Uvumilivu wa Jacob Zuma, hivi Rais Tanzania angedhalilishwa na kupingwa kiasi hiki ingekuwaje?

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Pamoja na Kuwa Tanzania Wapinzani na Watu wengine wanaikosoa Serikali na Wakati mwingine Rais Moja kwa Moja, Haijatokea Mbunge au Kiongozi mwingine yeyote Kumpinga Rais Kwa Kejeli na Dharau kwa Kiasi hiki, Jujulius Malema alivyomfanyia Rais Zuma tena Mbele yake. Lakini Ninachomheshimu sana Jakob Zuma, Pamoja na Kuwa wana jeshi Kubwa na Polisi wengi kuliko Tanzania, anatabasamu tu na kuacha msemaji ahukumiwe kwa upuuzi wake mwenyewe.

Inakuwaje Tanzania Inakuwaje Wapinzani wanakamatwa hovyo, Mpaka serikali inafuata watu wanachosema Whats app Kusikiliza mazungumzo binafsi na kufuungulia watu Mashitaka. Ingawa siungi mkono kumtuka yeyote labda aanze yeye matusi.

Kungekuwa na Utovu wa Nidhamu wa kiasi hiki, Nisingesema Kitu Kama Watu wangeshitakiwa.

Hebu sikia hii
 
UNAONGELEA TANZANIA IPI..MAANA TANZANIA KAMA MTOTO ANAPITIA HATUA MBALIMBALI ZA UKUAJI NA MABADILIKO MBALIMBALI YAKIWAMO YA VIONGOZI NA KATIBA NA TARATIBU ZA UONGOZI.

MFANO WAKATI WA NYERERE...KUMBUKA YULE GIRIKI ALIYESEMA KAIWEKA SERIKALI MFUKONI

MFANO WAKATI WA MWINYI....RUKSA MPAKA AKACHORWA NA WATOTO WA CHUO KIKUU NA KUZABWA KIBAO NA YULE USTADHI WA DIAMOND JUBILEE

MFANO WAKATI WA MKAPA...MUULIZE JENERALI ULIMWENGU ATAKUAMBIA

MFANO WAKATI WA KIKWETE....KILA MTU ALIKUWA HURU KUMTUKANA NA KUMKASHIFU YEYE AKASEMA HUO NDIO UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MFANO WAKATI HUU....SINA MENGI YA KUSEMA ILA TUNGOJE UKIISHA TUTAKUWA NA NAFASI YA KUUJADILI NA KUONA KAMA KWELI UMEFIKIA AU UKO CHINI YA VIGEZO VYA JACOB ZUMA.
 
Mbona rais wetu mstaafu alikuwa akiporomoshewa zaidi hivi.ndani na nje ya bunge.
 
Mi hata sijui nchi yetu inaelekea wapi?;

Watu tumejawa na uoga hata wa kitetea haki zetu!

Nani hajui Lowassa anatukanwa na wanasiasa tena majukwaani! Mbona hawafunguliwi mashtaka? Sana sana wanapewa vyeo kama zawadi kwa matusi yao!

Nani hakumsikia Mzee mkapa alivyowaita watu nanukuu ' Malofa, Wapumbavu' na hakuna aliyekemea, sana sana tuliona watu wakipiga makofi na kushangilia

Hii Sheria imetungwa kwa ajili watu gani?
 
kuhusu lowasa kutukanwa, nadhani ni yeye hajaamua kuwashitaki wanao mtukana. Ila sheria ina mruhusu kuwashitaki. Kwa mtazamo wangu nadhani kuna njia nzur za kufikisha ujumbe na ukaeleweka bila ya kumtukana mtu.
 
Pamoja na Kuwa Tanzania Wapinzani na Watu wengine wanaikosoa Serikali na Wakati mwingine Rais Moja kwa Moja, Haijatokea Mbunge au Kiongozi mwingine yeyote Kumpinga Rais Kwa Kejeli na Dharau kwa Kiasi hiki, Jujulius Malema alivyomfanyia Rais Zuma tena Mbele yake. Lakini Ninachomheshimu sana Jakob Zuma, Pamoja na Kuwa wana jeshi Kubwa na Polisi wengi kuliko Tanzania, anatabasamu tu na kuacha msemaji ahukumiwe kwa upuuzi wake mwenyewe.

Inakuwaje Tanzania Inakuwaje Wapinzani wanakamatwa hovyo, Mpaka serikali inafuata watu wanachosema Whats app Kusikiliza mazungumzo binafsi na kufuungulia watu Mashitaka. Ingawa siungi mkono kumtuka yeyote labda aanze yeye matusi.

Kungekuwa na Utovu wa Nidhamu wa kiasi hiki, Nisingesema Kitu Kama Watu wangeshitakiwa.

Hebu sikia hii

Kila jambo lina wakati wake, hata hivyo haitoshi tu kutumia yaliyotokea S.A kuhukumu yanayotokea TZ, ni nchi mbili zenye historia tofauti na mifumo ya uendeshaji wa siasa zao ni tofauti pia.
 
