Uvivu wa kufikiri na ushabiki wa kijinga wa hii Timu ndio Mahdi zetu

sizonjemadawa

JF-Expert Member
Feb 11, 2017
1,057
2,000
Kufahuru mtihani ni jambo moja na kuweza kugundua mambo ni jambo jingine,

Hii timu imeongoza tangu mwanzo hadi leo hii, bado inaongoza tu, mambo yote yanashughulikia hii Timu, kuna watu kwenye Timu wameliingiza taifa kwenye hassara kubwa, ambazo timu pinzani zilizipigia kelele sana wakatumia uwingi wao kuzima hayo yote,

Kuna watu kwenye Timu wametajwa kuwa wameliingiza taifa kwenye hassara, kwa kusain mikataba mibovu, watu haohao wanasimama na kumpongeza kiongozi wao, na mashabiki bila kufikilia wanafuata tu, kwa Nini mashabiki hawahoji swala la kuchukuliwa hatua watu wote waliotajwa na sasa wanabadilisha mada kuwa pongezi,

Ni mtu aliyechanganyikiwa peke yake atakayeungana na mwalifu ili kumtetea kiongozi ambaye hajamchukulia hatua mwalifu anayempongeza, huu ni wakati wa kuwageukia wabunge wote na kuwauliza kwa nini walikuwa wanasema ndiooo, kwa mikataba ya dharula, tuache ushabiki pembeni, uccm na uchadema + ucuf ndio Matunda wa haya yote, wangekuwa wanawasikiliza na kujadili hoja leo naamini tusingefika Huku, nani ambaye hajui kuwa upinzani walipigia Kelele mikataba wakapuuzwa na wabunge wa ccm na mashabiki wao kwa ujumla, hakuna aliyeunga mkono, nafikiri wakati ndio sasa kuwageukia wabunge na kuwauliza zile ndio inamaana mlikuwa hamsomi mnaitikia tu, ili wawe makini, waache kujadili pongezi Bali wajadili watu waliotajwa wafanywe nini, waadhimie wachukuliwe hatua ili wengine iwe fundisho, siyo wanakuja kutisahaulisha na swala la pongezi kwa mkulu, na kumwita Tundulisu siyo mzalendo,

Mnashindwa kujiuliza prof: anashindwaje kugundua kuwa huu mkataba siyo rafiki kwa miaka yote, leo hii mnaungana nao kumpongeza mtu ambaye hajawachukulia hatua, mnakuja kuwaita chadema cyo wazalendo, wakati hawajawai hata kutia saini kwenye mkataba, nilifikiri mtawaiata wanachama Wenu wote waliosababisha haya na kuwapa adhabu, ndio kwanza mnakuja kumtafuta Mchawi upinzani wakati wachawi mnaishi nao huko huko mnakosifiana

[HASHTAG]#sipingi[/HASHTAG] juhud za mh: Rais bali najiuliza mawazo ya kundi lake la ndiooo#
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom