figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
1. Fikiri kwa umakini mpaka ujue nini unahitaji katika maisha yako kwa sasa, wakati ujao, wakati uliopo na wakati ambao hautakuwepo.
2. Usiishi kwa kuiga bali uishi kwa nidhamu ya kuheshimu kila ulichonacho na muelekeo wa ndoto zako uliouchagua ndio uwe ndio dira yako
3. Hata kama una mipango mikubwa ya kujenga dunia yako, kuanza na ulichonacho bila kujali udogo wake ndiko kutakufikisha huko. Akili yako, matamshi yako na matendo yako ndivyo vitakupeleka huko
4. Uwezo ulioumbwa nao ni mkubwa sana. Jitahidi kutumia uwezo mkubwa uliopewa ili utimize makusudi ya Mungu kukupa uwezo huo.
5. Hakikisha kila kinachopita mkononi mwako kinaleta mabadiliko bila kujali ni ya ukubwa gani.
6 Kila tendo lina athari chanya au hasi kwa maisha yako. Hakikisha kila tendo linaboresha maisha yako na epuka matendo yanayokudhoofisha
7. Usitumainie ajira maana ajira huanza baada ya kufikisha miaka 18 na inakoma ukiwa na miaka 55-60. Wewe tumaini uwekezaji maana unaweza kuuanza ukiwa na mwaka mmoja na uwekezaji wako ukadumu hata baada ya kufa.
8. Epuka makundi na marafiki wasiojua wanakokwenda maana ukiwafuata mtapotea wote na dunia itawasahau
9. Mshirikishe Mungu mambo yako yote maana yeye amekuumba ili utawale. Ukimshirikisha atakuonesha wapi utawale
10. Usitelekeze kipaji au uwezo wowote wa kipekee ulioumbwa nao na kudandia vipawa vya watu wengine kuepuka utumwa.
11. Epuka kuwa na pesa ambayo haizalishi lakini epuka zaidi kutafuta pesa ambayo hujui cha kuifanyia maana itakuangamiza
12.Usijenge urafiki na uoga maana hakuna mafanikio kwa waoga
13. Usikurupuke kny Jambo bila kupata taarifa za kina au mtu wa kukuongoza katika jambo hilo
14. Kamwe usiishi kwa bajeti za dharura bali uwe na mpango maalumu wa matumizi
15. Usipoteze muda kutafakari na kujadili maisha ya watu wengine wakati maisha yako yanagalagala maana huyafikirii wala kuyajadili.