Uwingi wa damu mwilini

dah kwel binadam tunatofautiana,,yaan wewe unahitaj kupunguza damu mm nahita iongezeke doh

Kama unahitaji kuongeza damu siyo kazi kubwa ndugu.
1. Hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku, usisubiri dehydration (kukaukiwa) kiasi cha mkojo kuwa wa njano
2. Usikose matunda kwenye mlo wako wa siku, lakini kadiri iwezekanavyo kula matunda in an empty stomach. Usile matunda wakati unabugia ugali au wali.
3. Usikose mboga za majani kwenye mlo wako wa siku, alafu zipikwe vizuri..
4. Epuka kula vyakula vya kukaanga sana na mafuta. Mimi napenda kula vyakula vya asili na napika kwa kuchemsha badala ya kukaanga. Ukija kwangu hukosi vitu kama viazi, karoti, mchicha, ndizi.
5. Epuka vileo na uvutaji wa sigara na vitu vingine vinavyoambatana na hivyo.
6. Epuka kunywa soda mara kwa mara.

Kwa mtazamo wangu naona kama hauna ugonjwa unaokusumbua, kuongeza damu ni rahisi sana tena kwa gharama ndogo sana. Ishi maisha ya asili, epuka fast food hazisaidii sana.
 
mkuu hivo vyote nmefanya lakn wap hii mara ya nne sasa naishiwa damu, mpaka nahis nakuf
 
Kuna sehemu nilipima nimeambiwa damu damu yangu ni nyingi ipo 22
 
Damu ikiwa nyingi inakuwa nzito!!! Umenitisha as nina tatizo la damu kuzidi mara kwa mara!!
 
mkuu hivo vyote nmefanya lakn wap hii mara ya nne sasa naishiwa damu, mpaka nahis nakuf

Umeshawahi kutumia juice ya beetroots? Ile nasikia ni kiboko kwa kuongeza damu
 
Umeshawahi kutumia juice ya beetroots? Ile nasikia ni kiboko kwa kuongeza damu
yaan mkuu mpaka kaz nashndwa kufanya je minyoo inamaliza damu halaf hiyo beetroots kwa mwanza inapatikana wap
 
Imeeleweka sana na asante kwa mchango wako,

Swali: Wanawake uingia period na wana bleed inakadiliwa ni nusu kikombe cha chai jee ni mechanism gani inahusika ku fulfil damu iliyopotea kwenye hedhi?
 
Mkuu jaribu kwenda hospitali binafsi ufanye vipimo zaidi. Kuongezewa damu mara nne si jambo la kawaida.
 
ugonjwa nilionao kwa sasa nikwenye viungo kama mikononi kwenye maungio nasikia kama vtu vnasagana pia mgongo ukikaa kdogo ukijinyoosha unasikia kha kha kha kwenye kiuno pia hata kweny vdole vya miguu na mikonon
Check magonjwa nyemelezi
 
Imeeleweka sana na asante kwa mchango wako,

Swali: Wanawake uingia period na wana bleed inakadiliwa ni nusu kikombe cha chai jee ni mechanism gani inahusika ku fulfil damu iliyopotea kwenye hedhi?
Ndo maana hata rates zao ziko chini!
Pili damu wanayopoteza haitishi kiasi cha kuweza kushusha sana Damu labda isiwe Normal i.e Kiwango chake na siku zake zipitilize.

Isitoshe process nzima ya utengenezaji damu iki detect damu kushuka inaangalia kama una viambata i.e madini chuma hivo inatengeneza cell damu za kutosha kulipiza zile zilizopotea

Kama hauna madini chuma ya kutosha au folic acid hauna mwilini utengenezaji huu utakwama!
 
Shukrani mkuu.
 
Imeeleweka sana na asante kwa mchango wako,

Swali: Wanawake uingia period na wana bleed inakadiliwa ni nusu kikombe cha chai jee ni mechanism gani inahusika ku fulfil damu iliyopotea kwenye hedhi?

Niliwahi kuelezwa na daktari kwamba wale wanaotoa damu salama huwa wanatoa takriban nusu lita. Mara baada ya kutoa damu, ndani ya masaa 24 kama atakunywa maji ya kutosha na kula vyakula vinavyotakiwa basi anakuwa amerudisha body fluid (majimaji ya mwili) katika ujazo ule ule. Isipokuwa, kuna zile chembechembe tatu zinazounda damu yaani white blood cells, red blood cells and plateless zenyewe zinajirejuvinate (zinajirudisha kwenye kiwango chake baada ya wiki tatu. Ndiyo maana baada ya kutoa damu, unaweza kwenda tena kutoa damu baada ya mwezi mmoja bila madhara yoyote.

Kwa kusema hivi, mwanamke anayetoa damu nusu kikombe cha chai wakati wa hedhi hicho ni kiwango kidogo sana na anaweza kurejesha ndani ya siku chache sana. Hakuna madhara yoyote kama afya yake iko sawa
 
yaan mkuu mpaka kaz nashndwa kufanya je minyoo inamaliza damu halaf hiyo beetroots kwa mwanza inapatikana wap

Beetroots inapatikana sokoni wanapouza mboga za majani. Sijui kama unaifahamu yenyewe ipo kama viazi lakini iko na shape kama kitunguu au carrot. Iko nyekundu damu ya mzee. Ingia kwenye google search utaiona ina faida nyingi sana mwilini, nina document kabisa ya faida zake na namna ya kutumia. Ni nzuri pia kwa akina mama wanaopata tabu ya bleed na maumivu.
 

Attachments

  • Beetroots 4.PNG
    63.9 KB · Views: 94
  • Beetroots 4.PNG
    63.9 KB · Views: 93
Asanteh sana kwa fafanuzi makini mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…