Uwezekano wa kilimo cha Karafuu, Tanga, Lindi na Mtwara

fungafunga

Senior Member
Mar 30, 2010
116
155
Ndugu wanajamvi.

Naomba wataalamu wa kilimo wanijibu swali hili muhimu ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa miaka mingi. Kama karafuu inastawi vizuri unguja na pemba ambayo ni kisiwa chenye hali ya hewa na udongo unaofanana na pwani ya tanzania bara hasa mikoa ya Tanga, Lindi na Mtwara.

Hivi hakuna uwezekano zao hili likawa linastawi katika maeneo haya pia?
 
Mkuu hata huko Lina stawi vizuri TU sijui kwanini hawajiongezi? Hapa Dodoma TU ndo pa kame na yanastawi
 
tanga wanalima sana karafuu iliki amdalasini n pilipili manga kwa mtwara sijajua ila pia mkoa wa morogoro wanalima sana kalafuu iriki amdarasini vanira pilipili manga tena kwa wingi sana kama karafuu asaivi kiln 9000 na soko amna kilimo chenye ela nyanya ukiotoe unaweza kupga ela sna
 
Mkuu habari

Nitakujibu nikiwa kama extension officer

Ili ulime unahitaj kujua mambo mengi na sio kubashiri
Mazao hukubali sehem kutokana na hali ya hewa,udongo,n.k sasa unapozungumzia Kwa haraka haraka kwamba Zanzibar na lindi au mtwara zinafanana umeangalia vigezo gani?

Je umepima sample za udongo umekuta sawa?

Umeangalia hali ya hewa?

Uoto wa asili au?

Umewahi jiuliza kwnn kusini wanalima sana korosho na Ufuta+karanga?

Basi tambua kua kilimo ni science kwahyo huwez kupanda kitu bila kukifanyia utafiti ukijua alkaline na acidity ya udongo ndio chanzo cha kujua Aina gan ya zao litastawi
 
Ndugu wanajamvi.

Naomba wataalamu wa kilimo wanijibu swali hili muhimu ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa miaka mingi. Kama karafuu inastawi vizuri unguja na pemba ambayo ni kisiwa chenye hali ya hewa na udongo unaofanana na pwani ya tanzania bara hasa mikoa ya Tanga, Lindi na Mtwara.

Hivi hakuna uwezekano zao hili likawa linastawi katika maeneo haya pia?
Spice zinastawi sana katika mwinuko hivyo bhas uwe unajua Visiwa hasa pemba inasemekana iko juu yaani imeinuka lakini inapitwa na mkondo wa bahari wa baridi (Cold sea currents) ukiangalia Muheza au Lushoto ziko juu na mwisho Morogoro vijijini au Mvomero (katika majaribio) yote ni maeneo ya juu.
Sijaelekea kwenye masuala ya joto,udongo na tabia zingine ila hili litakuongoza kunielewa.
Mtwara labda Newala na maeneo ya chiwata (Makonde plateau) na Lindi ni Rondo plateau kuanzia Ntauna mpaka Namupa Namupa hivi....
 
Back
Top Bottom