Uvujishaji siri za Serikali: Profesa Muhongo mtegoni

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
22,988
Reaction score
27,924
Haya kumekucha Prof Muhongo matatani tena ahusika na kumtumia meseji yule mama mkurugenzi wa wakala wa vipimo.Mkurugenzi amtaja live uliambiwa hili ni jipu, ukakataa linakutumbukia asubuhi mapema.

Kazi kwako sasa

===================


Chanzo: Mtanzania
 
Pamoja yote yalotukia huko nyuma kuhusu huyu mtu, mkulu hakusikia wala kuona, tusubir Na tuone hatua gani atachukua dhidi yake
 
Hii inayoingiza mafuta ni ya,,,,,,,......what,next nilimsikia askofu shoo akisema majipu yatumbuliwe kwa haki,tujiulize ni kwa nini anatanguliza sms???
 
Hahaaaa.. alitaka kumunusuru best yake asitumbuliwe sivyo... Kazi kweli kweli.

Me huyu jamaa nilichomchukia nikuwaambia Watanzania wakauze juice. Kwamba nchi itajengwa na wageni...ujinga mtupu.

Wenzetu wanapewa vipaumbele kuinua taifa lao na rasilimali zinawafaidisha wao. Sisi tunaishia kufaidisha wageni tu. Sijui hata watu wana matatizo gani vichwani mwao.
 
Apo chacha tuone...maana limejivumbua lenyewee nione sasa iz this makufuli serious with his work.
 
Mbona watu wote huwa tunatumiana SMS?, acheni hizo, huyo mama alikosa point ya kujitetea akaona amsingizie mzee wa watu
 
Nadhani alitaka kumsaidia yule mama MWIJARUBI, naona jina linafanana na jina la kati la mwenyewe Muhongo.
 
siku ya kufa nyani miti yote huteleza....huu msemo una maana kubwa sana! hata iweje utaumbuka tuu
 
Kauli ya membe inatimia kuwa jpm anawatumbua watumishi ambao hajawateua yeye na tuone atakao wateu yeye majaliwa alisema apewa jina la aliye tuma sms haya kapewa jina waonyeshe misuli sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…