Chigurh
Member
- Apr 2, 2025
- 23
- 86
Kwa maoni yangu, kutokana na watu mbali mbali nliokutana nao hapa bongo, naona kama uwezo wetu wa kufikiri kama nchi upo chini sana. Hivyo basi, hata ungesema ufute kazi watu wote wa idara nyeti na muhimu ili uajiri wale wenye uwezo na ujuzi zaidi, bado ungetukana na changamoto ya kwamba hatuna watu kama hao wakutosha. Vyovyote vile, mambo yangebaki yale yale.
Tofautisha elimu na uwezo wa kufikiria. Ndio, watu wenye elimu mara nyingi huwa na uwezo wa kufikiri wa juu kidogo, lakini wapo wengi sana wenye elimu na uwezo wa kufikiri mdogo sana.
Kuzuiwa kwa mambo ya kidunia kutufikia imetufanya tudumae sana. Fikra zina banwa, ukijaribu kuleta mjadala, unawekwa ndani. Watu wengi bongo hawajui yanayoendelea duniani au jinsi watu wengine wanavyofanya mambo yao. Ndo maana unapata maswali kama "Nani aliwaruhusu Cnn kurusha satelite bila kibali"
Dunia sio Tanzania tu. Mengi yanaendelea huko nje, na mengine yamepita na historia. Jitahidi kutumia mtandao kujielimisha kisayansi, teknolojia, na kisiasa pia. Pata exposure ya mambo tofauti tofauti ambayo pengine hujawahi sikia. Vinginevyo, tutabaki tunasema waarabu wanakuja kutusaidia, na wakati hao wenyewe wanakimbilia kwa wazungu.