Uwekezaji: PPF yaendeleza eneo la ekari 5 jijini Dar

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,169
1,073
Ndugu zangu, hii si siri ila nimeamua tu kuwanong'oneza tu, sio tetesi ni taarifa za kweli na zinazoweza kuthibitishwa kwa nyaraka, vielelezo pia ushahidi.. Plz naomba msininukuu vibaya.. sijasema hili ni jipu, tezi, busha wala uvimbe.. hamkawii kunisingizia..

Ni taarifa zenye mapana ya ukweli unaoweza kuthibitishwa kuwa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya umma japo kwa sasa wahusika na kuhifadhi na kulipa pensheni kwa sekta binafsi na zisizo rasmi.. Katika mipango mikakati ya kuwekeza michango ya wanachama wake kupitia sekta ya ujenzi wa nyumba, majumba n.k hivi karibuni mfuko umenunua kiwanja pembezoni mwa barabara ya Sam Nujoma {Mwenge-Ubungo} toka kwa kampuni binafsi kwa bei ya Dola za Kimarekani Milioni 8 sawa na zaidi ya bilioni 16.

Kwa ufahamu wangu mdogo sana, hizi ni pesa nyingi sana kutumika kununua kiwanja pakee katika maeneo husika.. Yamkini huu ni muendelezo wa maamuzi yasio na weredi, uzalendo, harufu ya ubadhirifu, kujinufaisha na tuhuma za wizi, ufisadi pia matumizi mabaya ya madaraka toka kwa viongozi/wafanyakazi/watumishi wanaopewa dhamana husika.

Kumekuwepo na kawaida yenye mizizi kwa wafanya manunuzi toka taasisi za Serikali {Mashirika ya Umma,Wizara na Wakala} kuweka cha juu mbali na asilimia 10 ambayo wamekuwa wakipata kwa lazima toka kwa wazabuni wenye kufanya kandarasi ktk taasisi husika.. Mzabuni asietoa asilimia 10 huyo amekuwa akikanwa, nyanyapaliwa, tengwa na zabuni zake kutupwa ama malipo yake kucheweleshwa kwa makusudi kabisa.

Kwa hili la PPF yamkini na taasisi zingine zenye kufanana na hii, Michakato ya manunuzi ya viwanja vya uwekezaji imekuwa ikihusisha idara zaidi ya moja katika kufikia maamuzi kama Miradi /Uwekezaji,Manunuzi {PMU}, Masoko {Marketing}, Sheria, Uhasibu na Utawala..

Hivyo basi kwa kuwa roho ya urafi, tamaa, wizi, ubadhirifu imekuwa mtambuka kwa kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki {Mbuzi hula majani kwa urefu wa kamba yake} vivyo hivyo mapana ya chajuu huwa makubwa zaidi ili kukonga nyoyo za washiriki.

Hili laweza kuthibitishwa na ukweli wa mali wanazomiriki wahusika wakuu wa hii michakato kutofautiana mno na uhalisia wa vipato vyao halali na pia mapato yao ,vitega uchumi vyao kuongezeka mara tu malipo yanapofanywa kwenda kwa wazabuni walio katika miradi dili .

Uchunguzi mahsusi waweza baini taarifa za kina kwenye miradi yote mikubwa inayohusisha matumizi ya mabilioni ya kodi, michango, misaada, ruzuku kama Ujenzi wa Bomba la gesi, Ununuzi wa Vivuko, TPA, RITA, TCRA, UTT, NSSF, PSPF, SUMATRA, DART, TANESCO, TFDA, MSD, VETA, Gaming Board, NMB, EPZA, TANROADS, TBA, REA, WMA, TANAPA, NFRA, MNH, TPF, TPDC, TPDEF, UDSM, DIT, TAMISEMI {Halmashauri, DAWASA, Mamlaka za maji, Wizarani...n.k.

Uchunguzi uende mbele zaidi hata kuwabana wafanyabiashara wasio na maadiri wanaofanya biashara na serikari..

Mfano ktk hili la PPF je baada ya malipo nani na nani waligawiwa,walitumiwa fedha,walilipwa,walitafunishwa mishkaki ama kuyweshwa mvinyo wa ushindi...yale ya Mkombozi na Tegeta Escrow yaweza jitokeza ama la ya viroba, lumbesa, Visandarusi {Stanbic}

Nakiri mimi si mtakatifu, Si msafi, Si Mzalendo wa kutukuza... Tanzania inapaswa kufanyiwa kupasuliwa na kutakaswa kweli kweli... Mwenyezi Mungu awatie nguvu na maarifa viongozi wetu wenye kiu na nia ya dhati kurejesha heshima, utu, usawa na heshima kwa wote.

=========
UFAFANUZI toka kwa mdau:

Eneo hili lipo mkabala na Mlimani City karibu na Kobil Oil Station na lina ukubwa wa ekari 5. Lilinunuliwa kwa Bilioni 12
 
Ni taarifa zenye mapana ya ukweli unaoweza kuthibitishwa kuwa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya umma japo kwa sasa wahusika na kuhifadhi na kulipa pensheni kwa sekta binafsi na zisizo rasmi..Katika mipango mikakati ya kuwekeza michango ya wanachama wake kupitia sekta ya ujenzi wa nyumba,majumba n.k hivi karibuni mfuko umenunua kiwanja pembezoni mwa barabara ya sam nujoma {Mwenge-Ubungo} toka kwa kampuni binafsi kwa bei ya Dola za Kimarekani Milioni 8 sawa na zaidi ya bilioni 16.

