shukran sana
 
Aisee kaka, nakushukuru sana.
Nyongeza yko ni kubwa sana kias kwamba naona ilifaa sana kusimam kama uzi. Lkn kwa maana uzalendo halis umeamua kushare knowledge hiyo katk huu uzi wetu.

Mungu akubariki sana. Kupitia comment hii kuna mengi nimeyapata na naendelea kuyatafakar kwa kina kwajil y kujijeng na kujitayarisha muda wote
 
Aiseee dah
 
Aloo safi kabisa inapaswa kuwa hivyo maana hivi vyama vya kisiasa kupitia ushawishi wao(influence yao) wameigawa nchi kikanda na pia wamevuruga umoja wa kitaifa, raia mapenzi yao katika taifa (uzalendo) yamepungua na kuelekezawa katika vyama. Hapa ndipo tunakutana na chawa kina L. M.

Matokeo yake badala ya kua kitu kimoja tunaishia kurumbana(kukashifiana).

Badala ya kua kitu kimoja kutatua faults tunategeana na kusubili upande mwingine ukosee ili ipatikane sababu(justification) ya kushusha ushawishi wa chama fulani, Sasa hili ni tatizo kwani sote tunajenga nyumba moja yanini kugombea fito.

Kuhusu kuazisha shilika hili suala hatuna budi itabidi tuanzishe tu maana kuna ombwe hapo katikati ukiachana na vyama na hawa wanaharakati ambao wapo mmoja mmoja unaona kuna kitu kina miss ambacho kitatuunganisha wote kama taifa tukafocus/tukawa na shabaha moja pasipo kujali tofauti zetu.

Tunaweza kuthubutu kwa kuanza na resources tulizonazo kwasasa then tutaimalika taratibu taratibu, mfano Tunaweza tukaanza na movement kupitia mitandao (social media).
 
1.hiyo ni vyombo vya ulinzi na usalama,wanalipwa
2.Kijeshi zaidi
3. Labda uwe kitengoni
4. Hata Taifa stars imefeli mbaya mbovu hapo AFCON.
5. Royal tours did that si unaona mwarabu alikuja kutimua njeree kule?
6. Kuna Mzee wetu humu anafanya hiyo kazi vizuri sana.
7. Umesikia wapi hiyo suala mkuu?bandari imekushinda kulinda,huko porini napo pamekushinda,unajua kabisa kuwa mali yote iliyoko hapa ni ya serikali kwa hiyo huo uzalendo ni pamoja na kutoa ushirikiano pindi serikali itakapo hitaji kuchukua mali zake.
Cha kufanya anza kuwafundisha watoto wako kuhusu uzalendo,ili siku moja watakua mfano wa kuigwa.
 
Samaki mkunje angali mbichi.
Shukran Mkuu, ufafanuzi wako umetupanua upeo kwamba msingi mkubwa wa uzalendo unaanzia katika ngazi ya familia katika malezi... hapa nimeelewa kwanini familia inatambulika kama Taasisi.

Katika hili nakubaliana nalo kwani mifano ipo wazi

Mfano.
Mataifa kama Japan China wanafundisha uzalendo na maadili mema tokea wanazaliwa kuna mahali nilisoma kua huko Israel tabia(Akili) ya mtoto inaanziwa kutengenezwa kuanzia kwenye ujauzito... nazani wote tunajua tabia za mataifa hayo kwa ujumla.

Hata hapa Tanzania kuna tofauti katika malezi mfano jamii ya watu wa nyanda za juu Kusini huwezi ukalinganisha na mikoa ya pwani(Dar, Moro,) kitu cha ajabu ni kwamba kutokana na kukosekana kwa jitihada za makusudi za kuendeleza uzalendo na maadili miaka ya hivi Karibuni hali imekua mbaya zaidi kiasi kwamba hata zile jamii zilizokua imara zimeanza kuporomoka kimaadili.

Jitihada zisipo chukuliwa kwa wakati hata hiki kizazi cha panyaroad wakiwa wakubwa na kwa wakati huo hali itakua mbaya zaidi pengine wakashindikana kudhibitiwa wakaunda magenge ya kihalifu kama kule Brazil.
 
