UVCCM yaicharukia serikali

AK-47

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2009
Posts
1,373
Reaction score
202
UVCCM leo wameonyesha ukomavu wa hali ya juu na kuguswa na maslahi ya taifa baada ya kutoa matamko kadhaa likiwemo la kuitaka serikali kuwataja hadharani wamiliki wa Richmond ili wabebe mzigo wa kuilipa Dowans sh bilioni 94 inayodai Tanesco. Aidha wametaka bodi ya mikopo ivunjwe kwa kuwa imeshindwa kazi kiasi cha kuzusha maandamano ya wanafunzi wa vyuo kila kukicha. Kama haitoshi wameitaka serikali kutoa ajira kwa vijana badala ya kuacha hali ilivyo sasa ambapo vijana wengi wapo mitaani hawana ajira jambo ambalo ni hatari.
 
:amen::amen::amen::amen: Kama ni habari ya ukweli
 
Nyie UV-CCM nani kawafungua midomo au ni kukosa mgao wa Dowans? Well, let's hope kelele za mlango safari hii zitamfikia mwenyekigoda wa chama pale magogoni. We're watching every move you make, just to make sure your current noise is not for the sake of gaining popularity.
 
Kama habari hii niya kweli basi ni vizuri endeleeni kutwangana wenyewe kwa wenyewe ili 2015 iwe rahisi kuwang'oa..... ila angalizo: Mmeona vijana wamejitenga na ninyi mwaka huu sasa mnafikiri mnaweza kubadili mawazo yao kwa porojo zenu!!!:frusty:
 
Watubu wahamie huku kwetu tupambane wote
 
propaganda
 
yes hii habari niyakweli nimeisikia sasa hivi ikirushwa na dotchvelle hapa wapo redio
 

Eeeeehhhhh na nyie, kelele huko!!! Siku zote mlikua wapi wakati yote haya yakitendeka??

Au mnajitokeza leo kwa sababu mmegundua UCHOYO WA WAZEE WENU huko ndani ya CCM walivyoamua kuishi kama vile dunia inaisha leo ndio mkagutuka kwamba NYINYI KAMA VIJANA WENZETU MNACHUUZWA na wazee hao na ndoto zenu kuja kutuongoza kuendelea kuyoyoma sio?????????????

Hebu kaanzeni na (i) kukemea Uchakachuaji wa kura 2010 kwanza, (ii) mkapitie masuala ya mikataba yote na kuturejeshea kodi zetu zilizotafunwa kimazingaombwe, (iii) mkaikemee CCM kutugawa Taifa la Tanzania kwa misingi ya kidini kama mbinu yenu kisiasa, ndio hapo baadaye mje tuzungumze.
 
Kiukweli nimeona hapa TBC jinsi hawa UVCCM walivyotoa tamko lao nawapa pongezi kwa kuonesha uzalendo kumbe si kila mwana ccm ameoza:A S thumbs_up::tea:
 
nasema hivi vijana tunataka mitaji si ajira, bodi ya mikopo iboreshwe na si kuvunjwa na pia dowans wamiliki wa dowans wafutiwe uraia na kufilisiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…