Uvivu wamuumbua!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,422
976
Jamaa akiwa amepiga suti nyeupe,alikuwa akisafiri kwa mguu kuelekea kijijini kwa wakwe zake pamoja na mkewe.Jamaa alibanwa na mkojo lakini akaona uvivu kuchepuka porini kukojoa,akaamua kujikaza mpaka afike.Zikiwa zimebaki hatua 100 kufika ukweni mara wingu zito likafunga na matone mazito ya mvua yakaanza kudondoka.Jamaa akaamua ajikojolee nguoni akiamini mvua itakayomnyeshea itasafisha mkojo wote aliojikojolea.Alipomaliza tu kujikojolea,mvua nayo ikakata hapo hapo tena ghafla akabaki na bonge la ramani kubwa ya mkojo sehemu za mbele ya suruali.
 

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,422
976
Mvuta bangi mmoja baada ya baada ya kupata cha Malawi aliamua kumwomba mtoto wake wa miaka mitatu amsindikize dukani.Yule mtoto alikataa kumsindikiza.Jamaa akaanza kulia kwa uchungu huku akimwambia yule mtoto;haya,si hutaki kunisindikiza dukani,kuanzia leo mimi sio ndugu yako tena,udugu wetu uishe leo!
 

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,422
976
Mvuta bangi mwingine aliamua kumfundisha mkewe kuvuta bangi.Mara ya kumvutisha bangi mke wake,jamaa akaenda kupumzika kibarazani.Mara ghafla akamuona mkewe anakimbilia getini huku kamshika mtoto wao mdogo kichwa chini miguu juu akiwa na kisu mkononi.Alipomuuliza mkewe anataka kufanya nini,wife akajibu;naenda nje kumchinja huyu kuku!.Jamaa akamdaka mkewe na kumrudisha ndani na toka siku hiyo ikawa ndo mwisho wa kuvuta bangi.
 

valid statement

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
2,843
835
Mtu mwenye upeo kama huu ni wa kumpima kama yuko mzima kiakili!Vinginevo anaweza hata akanya kwenye pot la mtoto akampa mkwewe akamwage chooni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom