Uvimbe kwenye uume

malaika wa motoni

Senior Member
Jul 28, 2016
131
102
Salaam.

Kama kama kichwa cha habari kinavyojieleza kuna Rafiki angu anaomba msaada wa kitabibu, anasema Tangu achepuke na mchepuko wake wa siku zote jmos ya tarehe 4 feb 2017, amepatwa na uvimbe sijui kipele, (kishimo) chenye maumivu makali kabla ya kichwa cha uume. Alipojaribu kupasua kulitokea particles zenye harufu mbaya sana, na baada ya masaa kadhaa ni kama ule uvimbe unarud mpya tena na usaa(Refill) akaamua kuwasiliana na Jamaa mmoja wa pharmacy kubwa hapo Mwanza na kumwelezea situation jamaa akamwambia yatakuwa magonjwa ya zinaa yan Male genital herpes(malenge lenge) so atafute dawa zifuatazo; Azithromycin, Aciclovir tables pamoja na Tube yake. Jamaa akanza dozi hadi leo ni siku tano hakuna mabadiliko yoyote akaamua kwenda maabara kuchek kipimo cha syphillis (RPR) wakakuta ni NEGATIVE. Jamaa wa Lab ikabid amwambie aende Hospital kaenda hospital na kuonana na Dr baada ya doctor kumfanyia oral diagnosis akasema hyo haiwez kuwa Viral infections, ila watakuwa bacteria so Dr naye aka suggest dawa zake za Antibiotics( Cipro, Doxycycline, Metronidazole, na Topical Mupirocin (Tube) jamaa amechanganyikiwa je aanze hii Dozi mpya..!!?

Kwa Mwenye utaalam naomba tumsaidie huyu mtu, mana haya maji maji(usaa) yanayotoka
Kwenye hizi vidonda yanamtesa sna.

Nomba kuwasilisha..
 
magonjwa ya zinaa mnayapataje? acheni zinaa au tumieni condom
afate ushauri wa daktari na sio pharmacy!ina maana hujui tofauti ya daktari na mpharmasia
Wafamasia wanapitia mafunzo ya magonjwa ya mwili na wanasaidia sana, kwa baadhi ya matatizo wanakupa ushauri wa dawa za kutumia, lakini hili tatizo la mkuu ni kubwa kumalizwa na mfamasia, anahitaji vipimo Zaidi.
 
mwambie afuate ushauri wa daktari na kama vipi na mkewe ampime na mchepuko upimwe wapate dozi wote ila kama anafanya kwa siri ooh ohooooo
 
We jamaaa acha kumsingia mwenziwe, we sema tu ni mimi naumwa, mbona kujikwaa ni kawaida:):):):):):):):)
Tena ukisema ni wewe utaisaidiwa more than 100%. Anyway keep along na maelekezo aliyokupa docta.
Pia kupona kkunahitaji muda, endelea kutumia hizo dawa for 5 days hope will see changes.
Pole sana
 
Mkuu Baada Ya Muda Fulani Huyo Dude Mwenye Kidonda Anakatika Kipande na Utabaki na Kibamia.... Kwahiyo Wahi Kwa Dokta Haraka Sana before too late....
 
We jamaaa acha kumsingia mwenziwe, we sema tu ni mimi naumwa, mbona kujikwaa ni kawaida:):):):):):):):)
Tena ukisema ni wewe utaisaidiwa more than 100%. Anyway keep along na maelekezo aliyokupa docta.
Pia kupona kkunahitaji muda, endelea kutumia hizo dawa for 5 days hope will see changes.
Pole sana

Hapana me ni messenger tu mkuu..
 
Duu pole sana jamaa angu.sema nini tumia hiyo dozi uliyoandikiwa na dr ni tiba sahihi kw Tatizo hilo.tena sio wewe wa kwanza kupatwa na tatizo hilo na dawa hiyo ndio tiba yake.
 
Tuambie upo mkoa gani tukuelekeze kwa wataalam,kumbuka magonjwa ya zinaa yamekuwa sugu sana siku hizi ndiomana huwezi kupewa dozi ya aina moja tu tena nyepesi na ukapona.kadili unavyochelewa matibabu ndio ugonjwa unazidi kujiimarishana kuharibu viungo vyako.
 
Jamaa yupo Mwanza..
 
Back
Top Bottom