Uwepo wa taarifa za kutisha juu ya mbunge hilda ngoye.

mwakajilae

Member
Mar 11, 2011
58
46
Kuna tetesi za kuendelea kushamiri kwa vitendo vya unyanyapaa kwa walemavu,taarifa hizi zimepatikana kutoka kwa wanakijiji anachoishi Mh Hilda Ngoye(mb) Viti maalumu CCM.,Wakazi wa Kiijiji cha Kikota katika Wilaya ya Rungwe wamemlalamikia Mh Mbunge huyo mwenye mtoto wake wa kwanza wa kiume ambaye ni mlemavu,kuendelea kumuweka ndani zaidi yamiaka ishirini sasa,kinyume na tamko la haki za binadamu,huku huyu mbunge akiwa katika chombo kiubwa cha kutunga sheria na kuwasihi watanzania kuacha kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha wanakuwa sehemu ya jamii na wanapata hudumaote zilizo za msingi zinazo kidhi mahtaji yao,huyu mbunge kwake hili ni kinyume,anazungumza asiyoyatenda,sasa ni wakati muafaka wa wanaharakati kulifuatilia suala hili kwa kina,kuhakikisha wanafika kijiji cha KIkota,kata ya Kiwila wilayani Rungwe ili tuweze kumjumuisha na jamii huyu mwenzetu mtoto wa kumzaa wa mama Hilda Ngoye(mb).,tuhakikishe anahesabiwa katika sensa ya mwaka huu.

Wanakijiji cha Kikota walionyesha maskitiko makubwa juu ya hali ya mbunge huyo kumfungia mwanaye ndani ya nyumba yake kwa mudamrefu sasa.
 
Mtoa uzi endelelea kutujuza ni ulemavu wa aina gani aliokuwa nao huyo kijana ili tupate pa kuanzia
 
Inategemea anamfungia kwa maana ipi, inawezekana anafanya hivyo kama njia ya kumlinda maana hali imebadilika sana siku hizi. Lakini kama anamfungia kwa njia ya Kinyanyapaa, basi hilo halitakuwa na tafsiri nyingine zaidi ya Ushirikina, na hilo litatupelekea kuanza kuhoji imekuwaje huyu mama anapata vyeo vya kisiasa mara kwa mara na kupima ufanisi wake.
 
Kumfungia mtu kwa sababu zozote zile ni unyanyapaa. Kama ni albino kuna shule zao kama hasikii kuna shule zao kama ana mtindio kuna sehemu zao na kama zimemruka kwa nini asipelekwe mirembe badala ya kumfungia ndani kama ni kweli anafungiwa ndani.
 
Unataarifa tofauti na alichosema?. Hata hivyo nijuavyo umbea ni habari itolewayo kuhusu mtu fulani bila ridhaa yake na huyo mtu alipenda iwe siri isijulikane. Nataka kuamini kuwa unaujua ukweli na kilicholetwa hapa ni ukweli uliotaka usijulilkane.

Oanisha mantiki inayojengeka katika kichwa cha habari hii na maneno mawili ya mwanzao ya habari yenyewe utaelewa.
  1. "Uwepo wa taarifa za kutisha...." Maana yake unataka kuleta habari iliyothitishwa au kutafitiwa na unamwondoa mashaka msoma juu ya ukweli wa taarifa yako. Sasa unapoanza kueleza kwa kusema "Kuna tetesi...." it is a contradiction in terms.
  2. Kwenye tafsiri yako ya "umbea" ongeza hii: Hata kueneza sifa mbaya za mtu usizoweza kuthibitisha ni umbea

Nataka ujue kwamba simjui kabisa huyo anayemzungumzia na wala sina taarifa tofauti na anayoileza. Ni kwamba mleta mada kajichanganya.
 
nipo njiani kuelekea huko kitaeleweka tuu!!
 
Taarifa zinatisha kweli!

Ni kijana wa kiume,umri miaka zaidi ya 20,ni mtoto wake wa kumzaa,ni jumamosi ya wiki jana nilikuwako huko na kukutana na wanakijiji cha mbunge,nimezungumza na lika la wazee,wakanithibitishia hilo,ni ulemavu wa akili,wanakijiji wanasikitika lakini wanamuogopa mbunge kama mjuavyo mbunge anavyokuwa mfalme kijijini,binafsi sijamuona,ila wanakijiji ambao ni wazee ndiyo walio nijuza suala hilo.
Hili ni suala zito,najua hapa jamvini kuna wataalamu wa masuala mbalimbali,tuende tukalitafiti ndipo tuje kukanusha ama kusikitika tukiwa na suluhu,mbaya ni kwa mbunge kujifanya ana dunia yake inayoruhusu amnyime ubinadamu mwenzie na kumfanya kama mnyama wa kufugwa afugwaye.
 
TAARIFA YA UONGO NA UZUSHI
inaelekea umetumwa na chama chako cha Chadema kusambaza uongo huu na uzandiki.
Hii ni roho mbaya sana na tunakuombea na wewe ukilema ili uonje adha hiyo.

Kwanza Mama Ngoye HAKAI Kikota, anakaa kijiji cha Mapandapanda, Kiwira au Mwankenja,karibu sana na maerehemu John Mwankenja aliyeuwawa kwa visasi vya watu kama huyu anayeeneza pepo la uongo.
ULAANIWE!!!
 
Mtoa mada ni kama changu anayetumika kwa haja ya mwanaume kwa siku moja, baada ya hapo hahitajiki.
 
Mtoa mada ni kama changu anayetumika kwa haja ya mwanaume kwa siku moja, baada ya hapo hahitajiki.

Tusibishanie eneo la tukio,tubishanie uwepo ama kutokuwapo kwa tukio,huu ndyo mjadala,pia kimaadili ya mjadala,suala lolote lenye mashaka ni lazima tulijadili kwa mapana na kulifanyia uchunguzi wa kina juu ya uongo au ukweli huo.
anailikuwa huko,nimeambiwa na wanakijiji,tulijadili then tulichunguze.
Endapo taatrifa hizi zitakuwa za uongo,ntamwomba msamaha huyu mama,kwangu huyu sina haja ya kumsingizia,kwasababu sinachochote cha kumsingizia kisiasa,huyu mama hawezi kuwa na utisho wowote wa kisiasa kwangu mpaka ni msingizie,ingekuwa ni hivo ningewachafua majabari ya kisiasa mkoani mbeya kama Mwakyembe na Mwandosya ili wasikubalike machoni kwa Watanzania.Naarifu hili ili kusimamia wasio na uwezo wa kupaza sauti zao kama huyu kijana wa mama huyu
Tuchunguze ,tujadiliane.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…