Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, alipoulizwa CCM imepokeaje uamuzi wa Bw. Chenge alionekana kutokuwa tayari kuzungumzia suala hilo. "Uwaziri wa Bw. Chenge mimi unanihusu nini, Uwaziri kilikuwa ni kibarua chake kilikuwa kikimsaidia yeye na watoto wake, sasa CCM iseme nini? Alihoji Bw. Makamba na kuongeza: "Wewe kama unataka niulize mambo yanayohusu muafaka, kuna mambo mengi yanayohusu CCM," alisisitiza Bw. Makamba.
Chanzo:
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6415
Mmmh, ukiangalia Makamba hapo kajibu hovyo ila kasema ukweli pengine bila kujijua.
Ni ukweli kuwa u-Waziri wa Tz ni kwa faida ya huyo mtu binafsi na watoto wake. Hili Makamba na CCM wanalijua na ndiyo maana hawalivalii njuga kunapokuwepo na masuala ya wizi, ufisadi, uzembe kazini, rushwa, ku-forge degrees, n.k.
Jiulize watu kama akina Ngasongwa, Kingunge, Mungai, Nchimbi, Karamagi, Chenge, Lowassa, Kikwete, Msabaha, Mathayo, Mramba, Kahama, Keenja, n.k. wamesaidia nini na u-Waziri wao zaidi ya kujineemesha wao na watoto wao?
Kama u-Waziri ungekuwa ni kwa faida ya Taifa na/au chama, basi wote waliopo madarakani sasa hivi wangekuwa jela, na chama t(w)awala kingekuwa kinara wa kulaani maovu yanayofanywa na 'viongozi ma-waziri' hao.
Tumlaani Makamba kwa kusema ovyo ila tukubali kuwa kafunua kikombe kabla mwanaharamu hajapita.