Uyoga wa magazeti kuelekea 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uyoga wa magazeti kuelekea 2015

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ndutu, Apr 4, 2011.

 1. n

  ndutu Member

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kufuatilia malumbano na mijadala inayoendelea katika uwanja wa siasa sasa hivi, ni rahisi kuhitimisha kwamba harakati za kurithi hatamu za uongozi wa nchi hii mwaka 2015 zimeanza. Wale wanaowania tayari wameshaanza harakati za kujiweka vizuri. Wanafanya hivyo ama kwa kujifagilia, kujisafisha (kama ni wachafu) au kuwachafua wenzao kama wanawaona ni tishio. Hili linatekelezwa kwa kutumia tsnia ya habari vilivyo na kwa hali ilivyo sasa, wengi wa waandishi wamepoteza maadili na hata weledi wao, wengi wakijikuta wakitumika katika harakati hizo.

  Katika siku za karibuni, tayari tumeshuhudia uyoga wa magazeti na majarida mapya yakimea na kuwaongezea mzigo wasomaji. Moja kati ya majarida hayo ni lile la UMOJA ambalo limeingia mtaani kwa kishindo. Katika toleo la kwanza, jarida hilo lilitoka na picha za maandamano ya CDM kule Arusha lakini kwa ndani, ikatoka makala ya mwanasiasa anayezungumziwa sana hapa nchi - Edward Lowassa. Wamiliki wa jarida hili wamejitambulisha kama Absalom Kibanda, mhariri mtendaji wa Tanzania Daima na mwanasheria Masatu Makaki. Wengine walioshiriki ni waandishi waandamizi wa gazeti la Tanzania Daima na Sayari, ambao hatujui kama ni waajiriwa rasmi au wanapiga 'deiwaka'.

  Habari zilizopatikana ni kwamba jarida hili litajivua gama karibuni na kuwa gazeti la kila siku na mdomo mahsusi wa Lowassa katika harakati zake za kuingia ikulu. Litatumika pia kuwatia adabu wanaharakati wa mapambano dhidi ya ufisadi na tayari mwanasiasa huyu ameshatoa ofisi, samani na fedha za kuendeshea gazeti hili ambao ofisi zake ziko huko mikocheni, Dar es Salaam.

  Swali la kujiuliza ni kwamba je, Msajili wa Magazeti anayaangaliaje magazeti haya na haoni kwamba haya ni sumu kwa umoja na amani ya nchi yetu? Je, ni sahihi kwa mtu au kikundi cha watu kuanzisha chombo cha habari maalum kwa ajili ya kusifia mmiliki au kuwachafua wale ambao anatofautiana nao kimisimamo? Vipi kuhusu waandishi wanaotumika kufanikisha mapango huo haramu? MCT na MOAT hawana mchango katika hili?
   
 2. T

  Tiote Senior Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  For sure, the authorities need to move swiftly and censure these media outlets that are set up for sinister motives lest we let this country degenerate into a failed state! People should not be allowed to use their ill gotten wealth to whip others while the power that be stands aside and look. This may a recipe for chaos!
   
 3. w

  watenda Member

  #3
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii inanikumbusha maneno ya Mzee Sumaye mwaka 2015, kwamba mtu anayetumia vyombo vya habari kuwachafua wenzake akiingia madarakani atatumia bunduki kusafisha njia. Pamoja na kwamba maneno yale hayakuwa yakiendana na rais tuliyekuja kumpata baadae (maana yeye amejipambanua kama mpenda uhuru wa kujieleza) lakini hawa walioibuka kutaka kumrithi Kikwete wanatoa uwezekano wa kutimia kwa maneno ya mzee Sumaye.
   
 4. b

  banyimwa Senior Member

  #4
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Du mzee! ulimaanisha 2005 au unafanya ubashiri? Hata hivyo nakubali kwamba maneno ya huyu jamaa ambaye tulimbeza wakati ule yanaleta sense sasa!
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa watanzania gani? Hawa hawa wa kizazi cha digital, ambao ni werevu wa kujua hila na ghilba zilizo uchi kama hizi? Wenyewe wanajua chombo gani cha habari ni makini na mengine yatabaki yanasomwa na waanzilishi, wapambe wao na familia zao. Wacha waanze tuone watakakoishia maana hili siyo gazeti la kwanza.

  Kuna Tazama, Taifa, rai, mtanzania, dira na mengine mengi lakini ulizia kiwango cha mauzo yake halafu utashangaa kwa nini bado wako sokoni. Yamepoteza mvuto na kubaki kuchakaa tu maskini!
   