Kwa ufahamu wangu mdogo sana hizi ni pesa nyingi sana kutumika kununua kiwanja pakee katika maeneo husika..Yamkini huu ni muendelezo wa maamuzi yasio na weredi,uzalendo,harufu ya ubadhirifu,kujinufaisha na tuhuma za wizi,ufisadi pia matumizi mabaya ya madaraka toka kwa viongozi /wafanyakazi/watumishi wanaopewa dhamana husika.

Kumekuwepo na kawaida yenye mizizi kwa wafanya manunuzi toka taasisi za Serikali {Mashirika ya Umma,Wizara na Wakala} kuweka cha juu mbali na asilimia 10 ambayo wamekuwa wakipata kwa lazima toka kwa wazabuni wenye kufanya kandarasi ktk taasisi husika..Mzabuni asietoa asilimia 10 huyo amekuwa akikanwa,nyanyapaliwa,tengwa na zabuni zake kutupwa ama malipo yake kucheweleshwa kwa makusudi kabisa.

Kwa hili la PPF yamkini na taasisi zingine zenye kufanana na hii,Michakato ya manunuzi ya viwanja vya uwekezaji imekuwa ikihusisha idara zaidi ya moja katika kufikia maamuzi kama Miradi /Uwekezaji,Manunuzi {PMU},Masoko {Marketing},Sheria,Uhasibu na Utawala..Hivyo basi kwa kuwa roho ya urafi,tamaa,wizi,ubadhirifu imekuwa mtambuka kwa kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki {Mbuzi hula majani kwa urefu wa kamba yake} vivyo hivyo mapana ya chajuu huwa makubwa zaidi ili kukonga nyoyo za washiriki.

Hili laweza kuthibitishwa na ukweli wa mali wanazomiriki wahusika wakuu wa hii michakato kutofautiana mno na uhalisia wa vipato vyao halali na pia mapato yao ,vitega uchumi vyao kuongezeka mara tu malipo yanapofanywa kwenda kwa wazabuni walio katika miradi dili .Uchunguzi mahsusi waweza baini taarifa za kina kwenye miradi yote mikubwa inayohusisha matumizi ya mabilioni ya kodi,michango,misaada,ruzuku kama Ujenzi wa Bomba la gesi,Ununuzi wa Vivuko,TPA,RITA,TCRA,UTT,NSSF,PSPF,SUMATRA,DART,TANESCO,TFDA,MSD,VETA,Gaming Board,NMB,EPZA,TANROADS,TBA,REA,WMA,TANAPA,NFRA,MNH,TPF,TPDC,TPDEF,UDSM,DIT,TAMISEMI {Halmashauri},DAWASA,Mamlaka za maji,Wizarani...n.k.

Uchunguzi uende mbele zaidi hata kuwabana wafanyabiashara wasio na maadiri wanaofanya biashara na serikari..Mfano ktk hili la PPF je baada ya malipo nani na nani waligawiwa,walitumiwa fedha,walilipwa,walitafunishwa mishkaki ama kuyweshwa mvinyo wa ushindi...yale ya Mkombozi na Tegeta Escrow yaweza jitokeza ama la ya viroba,lumbesa,Visandarusi {Stanbic}..

Nakiri mimi si mtakatifu,Si msafi ,Si Mzalendo wa kutukuza...Tanzania inapaswa kufanyiwa kupasuliwa na kutakaswa kweli kweli...Mwenyezi Mungu awatie nguvu na maarifa viongozi wetu wenye kiu na nia ya dhati kurejesha heshima,utu,usawa na heshima kwa wote....
 
Labda ni U.S.A umekosea au! Maana viwanja vya maeneo hayo havina thamani hiyo
 
hiyo pesa ni saw a kama wameinunua mlimani city mall na viwanja vyake. Lakini kama ni plot ya 40/40 pesa mingi sana
 
Hata yule mwekezaji sijui wa South Africa anayesemekana kauziwa kisiwa hajalipa hiyo hela ,16B ?? Haki ya Mungu Tanzania tuna safari ndefu
 
PPF kuanzia utoaji wa ajira mpaka utoaji wa mafao na uwekezaji ni ful Ubadhilifu...pale makao makuu utakutana na majina ya watoto wa mabalozi na makatibu wakuu na watoto wa wakubwa wa wakuu wa jeshi la polis.
 
Mimi nakaa jirani na hapo waliponunua na wameshaanza kujenga jengo la ghorofa 30.. Kiwanja ni kikubwa tu
 
..mojawapo ya jipu JPM anatakiwa kulitumbua ni bei za juu sana za viwanja na nyumba(real estate).... Hii industry kwa kweli inaendeshwa kwa ufisadi mkubwa Tz...na hamna regulation kabisa kwenye hili...haiwezekani bei ya kiwanja/Nyumba dar iwe kubwa kuliko London..ama New York..ama Beijing...mjini gani huu wa dar uwe na bei kubwa hivi ya viwanja/nyumba...wakati unanuka...na hata mvua ikinyesha tu haukaliki wala kupitika....something is very wrong with dar...
 
Ni kiwanja cha mpira (stadium) au cha kujenga?
Je kina ukubwa gani?
Mbona hawa watu wanatumia hela ovyo hivi
 
Mimi nakaa jirani na hapo waliponunua na wameshaanza kujenga jengo la ghorofa 30.. Kiwanja ni kikubwa tu
Oooh! Kumbe ndo pale wamefunga nondo tayari, kiwanja kikubwa kile na kipo eneo karibu na mlimani city lazima kitakuwa bei kubwa.
 
Oooh! Kumbe ndo pale wamefunga nondo tayari, kiwanja kikubwa kile na kipo eneo karibu na mlimani city lazima kitakuwa bei kubwa.
Kiwanja ni kikubwa sana zamani kulikuwa na kampuni ya kufyatua matofali pale... Kwa eneo lile dola milion 8 siwezi kubisha
 
Back
Top Bottom