Uwanja wa Taifa uboreshwe

akyo

Member
May 6, 2017
38
25
Habarin wa JF wenzangu.

Nikiwa kama mdau wa michezo hasa mchezo pendwa "soccer" huwa najaribu kufananisha viwanja vingi vya kimataifa na uwanja wetu wa TAIFA almaarufu Kwa Mkapa.

Nikivitazama viwanja vingi vya kimataifa vina feutures mbalmbali kama vile:

1. SCREEN

Sreen inayoonyesha matukio makubwa yanayoendelea wakati wa mchezo.Sreen hii inawasaidia mashabiki kuona matukio mbalmbali uwanjani hata kama goli limefungwa na mshabiki hakuliona tukio,Screen inaonyesha replay(marudio) ya goli lilivyofungwa.

Uwanja wetu wa taifa Sreen yake inaonyesha tu scrore.Ukiwa kama mshabiki, hasa ukikaa viti vya mzunguko na goli likafungwa, unaweza anza kuuliza kwa wanaosikiliza redio kuwa nani kafunga? IIi hali upo uwanjani.

2. MATANGAZO YA KIELEKTRONIKI
Haya ni chanzo kizuri cha mapato kwa Tim au Shirikisho na nchi kwa ujumla.

Uwanja wa taifa umekosa matangazo hayo.

USHAURI WANGU.
TFF na Wizara ya michezo wafanye haya:

1. Warekebishe ile screen iweze kuonyesha matuiko uwanjani. Hii itaongeza mwamko wa watu kujaa uwanjani hata kwa timu ndogo, ukitoa hawa kulwa na doto

2. Watengeneze matangazo ya kielectronic uwanjani. Hii itasaidia taasisi na asasi mbambali kutangaza natangazo hayo,na kuwa chanzo kingine cha mapato kwa serikali na TFF.

NAWASILISHA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri mzuri sana ila kwa jinsi viongozi wetu walivyo watasubiri mpaka magufuli awambie fanyeni hivyo ndo watachukua hatua
 
Maboresho ya kwanza yawe ni vyoo. Huwezi kuwa na uwanja kama ule ukakosa vyoo.

Wasimamizi wa ule uwanja ni watu wa ajabu sana, vyoo vinaharibika badala ya kutengeneza wanafunga.

Basi hata hivyo vichache vinavyofanya kazi miundombinu ya maji ni msamiati mwingine.
 
Back
Top Bottom