Pamoja na Kuwa Tanzania Wapinzani na Watu wengine wanaikosoa Serikali na Wakati mwingine Rais Moja kwa Moja, Haijatokea Mbunge au Kiongozi mwingine yeyote Kumpinga Rais Kwa Kejeli na Dharau kwa Kiasi hiki, Jujulius Malema alivyomfanyia Rais Zuma tena Mbele yake. Lakini Ninachomheshimu sana Jakob Zuma, Pamoja na Kuwa wana jeshi Kubwa na Polisi wengi kuliko Tanzania, anatabasamu tu na kuacha msemaji ahukumiwe kwa upuuzi wake mwenyewe.

Inakuwaje Tanzania Inakuwaje Wapinzani wanakamatwa hovyo, Mpaka serikali inafuata watu wanachosema Whats app Kusikiliza mazungumzo binafsi na kufuungulia watu Mashitaka. Ingawa siungi mkono kumtuka yeyote labda aanze yeye matusi.

Kungekuwa na Utovu wa Nidhamu wa kiasi hiki, Nisingesema Kitu Kama Watu wangeshitakiwa.

Hebu sikia hii
hihihiihihih hajatukanwa kaambiwa ila ukweli ila haya baadhi ya haya maneno yanamfaa j...............k.......................t............................................. tcra dont kill me
 
Inakuwaje Tanzania Inakuwaje Wapinzani wanakamatwa hovyo, Mpaka serikali inafuata watu wanachosema Whats app Kusikiliza mazungumzo binafsi na kufuungulia watu Mashitaka. Ingawa siungi mkono kumtuka yeyote labda aanze yeye matusi.

Kungekuwa na Utovu wa Nidhamu wa kiasi hiki, Nisingesema Kitu Kama Watu wangeshitakiwa.

Huwa najiuliza, hivi Magufuli mwenyewe huwa anajali sana kuhusu hayo "matusi" yanayotolewa au watu wanafuatiliwa kutokana na kimbelembele tu cha baadhi ya taasisi na watu kutaka kujipendekeza kwa Magufuli?

Na ikiwa ni kweli Magufuli anajali sana suala la "matusi", iweje wakati wa kampeni matusi mabaya yalikuwa yakitolewa kwa Lowasa na wala hakuonekana kulitilia uzito jambo hilo au hata kusema si vema watu wa CCM kufanya hivyo?

Na pia, hawa watu walio kimbelembele kufuatilia "matusi" yanayotolewa, kwa nini hatuoni wakitoa tamko au kuchukua hatua kwa "matusi" yanayotolewa dhidi ya vyama vya upinzani na wanachama wao?

Nachukia sana watu wanaofanya kazi kwa kujipendekeza kwa Magufuli. Natamani niwatukane matusi ya nguoni kabisa. Watu wanaacha kutumia fedha za umma kupambana na mitandao ya ujambazi wanahangaika kufuatilia sijui nani kasema nini kwenye WhasApp sijui. Ujima wa ajabu sana huu.

Mnapoteza nguvu na wakati (resources) katika vitu vidogo visivyo na mchango wa maana kwa wananchi ili tu mjionyeshe kwa raisi, na kuacha wananchi wakihangaishwa na majambazi na mitandao ya kitapeli ya internet. Mngetumia nguvu hizo kutafuta majambazi au kukomesha utapeli wa ki-electronic tungefika mbali sana. Ovyo kabisa kufanya kazi ili kujipendekeza kwa mtu.
 
Hapana Wapinzani wa South Afrika Ni hovyo sana, Hawana heshima wala adabu wala Staha, Tukifikia hapo Hutanisikia nikitetea Democrasia ya Namna hiyo hata kama CCM wakileta Vifaru Bungeni, au Kama Sio CCM chama chochote tawala hakiwezi kuongoza nchi kikiruhusu Uhuni wa Namna hii. Hata kama unachotetea ni sawa, Please sio kama hivi.

Naona Jacob Zuma Upole wake Umepitiliza!
 
Huwa najiuliza, hivi Magufuli mwenyewe huwa anajali sana kuhusu hayo "matusi" yanayotolewa au watu wanafuatiliwa kutokana na kimbelembele tu cha baadhi ya taasisi na watu kutaka kujipendekeza kwa Magufuli?

Na ikiwa ni kweli Magufuli anajali sana suala la "matusi", iweje wakati wa kampeni matusi mabaya yalikuwa yakitolewa kwa Lowasa na wala hakuonekana kulitilia uzito jambo hilo au hata kusema si vema watu wa CCM kufanya hivyo?

Na pia, hawa watu walio kimbelembele kufuatilia "matusi" yanayotolewa, kwa nini hatuoni wakitoa tamko au kuchukua hatua kwa "matusi" yanayotolewa dhidi ya vyama vya upinzani na wanachama wao?

Nachukia sana watu wanaofanya kazi kwa kujipendekeza kwa Magufuli. Natamani niwatukane matusi ya nguoni kabisa. Na hili suala la "matusi" limechukua sura mpya katika watu kujipendekeza kwa raisi.

Nilipingana sana na Matusi hayo Na nilipinga Mh. Magufuli kwa Kutokemea Matusi yale.

hahahahahaah huyu kijana anautani sana. Naona Zuma anacheka tu. Siasa wakati mwingine ni kuwa mpole
 
Zuma anajijua kuwa yeye ni mchafu,unafikiri Zuma atasema nini?

Ovaa
Lakini sio Bungeni Umwadress Rais Vile, Hata kama Unampinga, stick kwenye Utendaji wake, sio Maneno ambayo akiinuka na Kukupa Mkono(mtakatifu) Watu wataona umestahili
 
Back
Top Bottom