UVCCM: Tutalinda heshima ya nchi kwa gharama

UVCCM: Tutalinda heshima ya nchi kwa gharama

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amesema Vijana wa umoja huo wapo tayari kulinda heshima ya Tanzania kwa gharama yoyote dhidi ya vibaraka wanaochafua taswira ya nchi kwa lengo la kuwanufaisha Mabeberu.

Amesema matumaini yaliyorejeshwa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, lazima yalindwe kwani jasho la uhuru, demokrasia, muungano na maendeleo ya Taifa, CCM ndio wenye uchungu nalo.

Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa katika kupigania maslahi ya nchi yapo makundi yatakayoibuka kupinga hivyo lazima vijana wakae tayari kupambana dhidi ya vibaraka na mapambano hayo hayatorudi nyuma.

Kheri alitoa msimamo huo jana wakati akizungumza na Vijana na wanachama wa UVCCM mkoani Dodoma, ambapo ameeleza kuanzia sasa endapo akiibuka mtu mwenye ujasiri wa kutukana, vijana hawatatukana bali watafanya litakaloonekana linafaa kwa maslahi ya Taifa.

Alisema Vijana wa CCM wanafahamu wapi nchi ilipotoka na inapokwenda sasa wanapaswa kujitokeza kwa kauli na vitendo kulinda heshima ya nchi na viongozi.

Mwenyekiti huyo wa UVCCM alisema Serikali imekuwa ikitenga mabilioni ya fedha kugharamia miradi ya maendeleo lakini lipo kundi la Watu linakejeri hakuna kitu kinachofanyika.

Kheri alisema kuanzia sasa endapo akiibuka mtu mwenye ujasiri wa kutukana, vijana hawatotukana bali watafanya litakaloonekana linafaa kwa maslahi ya Taifa.

Aliwataka Vijana wa CCM kuwaonyesha Watu wa namna hiyo kuwa wapo tayari kuilinda nchi kwani uzalendo ni kuipigania serikali na chama.

Alisema hakuna mahali ukaitenganisha CCM na mema na historia ya nchi kwani uhuru, muungano, heshima, vyama vingi, demokrasia na mendeleo yamepatikana kutokana na busara ya viongozi wa CCM.

Mwenyekiti huyo alisema tabia ya Wanasiasa kusema uchaguzi ulikuwa huru ni pale anaposhinda na unageuka batili pindi anaposhindwa huo ni ufu wa fikra.

Aliwataka Vijana kuendelea kuhamasisha Wananchi kujiunga na CCM kwani hakuna chama kinachotoa uhuru na demokrasia kwa Watu wa kawaida kama CCM.

Chanzo: Gazeti la Uhuru


IMG-20180327-WA0473.jpg

 
Back
Top Bottom