Uwekezaji Kwenye Uber!

YonDu Udonta

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
723
569
Habari Wakuu!
Wakuu naomba kufahamu kwa undani biashara hii tukianzia na mtaji wake ambapo ni kununua chombo cha usafiri, uendeshwaji wake, faida zake, changamoto zilizopo!

Nina imani humu ndani kuna wataalamu watasaidia...

Karibu...
 
Gari yenye cc chini ya 1300 mwaka kuanzia 2005 kuja juu,kadi iwe biashara,Stika ya uber 80000,kibali cha jiji na TRA....ukitaka hesabu kwa siku 25000 service juu yako na mkataba ni kwa miaka 2 kwa siku 30000 service kwa dereva na vibali ni kwako!?changamoto bei zao hazieleweki zinapanda na kushuka,trafiki mabao,ajali na utunzaji madereva wengi ni wenge.....
 
Nashukuru Mkuu, hizi process kuanzisha nafatilia wapi?

Gari yenye cc chini ya 1300 mwaka kuanzia 2005 kuja juu,kadi iwe biashara,Stika ya uber 80000,kibali cha jiji na TRA....ukitaka hesabu kwa siku 25000 service juu yako na mkataba ni kwa miaka 2 kwa siku 30000 service kwa dereva na vibali ni kwako!?changamoto bei zao hazieleweki zinapanda na kushuka,trafiki mabao,ajali na utunzaji madereva wengi ni wenge.....
 
Gari yenye cc chini ya 1300 mwaka kuanzia 2005 kuja juu
CC za juu ya hapo na mwaka chini ya hapo hawahitaji au inakuaje mkuu...?

kadi iwe biashara,
Kusajili kadi ya biashara inakuwa ni kiasi gani mkuu...?

Stika ya uber 80000,kibali cha jiji na TRA
Kibali cha jiji pia gharama zikoje na TRA wanatoza vipi mkuu...? Na pia vipi kuhusu plate number ni lazma nyeupe au hata njano zinafaa...?

....ukitaka hesabu kwa siku 25000 service juu yako na mkataba ni kwa miaka 2 kwa siku 30000 service kwa dereva na vibali ni kwako!?changamoto bei zao hazieleweki zinapanda na kushuka,trafiki mabao,ajali na utunzaji madereva wengi ni wenge.....

Wao uber wanakata kiasi gani kwa kila trip na je kuna faida gani unapata ukiacha hela utakayoingiza kwa abiria utakaokuwa unapata mkuu...?

Natanguliza shukran zangu kwako kiongozi. Thanks a lot bro.
 
Kabisaaaa.
Yani hapo mmiliki unapata robo ya mahesabu na robo tatu anachukua dereva.

Hizo ni staili za upigaji wa waziwazi.

Mkuu hii Uber imekuja kuwa mbadala wa Taxi ambao ni directly abiria anakuja na unakubaliana nae gharama

Labda tuanzie apa, Taxi huwa zilikua zina rudisha shilingi ngapi kwa tajiri kwa siku?
 
Back
Top Bottom