UVCCM Taifa hakukaliki M/kiti kung'olewa?

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
Hali imeendelea kuwa tete ndani ya Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM), huku jumuiya hiyo ikitengua uteuzi wa wakuu watatu wa idara zake ambao walikataliwa na Baraza Kuu la chombo hicho lililokutana hivi karibuni, Visiwani Zanzibar.

Wakati hayo yakiendelea kuna na taarifa kwamba kumekuwa na mwendelezo wa harakati za kuandaa mkakati wa kumwondoa madarakani mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Sadifa Juma Khamis na kwamba vikao vya kupanga mkakati huo vilianza mara tu baada ya mkutano wa Zanzibar.

Watendaji waliosimamishwa ni Wakuu wa Idara za Oganaizesheni, Tumaini Mwakasege, Fedha na Uchumi, Omary Suleiman na yule wa Idara ya Chipukizi na Uhamasishaji, Omary Justus.

Chanzo: Mwananchi
 
Wapo katika mikakati ya kukiimarisha chama tu;
 
Last edited by a moderator:
Hivi hawa vijana wamelelewa vya kutosha na Chama au wamejiunga kwa utaratibu wa Crashing Programe!
 
et mwenyekiti umesema send off ifanyike kwa jirani yake wanauliza yupi. Harusi ni hotel ya nyota 3 au 2 waalikwa wanauliza na muda ni asb au alifajiri
 
hivi hawa vijana wamelelewa vya kutosha na chama au wamejiunga kwa utaratibu wa crashing programe!

utawaweza vijana wetu hawa? Ndo viongozi lakini! Kitu factory inatoa viongozi wa kesho mh! Kina napemh! Shigela mh!kazi ipo
 
wakati UVCCM wako busy kubamizana, sisi tuko busy na M4C.
 
Mwaka jana tulionya juu ya mipango iliyoratibiwa na akija Ben Saanane wakishirikiana na baadhi ya wagombea kwa lengo la kuivuruga UVCCM huko baadae.Tulipeleka hadi ushahidi kwa katibu mkuu Wilson Mukama pamoja na majina ya wagombea waliokua wakishirikiana na vijana wa upinzani wawasaidie kushinda uchaguzi hadi leo kimya.Kinachitokea UVCCM sasa hivi ni matokeo ya makundi na mengine yakisaidiwa kimkakati na vijana wa upinzani.Zile tuhuma za mwanadada Eddah Kishimba na Martine Shigella ambazo Ben aliweka humu bado mchezo unaendelea.Turudishe chama kwa wakulima na wafanyakazi.Tuache tabia ya unafiki,uhuni na kusalitiana kwa kuwa hakuna atakayesalimika
 
ukisikia tu UVCCM imeandikwa basi ujue ni kung'oana , ugomvi wa posho au pesa imepotea ! Hivi haiwezekani UVCCM kuendesha hata kongamano la kimataifa ? SHAME !
 
Ccm piga kote kote hadi wauwaji wasambaratike
 
ukisikia tu Uvccm imeandikwa basi ujue ni kung'oana , ugomvi wa posho au pesa imepotea ! Hivi haiwezekani uvccm kuendesha hata kongamano la kimataifa ? SHAME !
Viongozi wengi wa UVCCM wanachowaza ni lini watateuliwa kuwa ma-DC, ma-RC simply wanachowaza ni madaraka tu hakuna cha maendeleo.
 
CCM ni chama imara, hakiendeshwi kwa magazeti wala tararira. Hayo ni masuala ya kiutendaji tu. Walishaondolewa makm wa rais na mawaziri na ccm ikabaki kuwa imara sembuse sadifa bana
 
Viongozi wengi wa UVCCM wanachowaza ni lini watateuliwa kuwa ma-DC, ma-RC simply wanachowaza ni madaraka tu hakuna cha maendeleo.

wakati huohuo bavicha wanawaza kumwagia watu tindikali na kuwalisha sumu.. Refer igunga kesi with henry kileo, ben saanane kesi na lwakatare sagal
 
CHADEMA ni wafu watembeao, CCM haiwezi kusambaratika kwa sababu ya mwenyekiti wa vijana
 
wakati huohuo bavicha wanawaza kumwagia watu tindikali na kuwalisha sumu.. Refer igunga kesi with henry kileo, ben saanane kesi na lwakatare sagal

Chadema ni wafu watembeao, ccm haiwezi kusambaratika kwa sababu ya mwenyekiti wa vijana
CHADEMAimeingiaje hapa nyie mtetee mauchafu yenu wenyewe waacheni BAVICHA wajenge chama chao.
 
Hivi hilo kundi bado ni Nguzo ya chama chetu hiki?
Mwaka jana tulionya juu ya mipango iliyoratibiwa na akija Ben Saanane wakishirikiana na baadhi ya wagombea kwa lengo la kuivuruga UVCCM huko baadae.Tulipeleka hadi ushahidi kwa katibu mkuu Wilson Mukama pamoja na majina ya wagombea waliokua wakishirikiana na vijana wa upinzani wawasaidie kushinda uchaguzi hadi leo kimya.Kinachitokea UVCCM sasa hivi ni matokeo ya makundi na mengine yakisaidiwa kimkakati na vijana wa upinzani.Zile tuhuma za mwanadada Eddah Kishimba na Martine Shigella ambazo Ben aliweka humu bado mchezo unaendelea.Turudishe chama kwa wakulima na wafanyakazi.Tuache tabia ya unafiki,uhuni na kusalitiana kwa kuwa hakuna atakayesalimika
 
UVCC ni genge la wahuni na waporaji,maana vijana siku hizi hawataki kufanya kazi wamekalia ukuwadi wa kisiasa,hiyo ndio UVCCM ambayo tunategemea kupata viongozi wa taifa letu,si mnamuona NAPE alivyo ndio zao halisi la UVCC
 
Mwaka jana tulionya juu ya mipango iliyoratibiwa na akija Ben Saanane wakishirikiana na baadhi ya wagombea kwa lengo la kuivuruga UVCCM huko baadae.Tulipeleka hadi ushahidi kwa katibu mkuu Wilson Mukama pamoja na majina ya wagombea waliokua wakishirikiana na vijana wa upinzani wawasaidie kushinda uchaguzi hadi leo kimya.Kinachitokea UVCCM sasa hivi ni matokeo ya makundi na mengine yakisaidiwa kimkakati na vijana wa upinzani.Zile tuhuma za mwanadada Eddah Kishimba na Martine Shigella ambazo Ben aliweka humu bado mchezo unaendelea.Turudishe chama kwa wakulima na wafanyakazi.Tuache tabia ya unafiki,uhuni na kusalitiana kwa kuwa hakuna atakayesalimika
Ben Saanane na UVCCM? anashiriki katika siasa za maji machafu? Its hard to believe
 
Back
Top Bottom