 6. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #6
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwahiyo hili ni gazeti la CHADEMA na lowassa? mbona hatari kweli kweli
   
 7. e

  ebwana eh Member

  #7
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nchi ziliendelea huwa kuna vijarida kama hivi huwa vinaitwa tabloids, uingereza wana the sun,isitoshe kwamba hata babu alianza loliondo akaja mama mutalemwa halafu mjukuu kule mbeya nazani kuna umuhimu sana wa kuanzisha ushauri nasaa kuhusu magonjwa ya akili na madhara ya kuto kukubali kushindwa
   
 8. b

  banyimwa Senior Member

  #8
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mzee umejua ku-connect dots. Ngoja wenyewe watuambie
   
 9. b

  banyimwa Senior Member

  #9
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama hivyo unavyovizungumzia vimeanzishwa maalum na wamiliki kwa nia ya kuupotosha umma kwa kuwasafisah au kuwachafua watu. Tofauti ya hivyo jiarida ulivyosema vipo kila mahali na hiki cha hapa ni dhamira ya kuanzishwa kwake.
   
 10. e

  ebwana eh Member

  #10
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mzalendo,

  inawezekana maanake hata mzee sitta anasema kuna watu kumi tu wanayumbisha nchi hii, hivi karibuni nimefuatilia magazeti ya rostam na lowassa,wao wakibomoa CDM wao ni Mhe Rais Slaa na Mhe Zitto tu,hayo magazeti husana mtanzania wanakwambia mbowe kakomaa kisiasa,
  chonde chonde hapa sisemei ukanda hila muungano wa wafanyabishara kubaka nchi yetu, kwahiyo sishangai kabisa kwamba kuna element za kuungana kwa wafanya biashara kuzidi kothofisha mwenendo wa nchi hii

  hitimisho hata kunguru atengenezwaje kulika kwake kunataka moyo
   
 11. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #11
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  banyimwa,

  kaka sijui unaonaje hiyo qoute hapo maanake hapo mbona kama nikuhatarisha amani ambayo aipo tangu tupate uhuru
   
 12. w

  watenda Member

  #12
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hapa sasa kila kitu kiko wazi. Huwezi kuchangia nyumba na mwizi na huku wewe ukijua kwamba huyo manayechangia naye ni mwizi halafu watu wasikuone kwamba wewe nawe ni mwizi. Mwelekeo wa Tanzania Daima katika siku za hivi karibuni umejaa utata na maswali mazito, hasa katika kuunadi na kuusifia ufisadi wa hawa jamaa. Sasa leo Mhariri yule yule anapotumika huku kwingine unadhani hapo mtu atasema nini? Mimi nakwenda mbali kusema kwamba uhusiano hapa ni kati cha CDM na mafisadi maana Mbowe ni mwenyekiti wake!
   
 13. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #13
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  nguvu ya pesa aliyonayo lowassa ndio inampa kiburi kufanya yote haya.
  mbaya zaidi hela yenyewe katuibia watanzania.
  nadhani ni wakati muafaka sasa serikali ichukue hatua dhidi ya uyoga huu wa magazeti ili watu wenye nia chafu na nchi yetu wasifanikiwe.
   
 14. w

  watenda Member

  #14
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzalendo, hizo ndo gharama za kuutetea ukweli. Hata kama unauma ni lazima usemwe sasa ili kulinda mabaya ya mbele. Hapa kuna Unholly alliance!
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Huyu huu ndio uwezo wake wa mwisho kufikiri, inasikitisha.
   
 16. T

  Tiote Senior Member

  #16
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hili ndilo linalohitaji maandamano na people's power ya kikwelii! Siyo maandamano ya kiini macho na kumsema jk wakati wahusika mnakula nao na kuwasiliana, na hata kuchangia gharama za maandamano!
   
 17. T

  Tiote Senior Member

  #17
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli unauma! Mkuki kwa nguruwe kaka?
   
 18. shemasi

  shemasi Member

  #18
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtumishi wa Mungu nakemea kwa nguvu zote wanasiasa wa aina hii.
  wanasiasa wanatakiwa kutanguliza maslahi ya wananchi mbele na sio faida zao za kisiasa.
   
 19. n

  ndutu Member

  #19
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amen Mtumishi wa bwana!
   
 20. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #20
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sangara,
  mbona anaachiwa kuzurura mitaani kama mateja wa pale manyanya kinondoni,yani sheria aichukui mkondo wake? au kama anavyojigamba kwamba ungozi uliopo sasa( wa ******) kauweka yeye kwa pesa yake(pesa iliyoibiwa benki kuu na mshirika wake rostam) na sio kura za wananchi

  sie kama wananchi tueleweje uongozi kwa uliopo(******) kwa ku amuru majeshi ya shugulikie majangiri wa mbugani na kuacha majangiri hawa mitaani?
   
Loading...