Uwajibikaji Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwajibikaji Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fmesanga, Feb 25, 2009.

 1. f

  fmesanga Member

  #1
  Feb 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 14
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uwajibikaji ni kitu muhimu sana kwa nchi ye yote ile inayotaka maendeleo na ustawi wa kiuchumi. Kila mtendaji au kiongozi katika eneo lake la kazi anatakiwa awe na dhamana ya yale yote yanayotokea katika eneo lake. Hii ni pamoja na kubeba dhamana ya wale walio chini ya huyo mtendaji/kiongozi. Maana yake nini?

  Maana yake ni kwamba mtendaji/kiongozi awe tayari kukabili tuhuma au pongezi zote zote zitakazoelekezwa katika hilo eneo ambalo huyo mtendaji/kiongozi anasimamia. Je hapa kwetu Tanzania tunafanya hivyo? Viongozi na watendaji wakuu serikalini wanayo hiyo tabia ya uwajibikaji kwa yale yatokeayo kwenye maeneo yao?

  Jibu ni wazi: watendaji wengi hapa Tanzania hawana hiyo tabia ya kuwajibika - mawaziri, wakuu wa mikoa, makatibu wakuu wa wizara, wakuu wa wilaya, wakuu wa mashirika ya umma, wakurugenzi, n.k. Hii inaweza kutafsiriwa kwamba dhana nzima ya utawala bora hapa Tanzania bado ni ndoto. Kulindana kumezidi. Viongozi au watendaji wabovu wamekuwa wakineemeka na kuzidi kupeta kwa kubebwa na wakubwa zaidi yao, huku wachapa kazi wakikashifiwa, kubezwa na kudharauliwa.

  Nadhani mtu anayetakiwa awe mstari wa mbele kuleta mabadiliko ya uwajibikaji ni rais wa nchi. Yeye kikatiba ndiye anateuwa na kuondoa watendaji wakuu wengine wote serikalini na mashirika ya umma. Rais akishafanya
  uzembe kidogo tu katika teuzi zake, basi utendaji wa kazi katika hizo taasisi au wizara unakuwa mbovu, na unaligharimu taifa pesa nyingi kwa njia mbalimbali na kuendeleza ufisadi.

  Uzembe unaweza kufanywa na rais kwa kuteua marafiki, ndugu, jamaa, maswahiba na watu wa aina hiyo ambao hawana sifa za kutekeleza wajibu katika nafasi hizo walizoteuliwa. Kibaya zaidi ni rais anapowaoena aibu kuwawajibisha hao marafiki, ndugu, jamaa, swahiba, n.k. aliowapa dhamana za juu serikalin au mashirika ya umma. Mifano ya watendaji wasiomudu kazi zao ni mingi wakiwemo mawaziri na wakuu wa mashirika ya umma.

  Ni wazi kama rais hawawajibishi wale anaowateua kwa utendaji usiorisha basi naye hawajibiki - kitu kisichotakiwa maana hao wazembe huvuruga nchi na kudidimiza maendeleo. Tuige mifano ya wenzetu wa nchi zilizoendelea, k.m. Japan, Marekani, Uingereza, n.k. ambapo mtendaji/kiongozi huwajibika hata kwa jambo amalo yeye binafsi hakulitenda mradi tu limetendwa na mtu aliyeko chini ya himaya yake.

  Tulie na rais wetu atupe watendaji wazuri wenye kufuata maadili, kuheshimu wananchi, wasio na kashfa zozote, na juu ya yote wenye kuwajibika. Asiwateue tena watu wenye kashfa kama Mh Masha (waziri wa mambo ya ndani), David Mattaka (Mkurugenzi Mkuu wa ATCL), n.k. Tunamtakia rais kazi njema ila aache tabia ya kubeba wasiobebeka, wanaomhujumu.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks but no thanks...

  topic uliyoleta ni ngumu sana kwa uongozi wetu kuanzia mitaani mpaka ikulu... Labda private sector na some NGOs...

  Probably Ubwabwajaji Tanzania would make sense to viongozi

  Duh...
   
Loading...