Patashika ya michuano ya Simba Super Cup inafikia mwisho leo January 31, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ambapo Mnyama Mkali Simba SC inapepetana na Mabingwa wa Afrika mara tano TP Mazembe kutoka Congo.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku kila timu kuhitaji ushindi na kunyakua taji hilo, Simba SC aliweza kushinda mchezo wa kwanza huku TP Mazembe akipoteza.
Je TP Mazembe atakubali kupoteza michezo yote miwili na Simba SC kushinda michezo yote miwili? Jibu ndani ya dakika 90 za mchezo huu.
Kumbuka mtanange huu ni kuanzia saa 11: 00 Usikose Ukasimuliwa.
.... Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Kikosi cha Simba SC
Beno Kakolanya
David Kameta
Mohamed Hussein
Pascal Wawa
Joash Onyango
Taddeo Lwanga
Miraji Othuman
Rally Bwalya
Chris Mugalu
Claotus Chama
Luis Miquissone
Subs:
Salim, Gadiel,Kennedy, Morrison, Mzamir, Ajibu, Kagere, Kahata, Lokosa, Peter, Chikwende
View attachment 1690873