Uwekezaji na ujinga wetu wa milele!

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Salamu wanajamvi!

Naam! naona tunarudia makosa yetu ya toka enzi na enzi.Mara hii tupo kwenye mvutano mkubwa usio na sababu na wawekezaji wa migodi ya dhahabu.Mabepari wana akili sana.Hawaanzi shughuli yeyote ya kiuchumi inayo hitaji uwekezaji wa mtaji mkubwa bila kujiridhisha kwamba mikataba wanayo wekeana na Nchi husika italeta faida.Mikataba ile watu tulio waamini walisaini kwa niaba ya Nchi na Bunge likapitisha.leo tunasema wanatuibia.Wapo wanao sema serikali iko sawa kuzuia usafirishaji wa mchanga, na wenye akili wachache wanasema hapana, kuna kitu hakiko sawa mahali fulani.

Kifupi ni kwamba ukisha ingia mkataba maana yake pande zote lazima zitekeleze vipengele vya mkataba kama ulivyo.Kama kuna upande mmoja umezinduka na kuona mkataba hauwafaidishi,dawa siyo kuusitisha bila kufuata taratibu! Mikataba hii tuliikubali wenyewe kwa kusema tuna jenga mazingira bora ya uwekezaji.Na kwa hakika tulikuwa na mazingira bora kwa mabepari kuja kuchukua rasilimali zetu kwa amani kabisa.kupanga ni kuchagua.

Kwanini tunarudia makosa kila wakati? Wazungu hawa wana mikataba halali ya kuchimba Dhahabu na madini mengine, mikataba hiyo na sisi tunayo,kwanini tuingie kwenye hatari ya kulipa fedha nyingi kama fidia ya hasara wakati njia bora ya kufikia muafaka ipo? kule wanako pakia ule mchanga hakuna mamlaka zetu zinazo dhibiti kuona Nchi haiibiwi? Kuna tatizo mahali.

Mambo ya kisheria tukiyatatua kisiasa hatufiki mbali, tunajidanganya.Tupende tusipende ni lazima tufuate taratibu za kufikia maridhiano upya.Sera ya madini ilikuja wakati mikataba ya kuchimba Dhahabu imesha sainiwa na pande zote.Ndio maana tukahoji wakati ule kwanini tuna ruhusu uchimbaji wa madini kabla ya kupitisha sera ya madini?

Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba turudi kwenye meza ya majadiliano na wawekezaji. Hili halikwepeki. Wazungu wana hila sana na wana ushirikiano sana linapo kuja suala la kiuchumi na lenye masilahi kwao.Wakiungana kutusambaratisha hakika tutaangamia.

Wangapi wanajua kwanini mwalimu Nyerere aliamua kurudisha mashamba ya chai aliyo taifisha kwa Mwingereza?Wazungu waliungana hawakutaka kununua chai yoyote kutoka Tanzania, mwisho tukasalimu amri.Tufike mahali tutenganishe siasa na masuala ya uchumi.
 
Watu wanafikiri hiyo ni sawa na biashara ya nyanya..
Kimsingi tunajidanganya kuwa wakali wakati tumesha ingia mikataba.Wazungu hawakuwa wajinga kuhamisha vifaa vya kuchimbia dhahabu kutoka Ghana kuja kwetu. Walijua wamepata mali nyingi bure kabisa kwasababu ya tamaa ya watu walio pewa dhamana ya kuingia mikataba kwa niaba ya Nchi.Bunge pia lilipitisha kwa kishindo halafu leo tuna lalamika.
 
Salamu wanajamvi!

Naam! naona tunarudia makosa yetu ya toka enzi na enzi.Mara hii tupo kwenye mvutano mkubwa usio na sababu na wawekezaji wa migodi ya dhahabu.Mabepari wana akili sana.Hawaanzi shughuli yeyote ya kiuchumi inayo hitaji uwekezaji wa mtaji mkubwa bila kujiridhisha kwamba mikataba wanayo wekeana na Nchi husika italeta faida.Mikataba ile watu tulio waamini walisaini kwa niaba ya Nchi na Bunge likapitisha.leo tunasema wanatuibia.Wapo wanao sema serikali iko sawa kuzuia usafirishaji wa mchanga, na wenye akili wachache wanasema hapana, kuna kitu hakiko sawa mahali fulani.

Kifupi ni kwamba ukisha ingia mkataba maana yake pande zote lazima zitekeleze vipengele vya mkataba kama ulivyo.Kama kuna upande mmoja umezinduka na kuona mkataba hauwafaidishi,dawa siyo kuusitisha bila kufuata taratibu! Mikataba hii tuliikubali wenyewe kwa kusema tuna jenga mazingira bora ya uwekezaji.Na kwa hakika tulikuwa na mazingira bora kwa mabepari kuja kuchukua rasilimali zetu kwa amani kabisa.kupanga ni kuchagua.

Kwanini tunarudia makosa kila wakati? Wazungu hawa wana mikataba halali ya kuchimba Dhahabu na madini mengine, mikataba hiyo na sisi tunayo,kwanini tuingie kwenye hatari ya kulipa fedha nyingi kama fidia ya hasara wakati njia bora ya kufikia muafaka ipo? kule wanako pakia ule mchanga hakuna mamlaka zetu zinazo dhibiti kuona Nchi haiibiwi? Kuna tatizo mahali.

Mambo ya kisheria tukiyatatua kisiasa hatufiki mbali, tunajidanganya.Tupende tusipende ni lazima tufuate taratibu za kufikia maridhiano upya.Sera ya madini ilikuja wakati mikataba ya kuchimba Dhahabu imesha sainiwa na pande zote.Ndio maana tukahoji wakati ule kwanini tuna ruhusu uchimbaji wa madini kabla ya kupitisha sera ya madini?

Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba turudi kwenye meza ya majadiliano na wawekezaji. Hili halikwepeki. Wazungu wana hila sana na wana ushirikiano sana linapo kuja suala la kiuchumi na lenye masilahi kwao.Wakiungana kutusambaratisha hakika tutaangamia.

Wangapi wanajua kwanini mwalimu Nyerere aliamua kurudisha mashamba ya chai aliyo taifisha kwa Mwingereza?Wazungu waliungana hawakutaka kununua chai yoyote kutoka Tanzania, mwisho tukasalimu amri.Tufike mahali tutenganishe siasa na masuala ya uchumi.
Bunge lipi lilipitisha mikataba ya madini, gasi na mafuta?
 
Back
Top Bottom