UVCCM yawaonya vibaraka wanaowania Urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM yawaonya vibaraka wanaowania Urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Sep 10, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umesema hautasita kumuengua mgombea yeyote atakayebainika kutumiwa na makundi yanayodaiwa kuwania urais ndani ya chama hicho mwaka 2015.
  Katibu Mkuu wa Umoja huo, Martin Shigela alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya CCM mjini hapa na kubainisha kuwa iwapo kuna mtu aliyeingia kwa lengo hilo, ajiondoe mapema kabla hajabainika.
  "Hatutasita kumuengua mgombea yeyote atakayebainika kutumiwa kugombea nafasi ya uongozi ndani ya UVCCM na makundi yanayodaiwa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015," alisema Shigela.
  Hivi sasa kunaendelea usaili na kupitia fomu za wagombea wa nafasi mbalimbali za jumuiya hiyo, huku kukiwa na tetesi kuwa baadhi ya wagombea wanawania nafasi katika umoja huo kwa lengo la kutumiwa na baadhi ya vigogo wa CCM wanaotajwa kuwania nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.
  Shigela alisema Kamati ya Utekelezaji inakutana mjini hapa kwa lengo la kuchuja wagombea na anaamini kazi hiyo itakwenda vizuri kama walivyotarajiwa kwani katika uchaguzi wa ndani wa CCM kuanzia ngazi ya Kata hadi Wilaya, ulifanikiwa kwa asilimia 90 na zitakamilika kwa kipindi kifupi kijacho.
  Alisema watakuwa wakiweka alama kulingana na sifa, historia ya mgombea na uwezo wake wa uongozi ndani ya chama kwa lengo la kuhakikisha wanapata viongozi wazuri watakaokisaidia chama.
  "Kazi kubwa inayofanyika hapa ni kupitia fomu za wagombea na pili kuwahoji kwa miaka mitano ijayo watakifanyia nini chama na majina yote tutayapeleka Halmashauri Kuu pamoja na alama zake" alisema.
  Alisema vijana wengi wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali ngazi ya Mkoa na Taifa na kazi inayoendelea ni kuweka alama kwa ajili ya kuwapendekeza wagombea kwenye kikao kitakachokaa Septemba 12 na 13 mwaka huu na majina hayo yatapelekwa Baraza Kuu.
  Alisema baada ya Baraza Kuu kupitia itatoa mapendekezo, Halmashauri Kuu ambayo itatoa majina kwenda kwenye Mkutano Mkuu wa UVCCM ambao utafanyika Oktoba.

  CHANZO: GUMZO LA JIJI
   
 2. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Martin Shigella hajatimiza 40 yet? Same song kila siku, Yetu macho tunasubiri vitendo
   
 3. Warue

  Warue Senior Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 150
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Hii ni mizengwe tu!, wenyewe wana watu wao tayari. kwa habari rasmi hakukuwa na suala la kuhojiwa zaidi ya kuonyesha vyeti na pita.............
   
 4. C

  Concrete JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hakuna lolote ni ngonjera tupu, tena tumeshazichoka.
  UVCCM ilishakufa zamani sasa imebaki mizoga mitupu inayotumiwa na mafisadi.

  Huyo Martin Shigella ni mzee anayejifanya kijana, yeye hana habari kwamba wagombea wote wa nafasi za juu wa UVCCM ni project za wagombea urais wa CCM.

  Embu atuambie ni sheria au kanuni ipi inakataza mgombea wa UVCCM kupigiwa debe na vigogo wanaowania urais?

  Hili ndio tatizo la kukariri ngonjera za propaganda. Propaganda za magamba zimewaharibu kabisa, wamekuwa kama machizi vile, hawawezi tena kufikiri wenyewe.

  UVCCM imekuwa ni kijiwe cha vijana kwenda kutongozana tu, utawaona wako busy wakati wa kugombea tu. Ni uchafu mtupu.
   
 5. C

  Concrete JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hizi ndizo idara za kufuta ndani ya CCM, zinaongeza gharama tu, ruzuku ya chama imepungua sana, halafu hawa jamaa UVCCM bado wapo tu.

  Hawana msaada wowote kwa chama kipindi hiki, zaidi ya kula posho, kutumiwa kama Condom na kufamya umalaya tu.

  Wakati wa usaili ni bora wakapimana ngoma kabisa hii itawasaidia sana kuliko kukazania kuzungumzia mambo ya kufikirika tu.
   
 6. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Malisa yuko wapi? Ama ameachana na siasa uchwara? Katika vijana wa UVCCM wana busara nasi waropokaji ni Malisa na Bashe.
   
 7. k

  kwitega Senior Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yote hayo ni matap tap tu hakuna cha busha wala melisa
   
 8. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  shegella aache unafiki mara moja kwani hakuna mwana ccm ambaye hana kundi.hata yeye shegella ana kundi lake analolitumikia kwa kujua au kutokujua.
   
Loading...