Uwaziri: Nabaki au niondoe mtukufu rais

nunu

Member
Apr 11, 2011
38
3
Katika kusoma magazeti na kupitia mitandao mbali mbali ya jamii kuhusu sakata la uundwaji wa baraza la mawaziri kunajitokeza ugumu wa nani atoke na nani apishe ukiondoa wale waliotajwa tangu huko Dodoma.

Katika baraza hili lililopo na kwa yale yanayosemwa kuhusu uwezo wa baadhi ya mawaziri kushindwa kujibu hoja za wabunge kikamilifu bungeni kuna haja ya wao kujipima kupitia ahadi za chama (election manifesto) wakati wa kipindi cha mchakato wa uchaguzi 2010. Mambo makuu na kwa hakika mahitaji makubwa ya wananchi yamejikita katika haya:

1. Umaskini
2. Ufanisi bora katika kila sekta
3. Huduma za jamii kama afya, elimu, miundombinu, masoko ya mazao nk
4. Ajira
5. Rushwa Haya hapo juu yalisemewa vema kabisa na CCM na kwa kweli ndio pingu kati ya mchaguliwa na mchaguzi na ni crosscutting issues kwa kila wizara ukitoa namba 3.

Tangu mawaziri wetu wachaguliwe wampatie JK taarifa juu ya vile walivyotekeleza katika hayo na kwa wale ambao watabaki watainuaje kiwango cha utekelezaji wa hayo, VIWANGO VILIVYOPO HAVITOSHI. Naamini kuna baadhi wameshindwa kutimiza kwa kutosoma au kutojali ahadi alizosema aliyewapa dhamana au kwa kupuuza au kutowajibika tu na hawa waombe kutoka bila ya kuogopa jamii itawasemaje; wabaki na uwakilishi wa majimbo kwani nayo ni kazi nzito tu.

Mwalimu Nyerere alisema kitendo cha kujikosoa si cha kujidharirisha bali ni cha kujiimarisha. Mheshimiwa waziri nawe zibane taasisi zilizo chini yako wakupe taarifa za namna wamekusaidia wewe kumwezesha Mkuu wa nchi kufaulu kuyatekeleza hayo aliyoyanadi wakati wa uchaguzi.

Kila mmoja AWAJIBIKE KIKAMILIFU.
 
Back
Top Bottom