Hiyo itakuaa hatar kubwa sana aisss. Kuna kitu kinahitajika sasa kuliko kawaida ili kushape hiki kizazi
 
chanzo ni uwe uvccc kuwasifia wazee wa ccm na kutii amri zao
Hao chawa ndiyo chanzo Cha uzalendo kupotea. Maana chawa Hana address Leo yupo kichwani, kesho yupo kwenye nguo...Mtu yeyote mwenye tabia za kusifu pasipo haja hawezi kuwa mzalendo. Na ndiyo hao ambao ni chanzo Cha matatizo yote haya ya Sasa.

Nampenda sana Baba wa Taifa, ila Kwa sehemu alichangia hii tabia kumea na kukua katika taifa kwakupenda kusofiwa na kitotaka kukosolewa hata alipoonekana kukosea.

Pia kuweka Katiba ambayo yeye aliishi ya impunity mpaka kusababisha watu wote kuwa loyal Kwa wenye nafasi na siyo nchi. Kwa hili lazima kama Taifa tukubali kuvunja huu mfumo Ili tujenge taifa ambalo Kila mtu mwenye mchango apate nafasi ya kuutoa Kwa faida ya nchi na siyo persons
 
Hii ni kazi nzuri ya mabeberu wa Dunia hii ..Walijua haya ndiyo yatakuwa matokeo ndiyo sababu walilazimisha masharti ya IMF
 
Umeeleza kirefu sana
Usalama wowote wa nchi cha kwanza hakikisha wananchi wana chakula cha kula Tanzania usalama wa chakula ni mzuri na watu wana chakula hamna shida ya upatikanaji wa chakula .Watu asilimia kubwa wana uhakika wa chakula.Kama wapo wasio na uhakika ni wachache sana

Pili hakikisha asilimia kubwa ya wananchi wana ajira .Tanzania asilimia kubwa ya wananchi wana ajira.Asilimia 85 ya watanzania huishi vijijini wamejiajiri kwenye kilimo,ufugaji na uvuvi na mijini asilimia kubwa imeajiriwa serikalini au sekta binafsi viwandani,masokoni,biashara ndogo na kubwa za aina mbali .Wasio na ajira kabisa ni asilimia ndogo mno ya wakazi wa mijini

Tatu usalama wa nchi ni kuhakikisha asilimia kubwa wana makazi kwa kuweka sera rafiki za wao kupata makazi hili limewezekana kwa kuwa na sera nzuri za ardhi ambazo asilimia kubwa ya watanzania wana uwezo wa kumiliki mashamba,viwanja au nyumba

Hayo maeneo ukishayafikia una uhakika nchi kuwa salama

Hayo ndio mambo makubwa ya nchi kuwa salama na kuzalisha wazalendo
 
Alo walituweza walitukamatia pazuri nadhani tulikua na hali mbaya kiasi kwamba tulikua hatuna budi ni kukubali tu.

Lakini mambo mengine ni kutokuwajibika kwa mamlaka husika kuna viongozi hawatekelezi wajibu wao ipasavyo mfano mipango miji nashidwaga kuwaelewa.
Hii ni kazi nzuri ya mabeberu wa Dunia hii ..Walijua haya ndiyo yatakuwa matokeo ndiyo sababu walilazimisha masharti ya IMF
 
Nimepata point mkuu shukran
 
Sawa,
Well elaborated.
 
Viongozi kama Hayati JPM ni mfano tosha wa wazalendo wa Taifa hili.
1. Alikuwa tayari kujitoa sadaka kwa ajili ya nchi yake
2. Alipambana na upigaji serikalini kadri alivyoweza
3. Alipambana usiku na mchana ili nchi ipige hatua kimaendeleo n.k.

Ukiwa na kiongozi kama Hayati JPM, ni rahisi kuwa Mzalendo.

Lakini kwa hawa wengine, kila mmoja afanye tu kile kilicho sahihi machoni pake mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…