Uwekezaji katika tanzania unamsaidia nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwekezaji katika tanzania unamsaidia nani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chegreyson, Feb 1, 2012.

 1. c

  chegreyson JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 736
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 60
  Kwa mtazamo wa kwangu mimi NIONAVYO NA ninavyoamini ni kwamba ,HAIWEZEKANI NA HAITATOKEA MGENI WA NJE AJE KWA MOYO MMOJA AIENDELEZE TANZANIA NA WATANZANIA KWA NJIA HII TUNAYOTUMIA SASA YA UWEKEZAJI.

  Pili mimi naamini ya kwamba msaada wowote utakaotolewa na wenzetu hasa wa magharibi ni lazima uwe na sababu na ujilipe.
  Wenzetu baada ya kukaa na kuona kwao hakuna ajira za tutosha na sehemu pekee ya kutoa hizo ajira ni dunia ya tatu ndipo wakabuni mradi huu wa uwekezaji.

  Linalotokea NI KWAMBA tatizo linaanzia kwenye kituo cha uwekezaji ambapo mwekezaji anaanza kupata nafuu au kusamehewa kodi kwa kuingiza mitambo yake.

  Pili hiyo mitambo akishaiwekeza anaanza kulipwa capacity charge,ambayo ni kubwa kuliko faida inayopatikana kutokana na uzalishaji wake.
  Tatu mikataba ya uwekezaji haiwekwi vipengele vya msingi kama Mkurugenzi akiwa ni mwekezaji basi iwe ni lazima kwa naibu wake awe mzalendo, na vitu kama hivyo.Hii ingesaidia kuwa na uhakika wa ajira kwa Watanzania pamoja na kumonitor mwenendo wa mwekezaji.

  Kibaya zaidi wawekezaji hawa account zao ziko nje ya nchi,kiasi kwamba kama taifa hatuwezi kumonitor rasilimali zinavyotapeliwa huku tukiangalia.
  Na kwa kuwa nchi yetu ni dhaifu kufuatilia vitu kama hivi ndio maana leo hii wawekezaji wakija, wanakuja kuanzia wafagizi mpaka maafisa wa juu.
  Sisi kama nchi hawa maelfu ya vijana wetu wanaomaliza vyuo kwa migomo tutawapeleka wapi.

  Kwa hiyo nawaomba viongozi wetu kubadilika nchi hii itajengwa na Watanzania na sio hawa wanaokuja kuchuma Tanzaniana kutuachia maradhi na mashimo.
   
Loading...