Uvuvi haramu Ukerewe na uzembe wa serikali

Uvuvi haramu Ukerewe na uzembe wa serikali

MchunguZI

Platinum Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,048
Reaction score
2,239
Hivi karibuni nilikitembelea kisiwa cha ukerewe kwa niya njema kabisa! Kwanza ukiwa mjini Mwanza, kila bidhaa bora ya chakula yaani maembe, samaki, viazi, machungwa, nk. Vyote hutangazwa kwa jina la ukerewe, kwamba vimetoka ukerewe.

Ni kisiwa kizuri sana na sioni ajabu wilaya hii kuweza kuzalisha wasomi lukuki ktk nchi hii. Tatizo kubwa la kisiwa hiki kwa sasa ni chakula kupungua. Hii imetokana na ongezeko la watu waliohamia ili kujipatia maisha bora.

Binafsi nilipenda sana samaki wa ukerewe, lakini naona wamepungua sana na wote munaosikiliza habari, munafahamu matatizo ya uvuvi haramu jinsi unavyoliangamiza ziwa Victoria. Kuna watu wanatumia sumu na wengine nyavu (mitego) iliyozuiliwa. Kwa ufupi nilichokiona ni uzembe wa serikali ktk kusimamia sheria kama ilivyo ktk mbuga za wanayama na madini yetu.

Ukerewe, nimeambiwa na kushuhudia, nyavu haramu zinauzwa na mtu mmoja anayejiita ni maarufu, anaitwa Michael Mugabo. Yeye hajali kwa sababu tu watendaji wa serikali wana bei ndogo na anaweza kuwanunua hata kwa bia. Nasema bei ndogo kwa sababu kwa kiwango chochote, mtu kama Mugabo hana pesa za kumnunua mtu anayejifahamu ubora wake. Kama ilivyojadiliwa bungeni, tatizo la uvuvi haramu nintatizo la serikali siyo la mvuvi. Mtu kama huyu anauza vifaa vilivyozuiliwa kabisa! Nyavu zake haziko dukani lakini kila mvuvi anafahamu anazo ktk stoo ya nje ya duka! Je hili nalo ni gumu kama madawa ya kulevya au serikali dhaifu?

Nchi hii itadhalilika mpaka lini? Hili nalo linahitaji msaada kama wa kulinda tembo? Je, hali ikoje ktk wilaya zingine zinazozunguka ziwa Victoria? Pia kwa walajinwote wa samaki nchini, chukuweni tahadhari. Wakerewe wanaweza tofautisha samaki aliyevuliwa kwa sumu, lakini naamini sisi wengine tulioko Dar hatuwezi. Je, hatuwalishi sumu watoto wetu?
 
Kutokana na msg yako hii naweza kusema, nchi hii ni shimo la taka. Ninachofahamu pia ni kwamba takribani samaki wote wanaouzwa mikoa yetu hii ya Dar, moro, arusha, moshi, nk kote ambako tilapia wanafika, wote wanavuliwa kwa sumu.

Tabia hii ya uvuvi wa sumu inachochewa na wafanyabiashara ambao wanahangaika kutimiza malengo yao ya kibiashara. Kibaya zaidi hakuna muhusika yeyote anayeweza kusema anahangaika na matatizo kama haya. Sasa hivi wako bize na wizi wa pesa ili kushinda uchaguzi, basi!
 
Mchunguzi aliliona hili miaka 10 iliyopita. Ilikuwaje linajitokeza leo hii? Serikali ilikuwa wapi?. Nimekumbuka na kuanza kutafuta achives za JF. Leo hii naweza kusema tatizo lipo, lakini utekelezaji mbovu. Unatumia watu ambao wananeemeka kwa operation. Wanaisaidia serikali kudhibiti uvuvi haramu wakati wao hawana mtu wa kuwadhibiti.
 
Back
Top Bottom