Kwa kufuatilia malumbano na mijadala inayoendelea katika uwanja wa siasa sasa hivi, ni rahisi kuhitimisha kwamba harakati za kurithi hatamu za uongozi wa nchi hii mwaka 2015 zimeanza. Wale wanaowania tayari wameshaanza harakati za kujiweka vizuri. Wanafanya hivyo ama kwa kujifagilia, kujisafisha (kama ni wachafu) au kuwachafua wenzao kama wanawaona ni tishio. Hili linatekelezwa kwa kutumia tsnia ya habari vilivyo na kwa hali ilivyo sasa, wengi wa waandishi wamepoteza maadili na hata weledi wao, wengi wakijikuta wakitumika katika harakati hizo.
Katika siku za karibuni, tayari tumeshuhudia uyoga wa magazeti na majarida mapya yakimea na kuwaongezea mzigo wasomaji. Moja kati ya majarida hayo ni lile la UMOJA ambalo limeingia mtaani kwa kishindo. Katika toleo la kwanza, jarida hilo lilitoka na picha za maandamano ya CDM kule Arusha lakini kwa ndani, ikatoka makala ya mwanasiasa anayezungumziwa sana hapa nchi - Edward Lowassa. Wamiliki wa jarida hili wamejitambulisha kama Absalom Kibanda, mhariri mtendaji wa Tanzania Daima na mwanasheria Masatu Makaki. Wengine walioshiriki ni waandishi waandamizi wa gazeti la Tanzania Daima na Sayari, ambao hatujui kama ni waajiriwa rasmi au wanapiga 'deiwaka'.
Habari zilizopatikana ni kwamba jarida hili litajivua gama karibuni na kuwa gazeti la kila siku na mdomo mahsusi wa Lowassa katika harakati zake za kuingia ikulu. Litatumika pia kuwatia adabu wanaharakati wa mapambano dhidi ya ufisadi na tayari mwanasiasa huyu ameshatoa ofisi, samani na fedha za kuendeshea gazeti hili ambao ofisi zake ziko huko mikocheni, Dar es Salaam.
Swali la kujiuliza ni kwamba je, Msajili wa Magazeti anayaangaliaje magazeti haya na haoni kwamba haya ni sumu kwa umoja na amani ya nchi yetu? Je, ni sahihi kwa mtu au kikundi cha watu kuanzisha chombo cha habari maalum kwa ajili ya kusifia mmiliki au kuwachafua wale ambao anatofautiana nao kimisimamo? Vipi kuhusu waandishi wanaotumika kufanikisha mapango huo haramu? MCT na MOAT hawana mchango katika hili?