Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mbeya- Ndugu Amani Kajuna amezindua mashina ya wakereketwa na wanachama wa UVCCM Mbeya mjini.
Harakati hizo za Mwenyekiti huyo wa Vijana zinaashiria kutekelezwa kwa mkakati wa "fukuza Sugu, dumisha Amani Mbeya" ambao umeasisiwa na Vijana wa Mbeya chini ya uratibu wa Mwenyekiti huyo wa UVCCM.
Matawi hayo yatakayozinduliwa kila mtaa wa Mbeya mjini yatakuwa ni vituo maalum vya utekelezaji wa mkakati wa kulirudisha jimbo la Mbeya mjini kwa Chama Cha Mapinduzi.
Tangu kuanza kwa utekelezaji wa Mkakati huo, tayari mashina zaidi ya kumi na tano (15) yameshazinduliwa na kwamba vijana wameshajiweka vyema kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kunalirudisha jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Kwa jinsi hali ilivyo kwa sasa Mbeya mjini, inaonyesha kila dalili ya kuwa mwisho wa zama za Sugu na Nondo ndani ya Mbeya zimeisha.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndugu Amani Kajuna akifungua tawi la Mpugusu la wakereketwa wa Umoja huo Mkoani Mbeya.
Hivi ndivyo hali ilivyo katika mitaa ya Mbeya mjini, Vijana watanda mitaa yote wakihamasisha Amani na kuonyesha Ukakamavu wa Vijana wa CCM.
Wananchi wa Mbeya wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Mwenyekiti wa Vijana wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Amani Kajuna. Hakika Mbeya imesimama na Amani.